Nenda kwa yaliyomo

Tezi (meli)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 10:56, 10 Aprili 2019 na Kipala (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Kwa kundinyota linaloitwa Shetri tazama hapa Shetri (kundinyota)

Tezi ya jahazi ya kihistoria

Tezi (au: shetri) ni sehemu ya nyuma ya meli. Huko kuna usukani wa chombo unaoelekeza meli kule inakotakiwa kuelekea. Ni pia mahali pa rafadha inayosukuma chombo mbele.

Kwa meli kubwa za uvuvi mara nyingi nyavu za kunasia samaki huteremshwa tezini.