Nenda kwa yaliyomo

Chusa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ncha za chusa za zama za mawe za mwisho (kati ya mwaka 15,000 hadi 12,000 KK
Mwindaji wa Inuit (Eskimo) akishika chusa kwenye boti ya kayak, Hudson Bay, Kanada mnamo mwaka 1908-1914

Chusa ni kifaa kirefu chenye umbo la mkuki kinachotumiwa kwa shughuli za uvuvi na uwindaji wa wanyama wa majini.

Mara nyingi chusa imefungwa kwa kamba inayoruhusu mvuwi kuirudisha pamoja na windo.

Ncha za chusa za samaki kwa kawaida huwa na vipembe vikali vidogo vya kuelekea nyuma. Hivi vinaingia ndani ya mwili wa windo na kuizuia isitoroke.

Chusa zilipatikana tangu zama za mawe. Zamani na kimapokeo zilitengenezwa mara nyingi kwa kutumia ubao au mifupa iliyokatwakatwa kwa kupata vipembe vya kuelekea nyuma. Siku hizi ncha ni za metali.

Chusa zilitumiwa pia kama silaha. Katika michezo ya Roma ya Kale kulikiwa na magladiator walioitwa "wavuwi" waliotumia nyavu na chusa kama silaha zao.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.