Nenda kwa yaliyomo

Kendrick Lamar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sherehe ya tuzo ya Pulitzer 2018 - Kendrick Lamar
Sherehe ya tuzo ya Pulitzer 2018 - Kendrick Lamar

Kendrick Lamar Duckworth (amezaliwa 17 Juni 1987) ni rapa, mtunzi wa nyimbo, na mtayarishaji wa muziki kutoka mjini Compton, California, Marekani. Mara nyingi anatajwa kuwa mmoja wa marapa wenye ushawishi mkubwa. Kando ya kufanya shughuli za muziki kama msanii wa kujitegemea, Kendrick pia ni mmoja wa wanachama wa kundi la muziki aina ya hip hop maarufu kama Black Hippy akiwa na wasanii wenzake wa zamani wa lebo ya Top Dawg Entertainment (TDE) Ab-Soul, Jay Rock, na Schoolboy Q.

Lamar alianza shughuli zake za muziki akiwa kijana chini ya jina la kisanii la K.Dot. Alitoa kanda mseto iliyoitwa Y.H.N.I.C. (Hub City Threat Minor of the Year), ilivuta umakini wa wadau wengi wa muziki na kusababisha kusainiwa kwake na lebo ya TDE.[1] Alianza kupata umaarufu zaidi mnamo mwaka wa 2010 baada ya kutoa kanda mseto yake ya nne, Overly Dedicated. Mwaka uliofuata, alitoa albamu yake ya kwanza, Section.80, ambayo ilijumuisha wimbo wake wa "HiiiPoWeR". Kufikia wakati huo, alikuwa amejikusanyia wafuasi wengi mtandaoni na kushirikiana na marapa kadhaa mashuhuri. Baadaye alipata dili la kujiunga na lebo ya Dr. Dre, Aftermath Entertainment, chini ya uangalizi wa Interscope Records.

Albamu yake ya Good Kid, M.A.A.D City ilitolewa mwaka wa 2012, ilimletea umaarufu na mafanikio makubwa.[2] Albamu yake ya tatu ya To Pimp a Butterfly (2015), ilijumuisha vipengele vya muziki wa funk, soul, jazz, na maneno yalilenga zaidi maisha ya Wamarekani weusi. [3] Ilikuwa albamu yake ya kwanza kushika nambari moja kwenye Billboard 200 ya Marekani na ilikuwa na mafanikio makubwa sana. [4] Albamu yake ya nne, Damn (2017), ni albamu ya kwanza isiyo ya muziki wa klasiki na isiyo ya jazz kutunukiwa Tuzo ya Pulitzer ya Muziki. [5] Pia ilitoa wimbo wake wa kwanza nambari moja kwenye Billboard Hot 100 ya Marekani, "Humble". Wimbo huo pia ulitumika katika filamu ya Black Panther (2018) na mwaka wa 2022, alitoa albamu yake ya tano na ya mwisho akiwa na lebo ya TDE, Mr. Morale. & the Big Steppers. [6] [7]

Lamar amefikisha mauzo ya zaidi ya rekodi milioni 70 nchini Marekani pekee, na albamu zake zote zimeidhinishwa kufikia mauzo ya platinamu au zaidi na Recording Industry Association of America (RIAA).[8] Amepokea sifa nyingi katika sanaa yake, ikiwa ni pamoja na Tuzo 14 za Grammy, Tuzo mbili za American Music Awards, Tuzo sita za Tuzo za muziki za Billboard, Tuzo 11 za Tuzo za Muziki za Video za MTV, Tuzo ya Pulitzer, Tuzo ya Brit, na uteuzi wa Tuzo za Akademi. Mnamo 2012, MTV ilimtaja kuwa rapa mkali zaidi kwenye orodha yao ya kila mwaka.[9] Time ilimtaja kuwa mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani mwaka wa 2016.[10] Albamu zake tatu zilijumuishwa kwenye orodha ya Rolling Stone ya mwaka 2020 ya Albamu 500 Bora Zaidi za Muda Wote.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina Jukumu Maelezo
2018 Black Panther Soundtrack album
TBA Untitled film[11] Mtayarishaji Ametayarisha kwa kushirikiana na Parker County; inasambazwa na Paramount Pictures

Televisheni

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Jina la filamu Jina alilotumia Maelezo
2018 Power[12] Laces Episode: "Happy Birthday"
  1. Mike (2021-02-12). "Kendrick Lamar's Complete Discography". Tea And Weed (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  2. "Kendrick Lamar: the rise of a good kid rapper in a mad city". the Guardian (kwa Kiingereza). 2012-12-08. Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  3. "'To Pimp a Butterfly' remains an important display of the life and struggles of modern-day Black America". REVOLT (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  4. "Best Albums of the Decade (2010-19)". Metacritic (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-06. Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  5. "Kendrick Lamar wins Pulitzer Prize for music", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-04-17, iliwekwa mnamo 2022-08-01
  6. Sisario, Ben (2022-05-13), "Kendrick Lamar Returns With 'Mr. Morale & the Big Steppers'", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2022-08-01
  7. Mr. Morale & The Big Steppers by Kendrick Lamar (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-08-01
  8. "Gold & Platinum". RIAA (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  9. "Kendrick Lamar Brings Crown To Compton As 'Hottest MC in the Game" (kwa Kiingereza), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-03-12, iliwekwa mnamo 2022-08-01
  10. "Kendrick Lamar". Time (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-01.
  11. Grobar, Matt (2022-01-13). "Kendrick Lamar, Dave Free & 'South Park' Duo Matt Stone And Trey Parker To Produce Comedy Penned By Vernon Chatman For Paramount". Deadline (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-06.
  12. Kigezo:Cite magazine

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kendrick Lamar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.