Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Mandera

Majiranukta: 3°25′00″N 40°40′00″E / 3.41667°N 40.6667°E / 3.41667; 40.6667
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya Mandera
Kaunti
Nembo ya Serikali
Kaulimbiu: ""
Mandera County in Kenya.svg
Kaunti ya Mandera katika Kenya
Coordinates: 3°25′00″N 40°40′00″E / 3.41667°N 40.6667°E / 3.41667; 40.6667
Nchi Kenya
Nambari9
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kaskazini Mashariki
Mji mkuuMandera
Miji mingineEl Wak
Serikali
GavanaAli Ibrahim Roba
Naibu wa GavanaArai Mohamed Ahmed
SenetaMohamed Maalim Mahamud
Mwakilishi wa wanawakeAmina Gedow Hassan
BungeBunge la Kaunti ya Mandera
Wawakilishi Wadi30
Maeneo bunge6
Eneo
Jumlakm2 25 939.8 (sq mi 10 015.4)
Idadi ya Watu
Jumla867,457
Msongamano33
Majira ya SaaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti
mandera.go.ke

Kaunti ya Mandera ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Imepakana na Kaunti ya Wajir, na nchi za Somalia na Uhabeshi.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 867,457 katika eneo la km2 25,939.8, msongamano ukiwa hivyo wa watu 33 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Mandera.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kaunti hii ina mbuga ya pekee ya Kaskazini Mashariki ya Malka Mari na hifadhi ya kibinafsi ya Chacnabole. Ina vilima vinavyotandaa kutoka El Wak hadi Uhabeshi ingawa kiasi kikubwa cha ardhi yake ni nchi tambarare.

Kuna kanda mbili za ikolojia, kavu na nusu kavu. 95% ya kaunti ni nusu kavu na huwa na vichaka vyenye miiba katika sehemu za chini za vilima[2].

Kaunti ya Mandera imegawanywa katika maeneo yafuatayo[3]:

Eneo Bunge/Kaunti ndogo Kata
Mandera West Takaba Kusini, Takaba, Lagsure, Dandu, Gither
Banissa Banissa, Derkhale, Guba, Malkamari, Kiliwehiri
Mandera North Ashabito, Guticha, Marothile, Rhamu, Rhamu Dimtu
Mandera South Wargadou, Kutulo, Elwak Kusini, Elwak Kaskazini, Shimbir Fatuma
Mandera East Arabia, Libehia, Khalalio, Neboi, Mandera Mjini
Lafey Sala, Fino, Lafey, Waranqara, Alango Gof

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

[hariri | hariri chanzo]
  • Mandera West 98,300
  • Banisa 152,598
  • Kutulo 72,394
  • Lafey 83,457
  • Mandera Central 157,220
  • Mandera East 159,638
  • Mandera North 143,850

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
  2. "KENYA INTER AGENCY RAPID ASSESSMENT MANDERA COUNTY CONFLICT ASSESSMENT REPORT 19TH – 30TH JUNE 2014", Kenya Inter Agency Assessment, ilipatikana 13-04-2018
  3. "Kaunti ya Mandera Ilihifadhiwa 9 Aprili 2018 kwenye Wayback Machine.", Infotrak, ilipatikana 13-04-2018
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]