Wikimedia Foundation Privacy Policy
Sera hii imepitishwa na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia. Lazima isiepwe, isivunje, wala isipuuzwe na viongozi au wafanyakazi wa Shirika la Wikimedia, wala sera za mradi wowote fulani wa Wikimedia. |
Kwa sababu tunaamini kwamba hupaswi kutoa taarifa binafsi ili ushiriki katika vuguvugu la maarifa huru, unaweza:
- Soma, hariri, au tumia Tovuti yoyote ya Wikimedia bila kusajili akaunti.
- Jisajili kwa akaunti bila kutoa anwani ya barua pepe wala jina kamili.
Kwa sababu tunataka uelewe jinsi Tovuti za Wikimedia zinavyotumiwa ili tuziboreshe kwa ajili yako, tunakusanya baadhi ya taarifa wakati:
- Kutoa michango hadharani.
- Kusajili akaunti au kusasisha ukurasa wako wa mtumiaji.
- Kutumia Tovuti za Wikimedia.
- Kututumia barua pepe au kushiriki katika utafiti au kutoa maoni.
Tumeahidi:
- Kueleza jinsi taarifa zako zinavyoweza kutumika au kushirikiwa katika Sera hii ya Faragha.
- Kutumia hatua mwafaka kudumisha usalama wa maelezo yako.
- Kutouza maelezo yako kamwe au kuyashiriki na watu wengine kwa madhumuni ya utangazaji wa mauzo.
- Kushiriki maelezo yako tu katika hali chache maalum, kama vile ili kuboresha Tovuti za Wikimedia, kutii sheria, au kukulinda wewe na watu wengine.
- Kuhifadhi maelezo yako kwa muda mfupi zaidi iwezekanavyo unaolingana na malengo ya kuendesha, kuelewa na kuboresha Tovuti za Wikimedia, na majukumu yetu chini ya sheria inayotumika.
Jihadhari:
- Maudhui yoyote unayoongeza au mabadiliko yoyote unayofanya kwenye Tovuti ya Wikimedia yataweza kupatikana kwa uma na wakati wote.
- Ukiongeza maudhui au kufanya mabadiliko kwenye Tovuti ya Wikimedia bila kuingia, maudhui au mabadiliko hayo yatahusishwa hadharani na kwa wakati wote kwenye anwani ya IP iliyotumiwa wakati huo, badala ya jina la mtumiaji.
- Jamii yetu ya wahariri wa kujitolea na wachangiaji ni kikosi kinachojidhibiti chenyewe. Wasimamizi fulani wa Tovuti za Wikimedia, ambao huchaguliwa na jamii hutumia zana zinazowapa ufikiaji mdogo wa maelezo yasiyo ya umma kuhusu michango ya hivi majuzi ili waweze kulinda Tovuti za Wikimedia na kutekeleza sera.
- Sera hii ya Faragha haitumiki kwa tovuti na huduma zote zinazoendeshwa na Wakfu ya Wikimedia, kama vile tovuti au huduma zilizo na sera zake za faragha (kama vile Duka la Wikimedia) au tovuti au huduma zinazoendeshwa na watu wengine (kama miradi ya wasanidi programu wengine kwenye Huduma za Wingu za Wikimedia).
- Kama sehemu ya juhudi zetu za kutoa elimu na kufanya utafiti kote ulimwenguni, mara kwa mara tunatoa maelezo kwa umma na maelezo ya jumla au yasiyo ya kibinafsi kwa umma kupitia mafungu ya data na seti za data.
- Ili kulinda Wakfu wa Wikimedia na watumiaji wengine, ikiwa hukubaliani na Sera hii ya Faragha, unaweza kukosa kutumia Tovuti za Wikimedia.
Karibu!
Wakfu wa Wikimedia ni shirika lisilo la faida linaloendesha tovuti za ushirikiano na za kutoa maarifa bila malipo, kama vile Wikipedia, Wikimedia Commons na Wiktionary.
Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi.
- Tunakusanya Maelezo machache sana ya Kibinafsi kukuhusu wewe.
