Nenda kwa yaliyomo

Anelidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Annelida)
Anelidi
Nyungunyungu
Nyungunyungu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Nusuhimaya: Eumetazoa (Wanyama wenye tishu za kweli)
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Annelida (Wanyama kama nyungunyungu)
Ngazi za chini

Ngeli 5:

Anelidi ni faila ya wanyama wafananao na minyoo wenye mapingili kwa umbo wa pete. Katika faila hii kuna nyungunyungu, ruba na mwata. Wanatokea baharini, majini baridi na ardhini. Spishi nyingine huchimba katika ardhi au matope, nyingine huogelea majini. Ukubwa wao unaenda kutoka mm ≤1 hadi m 3.

Kila pingili linabeba nywele fupi ngumu zinazowasaidia wanyama hawa ili kwenda mbele au nyuma juu ya tabaka ya chini au ndani ya matobo yao. Mapingili ya Polychaeta yana nywele nyingi ambazo zipo juu ya aina ya “miguu” inayoitwa parapodia (maana: “kama miguu”). Clitellata hawana parapodia na wana nywele chache au hawana nywele. Lakini hawa wana ogani maalum kwa sehemu ya mbele ya mwili inayoitwa clitellum (taz. chini).

Spishi nyingi za anelidi zinaweza kuongezeka bila kuzaa. Sehemu za mwili zinajitenga na kuota mpaka mnyama mzima. Licha ya hayo kuzaa ni jinsi ya kawaida ya kuongezeka. Spishi nyingi ni mahuntha na hutengeneza mayai na manii, lakini baina ya Polychaeta kuna spishi zenye madume na majike. Spishi za Clitellata zinaweka mayai yao ndani ya mfuko wa ute unaochozwa na clitellum.