Nenda kwa yaliyomo

Chui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chui
Chui juu ya tawi
Chui juu ya tawi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Felidae (Wanyama walio na mnasaba na paka)
Nusufamilia: Pantherinae (Wanyama wanaofanana na chui)
Jenasi: Panthera
Spishi: P. pardus
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nususpishi 8:

Jina la kibiolojia Panthera pardus Linnaeus, 1758

Nususpishi

[hariri | hariri chanzo]

Tabia za umbo lake

[hariri | hariri chanzo]
Jike la chui wa Afrika kutoka nyuma.

Chui ni mnyama mwindaji anayewinda kimyakimya sana. Ingawa ni mdogo kuliko wanyama wote wa jenasi ya Panthera, chui bado anaweza kuwinda mnyama mkubwa kwasababu ya fuvu lake kubwa lenye taya zenye nguvu. Ukilinganisha na paka mwili wake ni mrefu zaidi na miguu yake ni mirefu. Urefu wa kichwa na mwili wake ni kati ya sm 125 na 165 na mkia wake unakaribia sm 60 mpaka 110. Urefu wa mabega ni sm 45 mpaka 80. Chui dume ni wakubwa 30% zaidi ukilinganisha na jike, kufikia uzito wa kg 37 mpaka 91 ukilinganisha na jike wenye kg 28 mpaka 60. Chui wenye miili mikubwa hupatikana kwenye maeneo yaliyojitenga na wanyama wengine wala nyama hasa toka kwa wale jamii ya paka wakubwa waliozoeleka kama vile simba na chui wakubwa wenye milia,"tigers".

Chui mara nyingi huchanganywa na paka wengine wenye madoa, kama duma na jagwa. Hata hivyo wana mtindo tofauti wa madoa: duma wana madoa ya kawaida yaliyosambaa mwili wote; jaguar wana madoa madogo ndani ya vijimiraba; wakati chui ana madoa ndani ya miduara midogo kuliko ile ya jaguar. Chui ni mkubwa na mwenye misuli zaidi kuliko duma, lakini mdogo kidogo na mwenye misuli kidigo kuliko jaguar. Madoa ya chui ni ya mviringo kwa Afrika Mashiriki na huwa ya mraba kwa kusini mwa Afrika. Chui wameripotiwa kufikia mpaka umri wa miaka 21. Rangi mbalimbali.

Chui wa Afrika aina ya mweusi
Dume la chui wa Persia mwenye rangi zisizo za kawaida

Biolojia na tabia

[hariri | hariri chanzo]
Chui wa Afrika akipumzika mtini.
Chui wa Afrika akiketi juu ya mti kwenye Serengeti
Mawindo ya chui ya Afrika yakining’inia juu ya mti

Chui anafahamika kwa uwezo wake wa kukwea miti, na huonekana akijipumzisha kwenye matawi ya miti wakati wa mchana, akiburuza mawindo yake mpaka juu ya miti na kuining’iniza huko; [1] ingawa, yeye hana nguvu sana kama jamii nyingine ya paka. Chui naye pia ni mwenye nguvu sana, anaweza kukimbia mpaka km 58 kwa saa, kuruka mbele zaidi ya mita 6 na kuruka juu mpaka kufikia hata mita 3. [2] Chui kiasili ni miongoni mwa wanyama wanaowinda usiku, japo wamerekodiwa mara kadhaa wakiwinda mchana, tena hasa wakati anga likiwa si angavu sana. Wao hutumia muda wao mwingi kulala, aidha juu ya miti, kwenye miamba au kwenye nyasi.


Chakula na kuwinda.

[hariri | hariri chanzo]

Chui huwinda kwa utegemezi. Ingawa hupendelea wanyama wa umbo la kati, chui hula kitu chochote kuanzia kombamwiko alaye kinyesi mpaka wakubwa pofu dume mwenye kg 900. Milo yao hujumuisha sana wanyama wenye kwato na nyani, lakini rodent, reptilia, amfibia, ndege na samaki nao huliwa pia. Kwa Afrika, swala wa umbo la kati ndio chakula kikuu cha chui, hasa impa na swala wa Thomson. [3] Huko Asia chui hula mbawala, chitali na muntiako na pia aina ya paa wa Asia na Ibex.