- Hatukodishi wala kuuza Maelezo yako ya Kibinafsi kwa watu wengine.
Kwa kutumia Tovuti za Wikimedia, unakubali Sera hii.
Shirika la Wikimedia limejengwa juu ya kanuni rahisi, lakini thabiti: tunaweza kufanya makubwa zaidi tukiwa pamoja kuliko jinsi kila mmoja wetu anavyoweza kufanya akiwa peke yake. Hatuwezi kushirikiana bila kukusanya, kushiriki na kuchambua maelezo kuhusu watumiaji wetu tunapoendelea kutafuta njia mpya za kufanya Tovuti za Wikimedia rahisi zaidi kutumia, salama na zenye manufaa zaidi.
Tunaamini kuwa kukusanya na kutumia maelezo kunapaswa kwenda sambamba na uwazi. Sera hii ya Faragha inaelezea jinsi Wakfu wa Wikimedia, shirika lisilo la faida ambalo linamiliki Tovuti za Wikimedia, kama vile Wikipedia, linakusanya, kutumia na kushiriki maelezo tunayopokea kutoka kwako unapotumia Tovuti za Wikimedia. Ni muhimu kuelewa kwamba, kwa kutumia Tovuti yoyote ya Wikimedia, unaidhinisha kukusanywa, kuhamishwa, kuchakatwa, kuhifadhiwa, kufichuliwa na kutumiwa kwa maelezo yako kama ilivyoelezewa katika Sera hii ya Faragha. Hii inamaanisha kuwa ni muhimu kusoma Sera hii kwa uangalifu.
Tunaamini kwamba hupaswi kulazimika kutoa Maelezo ya Kibinafsi yasiyo ya umma ili ushiriki katika harakati ya maarifa yasiyolipishwa. Si lazima utoe maelezo kama jina lako halisi, anwani au tarehe ya kuzaliwa kujiandikisha kwenye akaunti ya kawaida au kuchangia maudhui kwenye Tovuti za Wikimedia.
Hatuuzi wala kukodisha Maelezo yako ya Kibinafsi, wala hatuwapi watu wengine ili wakuuzie chochote. Tunayatumia kujua jinsi ya kuwezesha Tovuti za Wikimedia ziwe za kuvutia zaidi na kufikiwa kwa urahisi, kubaini dhana zinazofanya kazi, na kufanya shughuli ya kujifunza na kuchangia ziwe za kufurahisha zaidi. Kwa ufupi: tunatumia maelelzo haya kuboresha Tovuti za Wikimedia kwa ajili yako.
Bila shaka, ni watu kama wewe, mabingwa wa maarifa yasiyolipishwa, ambao huwezesha Tovuti za Wikimedia ziendelee kutumika, na pia zinawiri na kustawi.
Fasili
Tunafahamu kuwa ni watu wachache tu miongoni mwenu wanaojua maneno ya kiufundi kama "pikseli za ufuatiliaji" na "akiba" zinazotumiwa katika Sera ya Faragha.
Iwe huna uzoefu wa istilahi ya faragha au wewe ni mtaalam ambaye angependa tu kujikumbusha, huenda utafaidika kutokana na Faharasa ya Istilahi Muhimu.
Kwa sababu kila mtu (si mawakili tu) anapaswa kuelewa kwa urahisi jinsi na kwa nini maelezo yake yanakusanywa na kutumiwa, tunatumia lugha ya kawaida badala ya istilahi rasmi katika Sera hii. Ili kusaidia kuhakikisha umeelewa istilahi muhimu, hili hapa jedwali la tafsiri:
Tukisema... | ...tunaamini: |
---|---|
"Wakfu wa Wikimedia" / "Wakfu" / "sisi" / "yetu" | Wikimedia Foundation, Inc., shirika lisilo la faida linaloendesha Tovuti za Wikimedia. |
"Tovuti za Wikimedia" / "huduma zetu" | Tovuti na huduma za Wikimedia (licha ya lugha zake), pamoja na miradi yetu mikuu, kama vile Wikipedia na Wikimedia Commons, pamoja na programu za simu, Violesura vya Usanidi wa Programu (API), barua pepe, na arifa; ukiondoa, hata hivyo, tovuti na huduma zilizoorodheshwa katika sehemu ya "Vipengele Ambavyo Havipo Chini ya Sera hii ya Faragha" hapa chini. |
"wewe" / "yako" / "mimi" | Wewe, licha ya kuwa wewe ni mtu binafsi, kundi au shirika, na licha ya kuwa unatumia Tovuti za Wikimedia au huduma zetu kwa niaba yako mwenyewe au ya mtu mwingine. |
"Sera hii" / "Sera hii ya Faragha" | Hati hii, yenye jina "Sera ya Faragha ya Wakfu wa Wikimedia". |
"michango" | Maudhui unayoweka au mabadiliko unayofanya kwenye sehemu yoyote ya Tovuti za Wikimedia. |
"Maelezo ya Kibinafsi" | Maelezo unayotupatia au maelezo tunayokusanya ambayo yanaweza kutumika kukutambulisha kibinafsi. Kumbuka, ingawa hatukusanyi aina zote za maelezo zifuatazo, tunazingatia angalau aina zifuatazo kuwa "maelezo ya kibinafsi" ikiwa si ya hadharani na yanaweza kutumiwa kukutambulisha:
|
"mtu mwingine" / "watu wengine" | Watu binafsi, vyombo, tovuti, huduma, bidhaa na programu ambazo hazidhibitiwi, kusimamiwa, au kuendeshwa na Wakfu wa Wikimedia. Hii ni pamoja na watumiaji wengine wa Wikimedia na mashirika au vikundi huru vinavyosaidia kukuza shughuli za Wikimedia kama vile tanzu za Wikimedia, mashirika yanayotekeleza mada maalum, na makundi ya watumiaji pamoja na watu wa kujitolea, wafanyakazi, wakurugenzi, maafisa, wapokeaji ruzuku, na makandarasi wa mashirika au vikundi hivyo. |
Vipengee Vinavyoshughulikiwa na Visivyoshughulikiwa na Sera Hii ya Faragha
Isipokuwa kama ilivyoelezewa hapo chini, Sera hii ya Faragha inatumika katika kukusanya na kushughulikia maelezo kukuhusu wewe ambayo tunapokea unapotumia Tovuti za Wikimedia. Sera hii inatumika pia kwa maelezo tunayopokea kutoka kwa washirika wetu au watu wengine. Ili kuelewa zaidi kuhusu vipengele vinavyoshughulikiwa na Sera hii ya Faragha, tafadhali rejelea hapa chini.
Mifano ya Vipengele Vinavyojumuishwa kwenye Sera Hii
|
---|
Kwa maslahi ya uwazi, Sera hii ya Faragha inashughulikia, bila kubagua lugha:
|
Hata hivyo, Sera hii ya Faragha, haishughulikii hali zingine ambapo tunaweza kukusanya au kuchakata maelezo. Kwa mfano, baadhi ya matumizi yanaweza kushughulikiwa na sera tofauti za faragha (kama zile za Duka la Wikimedia) au tovuti au huduma zinazoendeshwa na watu wengine (kama vile miradi ya watengenezaji wengine kwenye Huduma za Wingu la Wikimedia). Ili kuelewa zaidi kuhusu vipengele ambavyo havishughulikiwi na Sera hii ya Faragha, tafadhali rejelea hapa chini.
Maelezo zaidi kuhusu vipengele ambavyo havishughulikiwi na Sera hii ya Faragha
|
---|
Hii ni sehemu ya Sera ya Faragha na inanuiwa kueleza kwa undani hali ambazo hazishughulikiwi na Sera yetu ya Faragha.
