Maskarena
Mandhari
Maskarena ni funguvisiwa katika Bahari Hindi takriban 900 km mashariki ya Madagaska. Kwa jumla ni visiwa vya dola la Morisi pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.
Visiwa muhimu ni Morisi, Réunion, Rodrigues na Cargados Carajos.
Asili ya jina ni nahodha Mreno Pedro Mascarenhas aliyekuwa Mzungu wa kwanza wa kuzitembelea. Havikuwa na wakazi lakini Mascarenhas alitoa taarifa ya kwamba alikuta mabaki ya meli iliyowahi kuharibika kitambo.
Kwa hiyo inaaminika ya kwamba mabaharia Waarabu labda pia Wahindi waliwahi kufika mara kwa visiwani bila kuanzisha makao ya kudumu. Lakini visiwa vilisaidia wasafiri baharini kupata chakula na maji na kupumzika kabla ya kuendelea na safari zao.