Kiashiria cha Maendeleo ya Watu
Mandhari
Kiashiria cha Maendeleo ya Watu (Kiingereza: Human Development Index; kifupi: HDI) ni namba ya takwimu ambayo inaashiria ubora wa elimu, matarajio ya muda wa kuishi, na pato kwa kila mtu na hutumika ili kuweka nchi katika safu nne za maendeleo. Nchi hufanikisha kiashiria bora ikiwa na elimu bora, muda mrefu wa kuishi, na pato kubwa la wastani.
Kiliendelezwa na mchumi Mpakistani Mahbub ul-Haq kikatumiwa sana na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ili kupima maendeleo.
Safu za maendeleo ni duni (<0.550), wastani (0.550-0.699), juu (0.700-0.799), na juu sana (>0.800).[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Data and statistics readers guide" (kwa Kiingereza). Umoja wa Mataifa. Iliwekwa mnamo 2024-04-12.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiashiria cha Maendeleo ya Watu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |