Nenda kwa yaliyomo

Mlangobahari wa Cook

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pande mbili za Newzealand na mlangobahari wa Cook katikati

Mlangobahari wa Cook (kwa Kiingereza: Cook Strait) ni sehemu ya bahari inayotenganisha visiwa viwili vikuu vya New Zealand ambavyo ni Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini. Inaunganisha Bahari ya Tasmania upande wa magharibi na sehemu ya kusini ya Bahari Pasifiki upande wa mashariki.

Bahari ina upana wa kilomita 22 pale ilipo nyembamba. Mlangobahari unapitiwa na feri za magari, malori na abiria wanaovuka umbali wa kilomita 96 baina ya Wellington upande wa kaskazini na Picton upande wa kusini katika muda wa masaa matatu.

Sehemu hii ya bahari ina dhoruba nyingi na mawimbi makali.

Mlangobahari huu ulipokea jina lake kutokana na James Cook aliyekuwa nahodha wa kwanza kutoka Ulaya aliyepita hapa kwenye mwaka 1670. Alitanguliwa mwaka 1642 na Mholanzi Abel Tasman aliyefikiri ni hori kubwa, hakutambua ni mlangobahari baina ya visiwa viwili tofauti.

Hata hivyo, Wamaori wenyeji wa New Zeland waliwahi kuvuka mlangobahari huu kwa karne kabla ya kufika kwa Tasman wakitumia mitumbwi yao mikubwa.