Nenda kwa yaliyomo

Kisafishi ombwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisafishi ombwe kilivyo.

Kisafishi ombwe (kwa lugha ya Kiingereza vacuum cleaner) ni kifaa kinachofagia na kusafisha sakafu, mikeka (carpet cleaning Archived 12 Septemba 2017 at the Wayback Machine.)na kuta kwa kutumia teknolojia ya kwamba mata hairuhusu pahala pawe ombwe.

Kisafishi ombwe hufanya hivi kwa kutumia pampu ya hewa ambayo hufanya pahala pawe ombwe na kwa njia hii kufyonya vumbi au takataka yoyote iliyokuwa pahala panaposafishwa. Huweza kufyonza takataka na hata unyevu.

Takataka au vumbi huokotwa kwa mfuko wa kisafishi ombwe. Visafishi ombwe hutumika nyumbani na hata kwa makampuni makubwamakubwa. Visafishi ombwe vya makampuni huwa kubwa na huweza kuhifadhi uchafu mwingi zaidi vikilinganishwa na vile vya nyumbani.

Kifaa hiki chaweza kutumia nguvu za umeme kupitia waya au hata betri ndogo.

Hizi ndizo aina za visafishi ombwe:

  • za kusafisha pahali paliporowa maji (wet/dry): visafishi hivi hutumika kusafisha pahala paliporowa maji au kwenye unyevu uliomwagika.
  • za kushikwa kwa mkono (handheld): hivi ni visafishi vidogo vinavyoweza kushikwa kwa mkono. Hutumika kusafishi mahala padogo na hutumia betri dogo. Baada ya kusafisha ni vizuri kuhakikisha kwamba kisafishi hiki kimetolewa uchafu kisije kikaanza kunuka.
  • za kubebea mgongoni (backpack): kisafishi hiki huwa si kikubwa sana na kina mishipi ya kumwezesha mtu kukibeba kwa nyuma ili aweze kutembea nacho.
  • kisafishi roboti (robotic): kisafishi hiki huweza kunadhifu mahala bila kudhibitiwa na mtu na ndio maana chaitwa kisafishi roboti.
  • kisafishi saikloni (cyclonic): badala ya kutumia vichungi kama visafishi ombwe vya kawaida, kisafishi hiki husafisha mahala kwa kutumia mbinu ya saikloni. Hewa huzungushwa kwa pahala palipo na uchafu na kuugawanya na baadaye kuchukua uchafu.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.