Sun Tzu
Sun Tzu (pia: Sūn Zǐ) | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Sun Wu |
Alizaliwa | mnamo 500 KK |
Nchi | China |
Kazi yake | Jenerali, mwandishi, mwanafalsafa |
Sun Tzu aliyeishi manmo mwaka 500 KK alikuwa jenerali, mwandishi na mwanafalsafa kutoka nchini China.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Hakuna mengi yanayojulikana juu yake. Aliitwa Sun Wu akapewa jina la Sun Tzu kwa heshima na "Tzu" ilimaanisha "mwalimu".
Alikuwa jemadari wa mfalme Helü katika ufalme Wu uliokuwepo kwenye mto Yangtse karibu na mdomo wake.
Kuna hadithi juu yake ya kwamba siku moja mfalme alimwamuru kuonyesha utaalamu wake kama jenerali. Akampa hawara 300 wa nyumba yake. Sun Tzu aliwagawa katika vikosi viwili akaweka hawara 2 waliopendwa hasa na mfalme kama maafisa. Baadaye aliwaeleza amri kadhaa akawapa amri watekeleze. Hawara walianza kucheka tu bila kufanya kitu. Sun Tzu alisema: "Kama amri si dhahiri na askari hawaelewi ni kosa la jenerali" akaeleza shughuli tena na kurudia amri. Mabinti walicheka tena. Sasa alisema: "Kama amri zinaeleweka na askari hawatii ni kosa la maafisa" akatoa amri ya kukata vichwa vya hawara 2 waliopendwa na mfalme. Baada ya kuona vifo vya wenzao wengine walitii bila kusita tena.
Mfalme aliyeshtuka mwanzoni aliona huyu anafaa kuwa jenerali alimfanya jemadari wa ufalme.
Mafundisho
[hariri | hariri chanzo]Aliandika kitabu "Sanaa ya Vita" kinachosomwa hadi leo anamoeleza nadharia ya vita.
Mafundisho yake ni ya kwamba vita ni jambo la hatari ni afadhali kuepukana nayo ka sababu mara nyingi inaharibu taifa na dola. Vita inapaswa kufuata shabaha ya siasa inayoeleweka na kumaliza baada ya kufika shabaha.
Alisema ni bora kuvurugisha mipango ya adui kuliko kupambana naye, halau ni afadhali kuvunja ushikamano wake na wasaidizi na kwenye nafasi ya tatu tu ni kuingia vitani na kushinda.
Athira
[hariri | hariri chanzo]Kitabu cha Sun Tzu inasomwa na kufundishwa hadi leo katika vyuo vya kijeshi mbalimbali. Kati ya viuongozi wa kijeshi waliotafakari ushauri wa kitabu hii ni
- Napoleon Bonaparte
- Togo Heihachiro, jemadari wa wanajeshi wa Japan katika vita ya Japani na Urusi ya 1905
- Mao Tsedong kiongozi wa wakomunisti nchini China
- Norman Schwarzkopf, jemadari wa Marekani katika vita ya ghuba ya 1990
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Works by Sun Tzu katika Project Gutenberg
- Kitabu cha Sanaa ya Vita Archived 24 Julai 2020 at the Wayback Machine.
- Sun Tzu and Information Warfare