Nenda kwa yaliyomo

Kimalta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimalta ni lugha rasmi kwenye nchi ya kisiwani ya Malta katikati ya Bahari ya Mediteranea. Kimalta huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti ikiwa ni lugha pekee ya familia hiyo katika nchi za Ulaya.

Kimalta ni karibu na Kiarabu cha Tunisia lakini huandikwa kwa alfabeti ya Kilatini. Misingi ya sarufi ni Kiarabu, lakini lugha imepokea maneno mengi kutoka Kiitalia na Kiingereza. Siku hizi takriban nusu ya maneno yana asili ya Kiitalia, na theluthi moja ni Kiarabu. Mengine yameingia kutoka Kiingereza.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya lugha ni funguvisiwa hilo kuvamiwa na Waarabu Waislamu mwaka 870. Hao walitawala hadi mwaka 1091 na katika kipindi hicho lugha ya Kiarabu ilienea visiwani.

Baada ya Ufalme wa Wanormandi wa Sisilia kupata utawala wa funguvisiwa la Malta, watawala wapya walivumilia lugha ya Kiarabu.

Katika karne zilizofuata Kimalta kikaendelea kujenga tabia za pekee na maendeleo ya Kiarabu barani.

Tangu karne ya 16 lugha ya kiutawala ilikuwa Kiitalia, lakini wakulima na wavuvi waliendelea kusema Kimalta.

Mwaka 1936 wakati wa utawala wa Waingereza Kimalta kilipewa hadhi ya lugha rasmi pamoja na Kiingereza badala ya Kiitalia.

Idadi ya wasemaji ni takriban watu 520,000.

Mifano ya maneno ya Kimalta

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya Kiarabu

[hariri | hariri chanzo]
  • wieħed („moja“) < واحد wāḥid
  • kbir („kubwa“) < كبير kabīr
  • raġel („mwanaume“) < رجل raǧul
  • ħobż („mkate“) < خبز ḫubz
  • qamar („mwezi“) < قمر qamar
  • belt („mji“) < بلد balad
  • id („mkono“) < يد yad
  • tajjeb („njema“) < طيب ṭayyib
  • saba' („kidole“) < إصبع ʾiṣbaʿ
  • sema („anga“) < سماء samāʾ'
  • marid („mgonjwa“) < مريض marīḍ
  • tqil („nzito“) < ثقيل ṯaqīl
  • xahar („mwezi“) < شهر šahr
  • tifla („binti“) < طفلة ṭifla
  • kelma („neno“) < كلمة kalima
  • marsa („bandari“) < مرسى marsan

Asili ya Kiitalia

[hariri | hariri chanzo]
  • gravi („muhimu“) < grave
  • lvant („mashariki“) < levante
  • skola („shule“) < scuola
  • parti („sehemu“) < parte
  • avukat (wakili) < avvocato
  • natura („hali asilia“) < natura
  • frotta („tunda“) < frutto
  • griż („kijivu“) < grigio
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimalta kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.