Wakati mwingine, watu wa kujitolea wanaweza kuweka zana ya kukusanya maelezo, kama vile hati, kifaa, pikseli ya ufuatiliaji au kitufe cha kushiriki kwenye Tovuti ya Wikimedia bila sisi kujua. Sera hii haidhibiti jinsi watu wengine wanavyoshughulikia maelezo wanayopokea kutoka kwa zana kama hiyo. Ukiona zana kama hiyo ya watu wengine, na unaamini inakiuka Sera hii, unaweza kuiondoa mwenyewe, au uripoti kwa kutuma ujumbe kwa privacywikimedia.org ili tukuchunguze. |
Ikiwa sera za jamii zinadhibiti maelezo, kama vile Sera ya CheckUser, jamii husika inaweza kuchangia katika sheria na majukumu yaliyowekwa katika Sera hii. Hata hivyo, hawaruhusiwi kuunda minghairi mpya au vinginevyo kupunguza kinga zinazotolewa na Sera hii.
Aina ya MaelezoTunayopokea Kutoka Kwako na Jinsi Tunavyoyapata
Michango Yako ya Hadharani
Chochote unachochapisha kwenye Tovuti za Wikimedia kinaweza kuonekana na kutumiwa na kila mtu.
Unapotoa mchango kwenye Tovuti yoyote ya Wikimedia, pamoja na kwenye kurasa za watumiaji au majadiliano, unaweka rekodi ya kudumu, ya hadharani ya kila kipengee cha maudhui ambacho unaondoa au kubadilisha. Historia ya ukurasa itaonyesha wakati ulitoa mchango au kufuta maudhui, pamoja na jina lako la mtumiaji (ikiwa uliingia katika akaunti) au Anwani yako ya IP (ikiwa hukuingia katika akaunti). Tunaweza kutumia michango yako ya umma, iwe imejumuishwa katika michango ya umma ya watu wengine au la, kukuandalia huduma mpya au bidhaa zinazohusiana na data au kufahamu zaidi kuhusu jinsi Tovuti za Wikimedia zinavyotumiwa, kama ilivyoelezewa hapa chini katika sehemu ya "Jinsi Tunavyotumia Maelezo Tunayopokea Kutoka Kwako” ya Sera hii ya Faragha.
Maelezo Yanayoonekana Hadharani
|
---|
Isipokuwa Sera hii ikisema vinginevyo, unapaswa kuchukulia kwamba maelezo ambayo unachangia kwenye Tovuti za Wikimedia, pamoja na Maelezo ya Kibinafsi, yataonekana hadharani na yanaweza kupatikana na mifumo ya utafutaji. Kama kawaida ya mambo mtandaoni, chochote unachoshiriki kinaweza kunakiliwa na kusambazwa zaidi na watu wengine mtandaoni, Tafadhali usichapishe maelezo yoyote ambayo hungependa yajulikane na umma, kama kufichua jina lako halisi au eneo lako katika michango yako. Fahamu kuwa data maalum uliyoweka hadharani au data iliyojumuishwa ambayo tunaweza kuwekwa hadharani inaweza kutumiwa na mtu yeyote kwa uchambuzi na kutoa maelezo zaidi, kama vile mtumiaji anatoka nchi gani, mwelekeo wake wa kisiasa na jinsia yake. |
Maelezo ya Akaunti na Usajili
Huhitaji kufungua akaunti ili utumie Tovuti yoyote ya Wikimedia.
Ukifungua akaunti, huitaji kutupatia jina lako au anwani ya barua pepe (ingawa unaweza, ukipenda, kama vile kwa huduma ya "Tuma barua pepe kwa mtumiaji huyu", kwa mfano).
Usipofungua akaunti, michango yako itahusishwa hadharani na anwani yako ya IP.
Ungependa kufungua akaunti? Safi! Hutaki kufungua akaunti? Hakuna shida!
Hutakiwi kufungua akaunti ili usome au kuchangia kwenye Tovuti ya Wikimedia, isipokuwa kwa hali nadra. Hata hivyo, ikiwa unachangia bila kuingia katika akaunti, mchango wako utahusishwa hadharani na Anwani ya IP inayolingana na kifaa chako.
Ikiwa unataka kufungua akaunti ya kawaida, kawaida tunahitaji jina la mtumiaji na nenosiri tu. Hata hivyo, ukichagua kutotoa anwani ya barua pepe, hatuwezi kukusaidia kurejesha nenosiri lako.
