Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Mwisho wa Ramadhani ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Waislamu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kuswali, baadaye hukutana kwenye karamu.
Mlango Kiswahili wa Lamu ni moja ya vielelezo bora vya usanifu wa Kiswahili unaopatikana pwani ya Afrika Mashariki. Milango hii yenye urembo wa kuchongwa kwa ustadi mkubwa ni ishara ya utajiri wa historia na utamaduni wa Waswahili. Mbao zinazotumika mara nyingi ni za mti mgumu kama mninga au mkongo, huku nakshi zake zikionyesha mchanganyiko wa athari za Kiarabu, Kihindi, na Kiafrika. Mara nyingi, milango hii ilikuwa ishara ya hadhi ya kijamii na ilitumika kufikisha ujumbe kupitia michoro na maandishi ya Kiarabu. Leo hii, milango ya Kiswahili inahifadhiwa kama urithi wa kitamaduni na kivutio cha watalii katika miji ya kihistoria kama Lamu na Zanzibar.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 98,644
Idadi ya kurasa zote: 196,175 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.