Chui hunyatia windo lake kimyakimya na dakika ya mwisho kasha kumrukia, humnyonga koo lake kwa kumng’ata haraka. Chui kwa kawaida huficha mawindo yao kwenye vichaka vilivyoshona au huyachukua mpaka juu ya miti, [4] na wana uwezo wa kubeba wanyama hata wenye uzito mara tatu ya uzito wao. Chui ndiyo mnyama pekee miongoni mwa jamii ya paka anayeweza kubeba mawindo yake juu ya miti. Uchaguzi wa mawindo kupitia tafiti umeonekana kuzingatia hali fulani ikiwemo ukubwa wa kundi analokuwemo mnyama awindwaye, ukubwa wa pori na mazingira yasiyoweza kuhatarisha maisha ya mwindaji, chui.

Kuzaliana na Mzunguko wa maisha.

[hariri | hariri chanzo]

Chui jike huko Sabi Sands maeneo ya Afrika ya Kusini. Ona madoa meupe anayotumia kuwasiliana na watoto wake wakati wa kuwinda kwenye nyasi ndefu.

Chui dume hufuata jike ambalo linamvutia, ingawa maranyingi kupigania haki za kuzaliana hutokea. Kutegemeana na eneo, chui hujamiiana mwaka mzima (Afrika na Asia) au kwa kipindi maalumu Januari mpaka Februari (Manchuria na Siberia). Chui jike kawaida huwa kwenye kipindi cha joto kwa siku 6 – 7. [5] Hubeba mimba kwa siku 90 – 105. [6] Watoto kwa kawaida huzaliwa kwa wingi wa 2 – 4, lakini kiwango cha kufa kwa watoto ni kikubwa kiasi cha kupona mtoto 1 – 2 tu kwa uzao mmoja.

Chui jike mwenye mimba hutafuta pango, uwazi kwenye miamba, mti wenye uwazi mkubwa au kichaka kwaajili ya kuzalia na kuweka makazi ya mwanzo. Watoto hufungua macho yao baada ya siku 10. Manyoya ya watoto huwa marefu na mengi kuliko ya wakubwa. Ndani ya miezi mitatu watoto huanza kuwafuata mama zao nje kuwinda. Wakiwa na umri wa mwaka mmoja chui wana uwezo wa kujilisha wenyewe lakini hubaki na mama zao kwa miezi 18 mpaka 24. [7]

Kuchangamana na jamii na hifadhi

[hariri | hariri chanzo]

Tafiti juu ya chui zinaonesha kuwa asilimia karibu 13% ya chui wote wanapatikana katika maeneo yanayotunzwa. Katika tafiti yao ya IUCN, Nowell and Jackson walisema chui dume huwa nahimaya ya kilomita za mraba 30-38, lakini jike huwa na kilomita za mraba 15-16 tu. [8]

Ikolojia

[hariri | hariri chanzo]

Kutawanyika na malazi

[hariri | hariri chanzo]
Msambao wa zamani (nyekundu) na sasa (kijani) wa chui.

Data kutoka mwaka 1996 zinaonesha kuwa chui ndio waliosambaa zaidi kwa wanyama wote jamii ya paka, na hasa katika sehemu za kusini mwa Asia na katikati mwa Afrika,ingawa tangu hapo kiasi hicho kimeanza kupungua.

