Bahari ya Tasmania
Mandhari
Bahari ya Tasmania ni bahari ya pembeni ya Pasifiki Kusini iliyopo kati ya Australia, Kisiwa cha Tasmania na New Zealand. Eneo lake ni takriban kilomita za mraba 2,331,000 likiwa na upana wa km 2,000 na urefu wa km 2,800. Maji yake hufikia kina cha mita 5,200.
Jina la bahari pamoja na kisiwa cha Tasmania limetokana na nahodha Mholanzi Abel Tasman, aliyekuwa Mzungu wa kwanza kupita huko na kuchora ramani mnamo mwaka 1642/1643. Mwingereza James Cook alifuata mnamo 1770 akakazia utafiti wa eneo. [1]
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Rotschi, H.; Lemasson, L. (1967), Oceanography of the Coral and Tasman Seas (PDF), Oceanogr Marine Biol Ann Rev, ASIN B00KJ0X6D4
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- ↑ "Tasman Sea". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)