Nenda kwa yaliyomo

Shirika la ndege

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tangazo la "Europe to South America in 3 Days"

Shirika la ndege ni kampuni inayotoa huduma ya usafiri wa anga wa kiraia kwa abiria na mizigo. Mashirika ya ndege hutumia ndege kutoa huduma hizi. Kawaida, mashirika haya hupewa leseni na idara husika ya serikali.

Mashirika ya ndege hutofautiana kwa ukubwa, toka mashirika ya ndege madogo ya safari za ndani na mashirika makubwa ya safari za kimataifa. Mnamo 2019 shirika la ndege kubwa kuliko yote duniani ni American Airlines Group.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mashirika ya ndege ya kwanza

[hariri | hariri chanzo]

DELAG, Deutsche Luftschiffahrts-Aktiengesellschaft I ndilo shirika la ndege la kwanza.[1] Lilianzishwa Novemba 16, 1909 kwa msaada wa serikali na kumiliki ndege zilizotengenezwa na Zeppelin Corporation. Makao yake makuu yalikuwa Frankfurt.

Safari ya kwanza ya ndege ilikuwa Januari 1, 1914, toka St. Petersburg, Florida kwenda Tampa, Florida, kwa ndege iliyomilikiwa na St. Petersburg and Tampa Airboat Line.[2]

Mashirika ya ndege ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu zaidi ni KLM (1919),[3] Avianca (1919),[4] Qantas (1921),[5] na Czech Airlines (1923).[6]

Mashirika ya ndege ya Ulaya

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni

[hariri | hariri chanzo]
Tangazo la KLM mwaka 1919, founded on 7 October 1919, the shirika zee la ndege linalotumia jina lake la asili
Ndege aina ya Handley Page W.8b ilitumia na Handley Page Transport, shirika la ndege Uingereza lililoanzishwa mwaka 1919.

Shirika la ndege zenye mabawa yasiyozunguka la mwanzo huko Ulaya ni Aircraft Transport and Travel, lililoanzishwa na George Holt Thomas mwaka 1916. Shirika la Ndege la Uingereza linatokana na shirika hili. Shirika hili lilitumia ndege zilizokuwa za kijeshi na kuzibadilisha ili ziweze kubeba abiria.

Agosti 25, 1919, shirika lilitumia ndege aina ya DH.16s kwa safari za ndege toka Hounslow Heath Aerodrome kwenda Le Bourget. Shirika hili lilipata sifa kubwa pamoja na matatizo ya hali ya hewa. Novemba 1919, shirika hili lilipata mkataba wa kusafirisha barua nchini Uingereza. Ndege sita za Jeshi la Anga la Uingereza aina ya Airco DH.9A zilitumiwa na shirika hili kusafirisha barua kati ya Hawkinge na Cologne. Mwaka 1920, ndege hizi zilirudishwa kwa jeshi hilo.[7]

Mashirika mengine ya ndege nchini Uingereza yalifuata – Handley Page Transport liliundwa mwaka 1919 likitumia ndege aina ya Type O/400 yenye kubeba abiria 12,[8] kwa safari za London-Paris.[9]

Shirika la kwanza la ndege la Ufaransa lilikuwa ni Société des lignes Latécoère, baadaye liliitwa Aéropostale, ambalo lilianza kazi mwaka 1918 kwa safari za kwenda Hispania. Société Générale des Transports Aériens liliundwa mwishoni mwa 1919, na wana ndugu wa Farman na ndege ya Farman F.60 Goliath ilisafirisha watu kati ya Toussus-le-Noble na Kenley, karibu na Croydon, Uingereza. Kampuni nyingine nchini Ufaransa ilikuwa ni Compagnie des Messageries Aériennes, iliyoundwa mwaka 1919 na Louis-Charles Breguet, ikisafirisha barua na mizigo kati ya Uwanja wa Ndege wa Le Bourget, Paris na Uwanja wa Ndege wa Lesquin, Lille.[10]

Junkers F.13 D-190 of Junkers Luftverkehr

Shirika la ndege la Ujerumani la Deutsche Luft-Reederei liliundwa mwaka 1917 na kuanza kazi Februari 1919. Shirika lingine la Ujerumani lilikuwa ni Junkers Luftverkehr, lililoanza kazi mwaka 1921. Liliendesha ubia wa mashirika ya ndege nchini Austria, Denmaki, Estonia, Ufini, Hungaria, Latvia, Norway, Poland, Uswidi na Uswisi[[]].

Shirika la ndege la Uholanzi KLM lilifanya safari ya kwanza ya ndege mwaka 1920, na ndio shirika zee kabisa duniani. Shirika hili liliundwa na Albert Plesman,[11] Safari yake ya kwanza ilikuwa ni kutoka Uwanja wa Ndege wa Croydon, London kwenda Amsterdam.

Huko Ufini, shirika la Aero O/Y (hivi sasa Finnair) liliundwa huko Helsinki Septemba 12, 1923. Safari yake ya kwanza ilikuwa ni kati ya Helsinki na Tallinn, mji mkuu waEstonia, Machi 20, 1924.

Muungano wa Kisovyeti uliunda Chief Administration of the Civil Air Fleet mwaka 1921. Huduma za safari za ndani za ndege zilianza Julai 15, 1923 kati ya Moscow na Nizhni Novgorod. Toka mwaka 1932 shirika hili limekuwa likitumia jina la Aeroflot.[12].

  1. "DELAG: The World's First Airline, using dirgibles". Airships.net. Iliwekwa mnamo 2010-08-22.
  2. "World’s First Commercial Airline | The Greatest Moments in Flight", Space.com. 
  3. "History - KLM Corporate". (nl-en) 
  4. "History - Avianca Holdings S.A. - www.aviancaholdings.com". www.aviancaholdings.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-15. Iliwekwa mnamo 2017-10-14. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  5. "Founders of Qantas | Qantas". www.qantas.com (kwa Australian English). Iliwekwa mnamo 2017-10-14.
  6. "About Us | Czech Airlines". ČSA.cz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-10-14.
  7. The Putnam Aeronautical Review edited by John Motum, p170 Volume one 1990 Naval Institute Press
  8. https://www.flightglobal.com/FlightPDFArchive/1961/1961%20-%200055.PDF
  9. "Airline History 1903 to 1919". www.airlinehistory.co.uk. Iliwekwa mnamo 2017-10-14.
  10. "World Aviation in 1919 - Part 1". Royal Air Force Museum. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Januari 2011. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2011. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Koninklijke Luchtvaart Maatschappij, N.V. History". International Directory of Company Histories. 28. 1999. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2013.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Aeroflot History | Aeroflot". www.aeroflot.ru (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-10-14.

Kusoma zaidi

[hariri | hariri chanzo]
  1. "A history of the world's airlines", R.E.G. Davies, Oxford U.P, 1964
  2. "The airline encyclopedia, 1909–2000.” Myron J. Smith, Scarecrow Press, 2002
  3. "Flying Off Course: The Economics of International Airlines," 3rd edition. Rigas Doganis, Routledge, New York, 2002.
  4. "The Airline Business in the 21st Century." Rigas Doganis, Routledge, New York, 2001.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shirika la ndege kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.