Nenda kwa yaliyomo

Alama ya uakifishaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alama za uakifishaji ni alama zinazotumiwa wakati wa kuandika pamoja na herufi. Kazi yake ni kusaadia kuelewa matini vyema, na kudokeza maana maalumu ya maneno au sehemu za sentensi, na kuonyesha muundo wa sentensi.

  1. .: inaitwa nukta, kituo kikuu, kikomo, kitone: Nayo hutumika:
    • Mwishoni mwa sentensi, kama vile "Tutafika alfajiri na mapema".
    • Kufupisha maneno, kama vile "S.L.P. (Sanduku la posta)". "Bw. Juma (Bwana Juma)"
    • Kutenga kiwango cha kitu, kama vile fedha, kilomita, kilogramu n.k. "Sh 6.80 (shilingi sita na senti themanini)" "Kilomita 2.5 (kilomita mbili na nusu)".
  2. , inaitwa Koma au mkato
  3. ? inaitwa alama ya kuuliza
  4. ! inaitwa alama ya mshangao
  5. ' inaitwa apostrofi au ritifaa
  6. " inaitwa alama za dondoo
  7. : inaitwa nuktambili
  8. ; inaitwa nuktamkato
  9. - inaitwa alama ya kistari

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alama ya uakifishaji kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.