Tycho Brahe
'
Tycho Brahe | |
---|---|
Tycho Brahe | |
Amezaliwa | 14 Desemba 1546 |
Amefariki | 24 Oktoba 1601 |
Kazi yake | mtaalamu wa astronomia nchini Denmark |
Tycho Brahe (aliyezaliwa kama Tyge Ottesen Brahe 14 Desemba 1546 – 24 Oktoba 1601) alikuwa mtaalamu wa astronomia nchini Denmark aliyejenga paoneaanga (kituo cha kuangalia nyota) cha Uraniborg.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Brahe alizaliwa katika familia ya makabaila wa Denmark akaendelea kuwa mtaalamu mashuhuri wa astronomia ya siku zake.
Alikuwa na uwezo mkubwa wa kuangalia nyota na kuelewa miendo yao. Alitumia muda mwingi kupima kikamilifu mahali pa nyota angani; hadi wakati ule wataalamu bado walikuwa wakitegemea orodha ya nyota ya Klaudio Ptolemaio ya miaka 1400 iliyopita iliyojulikana Ulaya kupitia tafsiri za Kiarabu. Tycho alifanya vipimo vyote bila darubini ambayo ilikuwa haijagunduliwa bado, akitumia vifaa kama roboduara (en:quadrant).
Orodha yake ilichapishwa baada ya kifo chake tu. Ilikuwa pia msingi kwa atlasi ya nyota ya Uranometria iliyotolewa na Johann Bayer mnamo 1603[1].
Mwaka 1572 aliona nyota mpya iliyoonekana kwa muda wa mwaka mmoja. Alichoona kilikuwa nyota nova yaani nyota iliyolipuka, hivyo kuonekana kun'gaa kwa ghafla. Alitambua ya kwamba hiyo nyota aliyoiona kuwa mpya haikuwa sayari.
Kati ya wanafunzi wake alikuwepo mwanaastronomia mashuhuri wa baadaye Johannes Kepler. Baada ya kifo cha Brahe, Kepler alirithi kumbukumbu yake juu ya miendo ya sayari ikamsaidia kutunga nadharia mpya ya mwendo wa sayari.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tycho Brahe’s great star catalogue First true successor to the Almagest, tovuti ya Ian Ridpath "Star Tales", iliangaliwa Oktoba 2017
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tycho Brahe, A picture of scientific life and work in the sixteenth century Kitabu cha J. L. E. Dreyer (1890) juu ya maisha ya Tycho Brahe kwenye tovuti ya wikisource.org
- Brahe, Tycho (1546-1601), tovuti ya scienceworld.wolfram.com, iliangaliwa Oktoba 2017
- Tycho Brahe, Accurate Astronomical Observations With Mechanical Instruments (Naked Eye Astronomy), Hands On Activity: Build and Use a Sextant or Quadrant, tovuti ya Julian Trubin, iliangaliwa Oktoba 2017
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tycho Brahe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |