Nenda kwa yaliyomo

Kisiwa cha Bering

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisiwa cha Bering (Picha ya angani); rangi nyeupe inaonyesha jinsi kinavyofunikwa na barafu wakati wa majira baridi
Kaburi la Vitus Bering

Kisiwa cha Bering (kwa Kirusi: о́стров Бе́ринга, ostrov Beringa) ni kisiwa cha Kirusi kilichopo ndani ya Bahari ya Bering takriban kilomita 230 upande wa mashariki wa Rasi ya Kamchatka.

Ni sehemu ya Visiwa vya Kamanda vinavyotazamwa kuwa sehemu ya magharibi ya pinde la Visiwa vya Aleuti.

Kisiwa cha Bering kina eneo la km² 1,660; umbo lake ni jembamba kikiwa na urefu wa km 92 na upana wa km 14-15.

Hakuna miti kwenye kisiwa hicho kutokana na hali ya hewa ambayo ni baridi mno pamoja na kuwa na upepo mkali, ukungu mzito na mitetemeko ya ardhi. Hapakuwa na wakazi wa kudumu katika historia, lakini tangu mnamo 1826 kuna kijiji cha wavuvi kinachoitwa Nikolskoye chenye watu 800.

Kisiwa kilipokea jina lake kwa kumbukumbu ya kamanda Vitus Bering aliyejiokoa hapa baada ya kuangamizwa baharini aliporudi kutoka Alaska kwenye mwaka 1741. Bering pamoja na mabaharia 28 alikufa kisiwani humo kutokana na ugonjwa wa kiseyeye. Mabaharia wengine waliweza kujiokoa kwa kula mwani na kujenga boti kwa kutumia vipande vya meli iliyovunjika.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Beringa, makala katika kamusi elezo ya www.oceandots.com (Kiingereza) - iliangaliwa Januari 2021 kupitia archive.org
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Bering kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.