Maelezo Zaidi kuhusu Majina ya Watumiaji
|
---|
Jina lako la mtumiaji litaonekana hadharani, kwa hivyo tafadhali kuwa mwangalifu kuhusu kufichua jina lako halisi au Maelezo mengine ya Kibinafsi katika jina lako la mtumiaji. Nenosiri lako linatumika tu kuthibitisha kuwa akaunti ni yako. Pia Anwani yako ya IP hutumwa kiotomatiki kwetu, na tunairekodi kwa muda. Hatua hii ni ya kulinda watumiaji wa Wikimedia na maudhui ya mradi; dhuluma ikitokea, anwani za IP zinaweza kutumika kufuatilia majina ya watumiaji kama sehemu ya uchunguzi. Hakuna Maelezo mengine ya Kibinafsi yanayohitajika: hakuna jina, anwani ya barua pepe, tarehe ya kuzaliwa wala maelezo ya kadi ya mkopo. Akaunti zinapofunguliwa haziwezi kuondolewa kabisa (ingawa unaweza kuficha maelezo kwenye ukurasa wako wa mtumiaji, ukipenda). Hii ni kwa sababu michango yako ya hadharani lazima ilinganishwe na mwandishi wake (wewe!). Wakati mwingine, jamii za Wikimedia zinaweza kuwasaidia watumiaji kuondoa maelezo ya ziada yanayohusiana na akaunti zao kwenye miradi. |
Ili kupata uelewa mzuri wa maelezo ya kidemografia ya watumiaji wetu, kujanibisha huduma zetu na kufahamu jinsi tunavyoweza kuboresha huduma zetu, huenda tutakuuliza maelezo zaidi ya kidemografia, kama vile jinsia au umri wako mwenyewe. Tutakufahamisha kama maelezo hayo yanakusudiwa kuwa ya hadharani au ya faragha, ili uweze kufanya uamuzi sahihi kuhusu kama ungependa kutupatia maelezo hayo. Daima, unatoa maelezo hayo kwa hiari kabisa. Ikiwa hutaki, si lazima—ni rahisi hivyo.
Maelezo ya Mahali
GPS na Teknolojia Nyingine za Mahali
Baadhi ya vipengele tunavyotoa hufanya kazi vizuri zaidi ikiwa tunajua eneo ulipo.
Ikiwa unakubali, tunaweza kutumia GPS (na teknolojia zingine zinazotumiwa kubaini eneo) ili tukuonyeshe maudhui yanayokufaa zaidi. Tunaweka siri maelezo yaliyochukuliwa na teknolojia hizi, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Sera hii. Unaweza kupata maelezo zaidi kwa kurejelea orodha ya mifano ya jinsi tunavyotumia teknolojia hizi katika Maswali Yanayoulizwa Sana.
Data msingi
Wakati mwingine, sisi hupokea kiotomatiki maelezo ya eneo kutoka kwa kifaa chako. Kwa mfano, ukipakia picha kwenye programu ya simu ya Wikimedia Commons, tunaweza kupokea data msingi kiotomatiki, kama vile mahali na wakati ulipiga picha, kutoka kwa kifaa chako. Tafadhali fahamu kuwa, tofauti na maelezo ya eneo yaliyokusanywa kwa kutumia GPS kama ilivyoelezwa hapa juu, mipangilio chaguomsingi kwenye kifaa chako cha mkononi kawaida inajumuisha data msingi kwenye picha au video unayopakia kwenye Tovuti za Wikimedia. Ikiwa hungependa tutumiwe data msingi na wala ionyeshwe hadharani wakati wa kupakia, tafadhali badilisha mipangilio kwenye kifaa chako.
Anwani za IP
Mwishowe, unapotembelea Tovuti yoyote ya Wikimedia, tutapokea kiotomatiki Anwani ya IP ya kifaa (au seva wakala) unayotumia kuingia mtandaoni, ambayo inaweza kutumika kutambua eneo lako la kijiografia.
Maelezo Yanayohusiana na Matumizi Yako ya Tovuti za Wikimedia
Tunatumia teknolojia fulani kukusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia Tovuti za Wikimedia.
