Uundaji wa viatu
Uundaji wa viatu ni sanaa ya jadi ambao umepitwa na wakati kwa sababu ya viwanda vinavyounda viatu.
Habari ya jumla
[hariri | hariri chanzo]Wanaounda viatu (fundi wa viatu hushona viatu ili kuziba shimo bali hawaundi viatu) huunda bidhaa mbalimbali za kuvaliwa miguuni kama vile viatu vya kawaida na vingine vinavyoundwa kwa matumizi tofauti, kama kuvaliwa shambani ama kuvaliwa kazini. Ama vile vya kudensi navyo ama kucheza nayo spoti.
Kwa jumla viatu hivi huundwa kwa ngozi, mbao , mpira, plastiki, jute au vitu vingine vinavyotoka kwa mimea na hasa kuundwa kwa vitu vinavyokaa na ni vigumu. Hii ni ili soli ya viatu idumu kwa muda na huwa imeshonwa kwa pande ya juu yenye ngozi.
Waundaji wa viatu hutumia kifaa cha zamani kilichoundwa kufanana na umbo la mguu wa mtu ili kuunda kiatu chake. Baadhi ya vifaa hivi huwa kwa jozi: moja ya mguu wa kulia na kingine cha mguu wa kushoto. Vingine huwa kombo ilhali vingine huwa vimenyooka.
Kazi ya uundaji wa viatu huonekana kwa idadi kadhaa katika utamaduni wa kisasa katika hadithi kuhusu muundaji wa viatu na wafanyikazi wake. Pia, kuna methali: "Watoto wa muundaji viatu huwa hawana viatu."
Mtakatifu msimamizi wa waundaji viatu ni Krispino wa Soissons.
Aina fulani za kale na za jadi za viatu ni:
- Ngozi ya wanyama kufungwa miguu na laini za ngozi ngumu kufungwa juu yao: zilizotumiwa na Warumi katika vita vyao kaskazini mwa Ulaya.
- Viatu vya mbao: viatu hivi, mara nyingi vimejaa majani ili kuhifadhi joto miguuni.
- Viatu rahisi: viatu, mara nyingi huwa havidumu (ingawa aina tofauti ya ngozi huwa na sifa tofauti).
Waundaji, siku hizi, hutumia matairi ya gari kuunda soli kwa bei nafuu zaidi na kutumika badala ya plastiki.
Mpishi, wakati mwingine, huitwa "Muundaji wa viatu" kama matusi, hasa kusema kuwa chakula chake huwa kigumu kama ngozi ya viatu.
Rabbi Yochanan Hasandlar, mwalimu maarufu wa karne ya 3 BK, anasemekana kuwa alichuma pesa ya matakwa yake kwa kuunda viatu, jina lake la utani linaonyesha, pia, kuwa alitoka Aleksandria.
Papa Urban IV, jina la kuzaliwa ni Jacques Pantaléon, alikuwa mtoto wa fundi wa viatu wa Troyes, Ufaransa.
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]- Amri ya Mashujaa wa St Crispin-Muungano wa Waundaji 50000 kutoka Marekani. 1870
- Muundaji wa viatu vya aina ya Sandal
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- LISTSERV 15.0 - MISHNAHYOMIT Archives Ilihifadhiwa 7 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Chumba cha Muundaji Viatu - Jumba la makumbusho ya maendeleo ya Canada
- Mwongozo wa kuunda viatu kwa kutumia mikono (si mashine) Ilihifadhiwa 12 Novemba 2020 kwenye Wayback Machine., kitabu kifunzacho mbinu ya uundaji wa viatu kwa kutumia mikono.