Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Embu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya Embu
Kaunti
Sanamu iliyo kati mwa mji wa Embu
Bendera Nembo ya Serikali
Kaulimbiu: "Land of opportunities"
Embu County in Kenya.svg
Kaunti ya Embu katika Kenya
Nchi Kenya
Nambari14
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naWilaya ya Embu (Kenya)
Mji mkuuEmbu
Miji mingineSiakago, Kírítirí, Manyatta, Runyenjes
Serikali
GavanaCecily Mbarire
Naibu wa GavanaKínyua Múgo
SenetaMúndigi Túonaga
Mwakilishi wa wanawakePamela Njoki
BungeBunge la Kaunti ya Embu
SpikaThirikú
Wawakilishi Wadi20
MahakamaMahakama Kuu, Embu
Maeneo bunge4
Eneo
Jumlakm2 2 820.7 (sq mi 1 089.1)
Idadi ya Watu
Jumla608,599
Msongamano216
Pato la Taifa PPP
Kadirio la 2024
Jumla increase KES $584.386 Bilioni [1] (ya 23)
Kwa kila mtu increase $910,491 (ya 4) [1]
Pato la Taifa
Kadirio 2024
Jumla increase KES 194.782 Bilioni [1] (ya 23)
Kwa kila mtu increase KES 303,497 (ya 4) [1]
Majira ya SaaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti
embu.go.ke

Kaunti ya Embu ni kaunti katika eneo la Mlima Kenya nchini Kenya. Kaunti hii inachukua eneo la km² 2,821. Kaunti hii ni makazi ya Waembu na Wambeere. Mji mkuu na mji mkubwa wa kaunti hii ni Embu.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 608,599 katika eneo la km2 2,820.7, msongamano ukiwa hivyo wa watu 216 kwa kilometa mraba[2]. Kufikia mwaka 2024, idadi ya wakazi inakadiriwa kuwa 608,599.

Makao makuu Embu Town (Kírímarí)

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Embu inapakana na kaunti za Tharaka Nithi (kaskazini), Machakos (kusini), Kitui (mashariki) na Kirinyaga (magharibi). Sehemu ya Mbeere hujumlisha 74% ya kaunti na ni kavu kuliko sehemu zingine. Sehemu nyingi za kaunti hupata mvua ya kiwango cha mm 500[3].

Mto Tana hupitia katika kaunti hii, upande wa kusini na mashariki katika mpaka na kaunti za Machakos na Kitui. Sehemu hii ya Mto Tana huwa na malambo ya uzalishaji umememaji, yanayojulikana kama Seven Forks Dams.

Mbuga zilizo katika kaunti hiii ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya na Hifadhi ya Kitaifa ya Mwea inayopakana na Bwawa la Kamburu.

Kaunti ya Embu imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[4]:

Eneo bunge Kata
Manyatta Ruguru/Ngandori, Kithimu, Nginda, Mbeti Kaskazini, Kirimari, Gaturi Kusini
Runyenjes Gaturi Kaskazini, Kagaari Kusini, Kagaari Kaskazini, Central Ward, Kyeni Kaskazini, Kyeni Kusini
Mbeere Kusini Mwea, Amakim, Mbeti Kusini, Mavuria, Kiambere
Mbeere Kaskazini Nthawa, Muminji, Evurore

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [5]

[hariri | hariri chanzo]
  • Embu East 129,564
  • Embu North 79,556
  • Embu West 127,100
  • Mbeere South 163,476
  • Mbeere North 108,881
    • Mt. Kenya Forest 22

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Embu GDP profile". Iliwekwa mnamo 2025-01-30.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  3. Fausta Mbura Njiru. "Hydrological information for dam site selection by integrating geographic information system GIS and analytical hierarchical process AHP" (PDF). Iliwekwa mnamo 2018-04-16.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.