Kama tovuti zingine, tunapokea kiotomatiki maelezo kukuhusu unapotembelea Tovuti za Wikimedia.
Pia tunatumia teknolojia mbalimbali zinazotumiwa sana, kama vile akiba, kukusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia Tovuti za Wikimedia, kuwezesha huduma zetu kuwa salama na rahisi kutumia, na kuwezesha kukupa huduma bora na zinazokufaa zaidi.
Tunataka kufanya Tovuti za Wikimedia ziwe bora kwako kwa kufahamu zaidi jinsi unavyozitumia. Mifano ya matumizi yako inaweza kujumuisha ni mara ngapi unatembelea Tovuti za Wikimedia, unachopenda, unachokiona muhimu, unavyofikia Tovuti za Wikimedia, na ikiwa utatumia huduma inayokufaa zaidi ikiwa tutaielezea kwa njia tofauti. Pia tungependa Sera hii na kanuni zetu zionyeshe maadili ya jamii yetu. Kwa sababu hii, tunaweka siri maelezo yanayohusiana na utumiaji wako wa Tovuti za Wikimedia, isipokuwa kama ilivyoonyeshwa katika Sera hii.
Maelezo Tunayopokea Kiotomatiki
Kwa sababu ya jinsi vivinjari vinavyofanya kazi, tunapokea maelezo kiotomatiki unapotembelea Tovuti za Wikimedia. Hii ni pamoja na wakati unatumia zana ya mtandaoni kwenye tovuti ya mtu mwingine ambayo hupakia maelezo kutoka kwa Wikimedia Sites. Maelezo haya yanajumuisha aina ya kifaa unachotumia (labda ikijumuisha nambari za kipekee za kitambulisho cha kifaa, kwa matoleo kadhaa ya beta ya programu tumizi za simu), aina na toleo la kivinjari chako, chaguo la lugha ya kivinjari chako, aina na toleo la mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako, wakati mwingine jina la mtoa huduma wako wa tovuti au wa simu, tovuti iliyokuelekeza kwenye Tovuti za Wikimedia, kurasa unazoomba na kutembelea, na tarehe na wakati wa kila ombi unalofanya kwenye tovuti za Wikimedia.
Kwa ufupi, tunatumia maelezo haya kuboresha huduma unayopokea kwenye tovuti za Wikimedia. Kwa mfano, tunatumia maelezo haya kuendesha tovuti, kudumisha usalama zaidi, na kupambana na ulaghai; kuboresha matumizi ya simu, kubadilisha maudhui na kuweka mapendeleo ya lugha, kujaribia vipengee ili kuona kinachofanya kazi, na kuboresha utendaji; kuelewa jinsi watumiaji wanavyotumia tovuti za Wikimedia, kufuatilia na kuchunguza matumizi ya huduma za anuwai, kupata uelewa zaidi kuhusu maelezo ya kidemografia katika Tovuti tofauti za Wikimedia, na kuchanganua mitindo.
Maelezo Tunayokusanya
Pia tunatumia teknolojia mbalimbali zinazotumiwa sana, kama vile akiba, kuelewa kuhusu jinsi unavyotumia Tovuti za Wikimedia, kuwezesha huduma zetu kuwa salama na rahisi kutumia, na kuwezesha kukupa huduma bora na zinazokufaa zaidi.
Tunakusanya aina kadhaa za maelezo kwa kutumia aina mbalimbali za teknolojia zinazotumiwa sana. Kwa ujumla, teknolojia hizi zinajumuisha pikseli za ufuatiliaji, JavaScript, na teknolojia anuwai za "data iliyohifadhiwa ndani ya kifaa", kama vile akiba na kuhifadhi ndani ya kifaa. Aina hizi za teknolojia pia zinaweza na wakati unatumia zana za mtandaoni kwenye tovuti ya mtu mwingine ambayo hupakia maelezo kutoka kwa Tovuti za Wikimedia. Tunatambua kuwa baadhi ya teknolojia hizi zina sifa mbaya katika jamii na zinaweza kutumiwa kwa madhumuni mabaya. Kwa hivyo, tungependa kufafanua kwa uwazi kwa nini tunatumia njia hizi na aina ya maelezo tunayokusanya kwa kuzitumia.
