Baku
Mandhari
Jiji la Baku | |
Nchi | Azerbaijan |
---|
Baku (Kiazeri: Bakı) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Azerbaijan. Iko kando la Bahari Kaspi kwenye rasi ya Apsheron kwa 40°23′N 49°52′E. Rundiko la mji lina wakazi milioni tatu pamoja na wakimbizi wengi kutokana na vita katika Kaukazi.
Mji una pande tatu:
- Mji wa Kale (İçəri Şəhər)
- Mji mpya uliojengwa tangu kupatikana kwa mafuta ya petroli katika karne ya 19 hadi 1920
- Mji wa Kisovyeti uliojengwa wakati wa utawala wa Umoja wa Kisovyeti.
Mji wa kale umezungukwa na ukuta kama boma. Sehemu hii iliingizwa na UNESCO katika orodha la urithi wa dunia.
Tangu 1872 Baku ilikuwa mahali pa maendeleo ya haraka sana kutokana na upatikanaji wa mafuta ya petroli. Kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia nusu ya mafuta yaliyopatikana duniani yalitokea Baku.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Baku kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |