Nenda kwa yaliyomo

Katerina wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Katerina alivyochorwa na Bernardino Luini (National Art Museum of Azerbaijan).
Mchoro wa Artemisia Gentileschi.
Mchoro wa Carlo Crivelli.
Picha takatifu ya Mt. Katerina wa Aleksandria, na vituko vya kifodini chake.

Katerina wa Aleksandria (kwa Kigiriki: Αἰκατερίνα ἡ Μεγαλομάρτυς; 282-305 hivi) alikuwa bikira Mkristo wa Aleksandria, Misri, ambaye aliuawa kwa amri ya kaisari Maxentius mwanzoni mwa karne ya 4[1].

Kadiri ya mapokeo, alikuwa wa ukoo maarufu[2] tena msomi.

Mwanamke aliyejaliwa akili kali, hekima na juhudi, kisha kuongokea Ukristo akiwa na umri wa miaka 14, aliongoza watu mia kadhaa kumfuata katika dini hiyo[3].

Tangu alipofia dini anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Novemba au 25 Novemba.[4][5][6]

Masalia yake yanaheshimiwa sana kwenye monasteri juu ya mlima Sinai[7].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Clugnet, Léon. "St. Catherine of Alexandria." The Catholic Encyclopedia. Vol. 3. New York: Robert Appleton Company, 1908. 1 May 2013". Newadvent.org. 1908-11-01. Iliwekwa mnamo 2013-08-26.
  2. "Great Martyr Catherine of Alexandria".
  3. "Saint Catherine of Alexandria". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2010-10-29.
  4. Calendarium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 1969), p. 147
  5. Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)
  6. http://catholicsaints.info/saint-catherine-of-alexandria/
  7. https://www.santiebeati.it/dettaglio/79050
  • Allen, Prudence, The concept of woman: the Aristotelian revolution, 750 BC-AD 1250, 1997 (2nd edn.), Wm. B. Eerdmans Publishing, ISBN 978-0-8028-4270-1
  • Walsh, Christine. The Cult of St Katherine of Alexandria in Early Medieval Europe, (Ashgate 2007)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.