Chui huishi zaidi sehemu zenye nyasi, miti kiasi na hasa pembezoni mwa vijito. Chui mara nyingi amefanyiwa tafiti akiwa katika misitu ya savanna, na ndio iliyotumika kutoa baadhi ya tabia zake. Kwa mfano kwa kawaida chui husemwa kuwa wao huwinda usiku lakini huko Afrika ya Magharibi wameonekana hasa kuwa wanawinda mchana. Pia chui wa misituni wanatabia ya kuchagua mawindo na huwa na tabia nyingi za msimu. [40] Huku akiwa katika misitu ya savanna, chui anaweza kuishi katika maeneo mengi: huko Urusi Mashariki ya Mbali, huweza hata kuishi kwenye jotoridi chini ya -25 digrii za Sentigredi.

Kazi za Kiikolojia.

[hariri | hariri chanzo]

Chui ni lazima apiganie chakula na malazi na wawindaji wingine kama simba, tigers , fisi madoa na mbwa mwitu wa Afrika hata na wale wa Asia. Wanyama hawa huweza kuiba mawindo ya chiu au hata kuwawinda kwa ajili ya kitoweo watoto wa chui. Chui ameweza kuishi na wanyama hawa pamoja kwa kuwa na muda tofauti wa kuwinda, na kutokuwa muda mwingi maeneo ambayo wanyama hawa wapo. Kwa usalama zaidi, chui hubeba aidha watoto wake au kitoweo chake alichowinda mpaka juu ya miti. Simba mara chache huweza kukwea juu ya miti kufikia chakula cha chui, na kama amevutiwa sana, tiger mkubwa anaweza pia kukwea mti kufikia chakula hicho.

Nowell na Jackson waliona nyakati Fulani ambapo chui walishirikiana na simba au tiger: hapa chui anaonekana kuua mnyama mdogo huku wenzake wakiwepo. Katika misitu ya Kitropiki chui hawaogopi jamii nyingine zap aka na kuwinda muda tofauti. Licha ya wingi wao, chui na tigers walionekana wakiishi pamoja bila ya ushindani mkubwa ambao ni kawaida kuonekana katika ukanda wa savanna.

Mahuluti

[hariri | hariri chanzo]
Pumapardi, picha ilipigwa 1904

Pumpard ni mnyama mahuluti aliyetokana na kuchanganywa chui na puma. Seti tatu za wanyama haw zilizalishwa kati ya mwaka 18900 na mapema 1900 na Carl Hagenbeck katika mbuga yake ya wanyama huko Hamburg, Ujerumani.

Chui na binadamu.

[hariri | hariri chanzo]
Mchoro wa mosaiki ukimwonesha mungu wa Kigiriki Dionysus akikalia kwenye chui, karne ya 4 K.K. Pella, Greece.

Chui wamejulikana kwa binadamu tangu enzi za kale na wameonekana kwenye sanaa, imani kwa nchi nyingi ambako walitokea kihistoria, kama vile Ugiriki ya kale, Persia na Roma, na hata kule ambako hawakuwepo ila kuanzia milenia za hapa karibuni, kwa mfano Uingereza. Matumizi ya sasa ya chui ni kama ngao ya michezo, ngao ya taifa imezoeleka sana kwa afrika, japo bidhaa nyingi duniani zinatumia jina hili.

Chui jike huko Sabi Sands, Afrika ya Kusini ikionesha kwa namna gani mtalii anavyoweza kuwasogelea chui

Licha ya umbo lake, mnyama huyu ni vigumu sana kuonekana mwituni. Sehemu nzuri za kuwaona chui katika afrika ni Sabi Sand Private Game Reserve huko Afrika ya Kusini, ambako chui wameyazoea magari ya safari na huonekana hata mchana kwa ukaribu kwelikweli. Huko Asia, huonekanakatika Mbuga ya Taifa ya Yala nchini Sri Lanka, ambako ni miongoni mwa seheme zenye chui wengi zaidi duniani, lakini hata hapa kuonekana hakujahakikishiwa kwasababu zaidi ya nusu ya mbuga imefungwa kwa jamii. Sehemu nyingine nzuri ya kuwona chui ni mbuga ya Taifa ya Wilpattu huko Sri Lanka, bila ya kusahau Madhya Pradesh na Uttarakhand huko India.