Kulingana na teknolojia tunayotumia, maelezo tunayohifadhi ndani ya vifaa yanaweza kujumuisha maandishi, Maelezo ya Kibinafsi (kama anwani yako ya IP), na maelezo kuhusu utumiaji wako wa Tovuti za Wikimedia (kama vile jina lako la mtumiaji au wakati ulizitembelea). Rejelea hapa chini upate maelezo zaidi.
Tunatumia maelezo haya kuwezesha huduma unayopokea kwenye Tovuti za Wikimedia kuwa salama na bora, kupata uelewa zaidi wa upendeleo wa watumiaji na jinsi wanavyotumia Tovuti za Wikimedia, na kwa jumla kuboresha huduma zetu. Hatutatumia akiba za watu wengine, isipokuwa ukituruhusu kufanya hivyo. Ukiona zana ya kukusanya data ya mtu mwingine ambayo hujaidhinishwa (kama vile zana ambayo huenda imewekwa kimakosa na mtumiaji au msimamizi mwingine), tafadhali tututmie ripoti utimumia [email protected].
Maelezo Zaidi kuhusu Maelezo Yaliyohifadhiwa
|
---|
Data iliyohifadhiwa ndani ya vifaa, JavaScript na pikseli za ufuatiliaji zinatusaidia kufanya mambo kama:
|
Ungependa kujua zaidi? Unaweza kusoma zaidi kuhusu akiba maalum tunazotumia, muda wake wa kuisha matumizi, na madhumuni ya kuzitumia katika Maswali Yanayoulizwa Sana.
Tunaamini ukusanyaji huu wa data husaidia kuboresha huduma kwa watumiaji, lakini unaweza kuondoa au kuzima baadhi ya maelezo au yale maelezo yaliyohifadhiwa ndani ya kifaa kupitia mipangilio yako ya kivinjari, kulingana na kivinjari chako. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu chaguo unazoweza kufanya kwenye Maswali Yanayoulizwa Sana. Ingawa maelezo yaliyohifadhiwa ndani ya kifaa huenda yasitumike katika tovuti zetu, huduma zingine hazitafanya kazi vizuri ikiwa utazima maelezo yaliyohifadhiwa ndani ya kifaa.
Ingawa mifano iliyotolewa hapa juu kuhusu maelezo yako yaliyokusanywa kupitia utumiaji wa zana za ukusanyaji maelezo inawekwa siri kulingana na Sera hii, tafadhali kumbuka kuwa maelezo mengine kuhusu hatua zilizochukuliwa na jina lako la mtumiaji yatafichuliwa kwa umma kupitia kumbukumbu za hadharani pamoja na hatua zilizochukuliwa na watumiaji wengine. Kwa mfano, kumbukumbu ya umma inaweza kujumuisha mabadiliko ya kihistoria ya makala au tarehe ambayo akaunti yako ilifunguliwa kwenye Tovuti ya Wikimedia pamoja na tarehe ambazo akaunti zingine ziliundwa kwenye Tovuti ya Wikimedia.
Jinsi Tunavyotumia Maelezo Tunayopokea Kutoka Kwako
Jumla
Sisi na watoa huduma wetu tutatumia Maelezo yako ya Kibinafsi kwa kusudi halisi la kutimiza madhumuni ya kufadhili, ikiwa ni pamoja na:
Kuendesha Tovuti za Wikimedia, kushiriki michango yako na kusimamia Huduma zetu.
|
---|
Tunashiriki katika shughuli hizi kusimamia uhusiano wetu na wewe, kwa sababu tuna nia njema na/au kutimiza majukumu yetu ya kisheria. |
Kutoa Huduma zinazokufaa.
|
---|
Wakati mwingine, tutabadilisha Huduma zikufae, kwa idhini yako; au kulingana na masilahi yetu halisi. |
Kutuma barua pepe na arifa za mawasiliano kuhusu vitu tunavyoamini vitakuvutia.
