Lance Henriksen
Lance Henriksen | |
---|---|
Henriksen mnamo 2010 | |
Amezaliwa | Lance James Henriksen 5 Mei 1940 New York City, New York, U.S. |
Kazi yake | Mwigizaji, Mwigizaji Sauti Mkongwe |
Miaka ya kazi | 1961 – mpaka sasa |
Ndoa | Jane Pollack (1995-mpaka sasa) |
Lance James Henriksen (amezaliwa 5 Mei 1940) ni mwigizaji wa filamu, msanii, anayefahamika zaidi na wapenzi wa TV kwa uhusika wake kwenye filamu za aina ya bunilizi ya kisayansi, aksheni na za kutisha kama vile The Terminator, na Alien, na kwenye kipindi cha TV kama vile Millennium.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Henriksen alizaliwa mjini Manhattan, New York City katika familia ya watu maskini kabisa. Baba yake alikuwa baharia wa Kinorwei na mwanamasumbwi aliyeitwa jina la utani la "Icewater" ambaye alitumia nusu ya maisha yake akiwa baharini tu. Mama'ke Henriksen alihaha kutafuta kazi akiwa kama mwelekezi wa wanengeaji, mhudumu, na mwanamitindo.[1][2] Wazazi wake walitalikiana akiwa na umri wa miaka miwili na alilelewa na mama'ke. Kadiri akuanvyo, Henriksen amejikuta akiingia katika matata mbalimbali wakatu yungali shuleni na kuthubu hata kuchungulia majumbani kwa watoto wenzi wake. Henriksen aliondoka nyumbani na kuachilia mbali shule akiwa na umri wa miaka kumi na miwili; hakujifunza kusoma mpaka alivyofikisha umri wa miaka 30, pale alipojiunza mwenyewe namna ya kusoma miswaada andishi ya filamu.[3] Ametumia ujana wake mwingi akiwa kama mtoto wa mtaani huko mjini New York. Kutembea na matreni ya mzigo nchi nzima, pia aliwekwa jela kwa makosa madogo kama vile ya uzururaji. Kilikuwa kipindi chake cha bahati kukutana na marafiki zake wa zamani Bw. James Cameron na Bruce Kenselaar.
Shughuli za uigizaji
[hariri | hariri chanzo]Kazi ya kwanza ya Henriksen ilikuwa kwenye tamthilia na alifanya kazi kama mwandalizi wa eneo la igizo; kwa kweli, alipokea uhusika wake kwa sababu alitengeneza seti nzima ya maandalizi. Mwanzoni mwa miaka yake ya 30, Henriksen alihitimu elimu yake ya uigizaji katika chuo cha Actors Studio na kuanza kuigiza huko mjini New York City.[4] Katika filamu, ameanza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya It Ain't Easy mnamo mwaka wa 1972. Henriksen akaenda kucheza katika nyusika mbalimbali na filamu pia. Nyusika hizo ni pamoja na kucheza kwenye filamu ya Steven Spielberg Close Encounters of the Third Kind (1977) na Damien: Omen II (1978). Pia amewahi kucheza kama mwanaanga Walter Schirra kwenye filamu ya The Right Stuff (1983) na mwigizaji Charles Bronson kwenye filamu ya TV mnamo 1991 - Reason for Living: The Jill Ireland Story.
Wakati James Cameron anatunga filamu ya The Terminator (1984), alipanga hasa uhusika wa Terminator uchezwe na Henriksen. Cameron alikwenda mpaka akachora picha ya Terminator kwa kutumia sura ya Henriksen. Bila kujali, uhusika hatimaye ukaenda kwa Arnold Schwarzenegger. Henriksen ameonekana kwenye filamu, alicheza kwenye uhusika mdogo wa Detective Hal Vukovich. Henriksen huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama roboti mwenye mwonekano wa binadamu, Bishop, kwenye filamu ya Aliens (1986, filamu nyingine ya Cameron) na Alien 3 (1992). Baadaye kaja kucheza kama Charles Bishop Weyland, mwonekano wa mtu uliotokana na Bishop wa awali, katika Alien vs. Predator (2004).
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Televisheni
[hariri | hariri chanzo]- Ryan's Hope (1980) - Preston Post
- Tales from the Crypt (1990) - Reno Crevice
- Millennium (1996-1999) - Frank Black
- The X-Files (1999) - Frank Black
- IGPX: Immortal Grand Prix (2005) - voice of Andrei Rubley
- Caminhos do Coração (2007) - Dr. Walker
- Transformers: Animated (2008-2009) - voice of Lockdown
- NCIS (2009) - Sheriff Clay Boyd
- Verizon Droid Commercial (2010)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Myatt, Sue (2004-02-06). "Short Early Biography of Lance Henriksen". Lance Henriksen Magic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-17. Iliwekwa mnamo 2007-07-09.
- ↑ Lance Henriksen Biography (1940?-)
- ↑ Myatt, Sue (2004-02-06). "The Web Magic Interview with Lance Henriksen: Frankly Speaking". Lance Henriksen Magic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-26. Iliwekwa mnamo 2007-07-09.
- ↑ Myatt, Sue (2004-02-06). "The Web Magic Interview with Lance Henriksen: By Invitation Only". Lance Henriksen Magic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-26. Iliwekwa mnamo 2007-07-09.
- ↑ First Image of Lance Henriksen in 'Scream of the Banshee'!
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Lance Henriksen at the Internet Movie Database
- Lance Henriksen katika Internet Broadway Database
- Lance Henriksen at FEARnet
- Lance Henriksen katika All Movie Guide
- Lance Henriksen Magic Ilihifadhiwa 24 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.
- Films in Review interview Ilihifadhiwa 9 Septemba 2018 kwenye Wayback Machine.
- The Making of Hard Target