|
---|
Tutakutumia aina hizi za barua pepe tu kwa idhini yako isipokuwa kama inaruhusiwa kwa sheria husika. Hatuuzi, kukodisha, au kutumia anwani yako ya barua pepe kukutangazia bidhaa au huduma za watu wengine. Unaweza kudhibiti aina ya arifa unazopokea na ni mara ngapi unazipokea kwa kwenda kwenye Mapendeleo yako ya Arifa na Wasifu wa mtumiaji. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu barua pepe na arifa na jinsi ya kubadilisha mapendeleo yako katika Maswali Yanayoulizwa Sana. |
Kutuma tafiti za hiari na kuomba maoni.
|
---|
Tutakufahamisha kila mara, tukikupa fursa ya kushiriki maoni yako, jinsi tunavyopanga kutumia majibu yako na Maelezo yoyote ya Kibinafsi unayotupa. Si lazima ujibu tafiti zetu wala kutoa maoni. Tutakutumia barua pepe za aina hizi za barua tu kwa idhini yako isipokuwa kama inaruhusiwa kwa sheria husika. Unaweza kudhibiti aina ya arifa unazopokea na ni mara ngapi unazipokea kwa kwenda kwenye Mapendeleo yako ya Arifa na Wasifu wa mtumiaji. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu barua pepe na arifa na jinsi ya kubadilisha mapendeleo yako katika Maswali Yanayoulizwa Sana. |
Kuboresha Tovuti za Wikimedia na kufanya huduma unayopokea iwe salama na bora.
|
---|
Tunashiriki katika shughuli hizi kudumisha zaidi uhusiano wetu na wewe, kwa sababu tuna nia njema na/au kutimiza majukumu yetu ya kisheria. |
Zingine
Maelezo ya Mahali
GPS na Teknolojia Nyingine za Mahali
Kama ilivyoelezwa hapa juu, tunaweza kutumia teknolojia za eneo zinazotumiwa sana kukuonyesha maudhui muhimu zaidi. Kwa mfano, programu zetu za simu zinaweza kutambua nakala kutoka Tovuti za Wikimedia kuhusu mambo yanayokuvutia yanayofanyika karibu nawe. Kukumbuka, unaweza kukubali na/au kuzima ufikiaji wetu wa teknolojia hizi za eneo wakati wowote, kwa mfano, kupitia huduma asili za OS kwenye simu yako, na bado utumie Tovuti za Wikimedia.
Data msingi
Kama ilivyotajawa hapa juu, sisi hupokea kiotomatiki maelezo ya eneo kutoka kwa kifaa chako. Kwa mfano, ukipakia picha ukitumia programu ya simu ya Wikimedia Commons, tafadhali fahamu kuwa mipangilio chaguomsingi kwenye kifaa chako cha simu husababisha maelezo yanayohusiana na picha yako kujumuishwa kwenye upakiaji. Kumbuka, ikiwa hungependa tutumiwe data msingi na wala ionyeshwe hadharani wakati wa kupakia, tafadhali badilisha mipangilio kwenye kifaa chako.
Anwani za IP
Unapotembelea Tovuti yoyote ya Wikimedia, tutapokea kiotomatiki Anwani ya IP ya kifaa (au seva wakala) unayotumia kuingia mtandaoni, ambayo inaweza kutumika kutambua eneo lako la kijiografia. Tunaweka siri Anwani za IP, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Sera hii. Ukitembelea Tovuti za Wikimedia kwa kutumia kifaa chako cha mkononi, tunaweza kutumia anwani yako ya IP kuwapa watoa huduma maelezo yasiyokutambua kwa jina au ya jumla kwa kuhusu kiwango cha matumizi katika maeneo fulani.
Tunatumia maelezo haya ya maeneo kuwezesha huduma unazopokea kwenye Tovuti za Wikimedia kuwa salama na bora zaidi, kupata uelewa zaidi wa mapendeleo ya watumiaji na jinsi wanavyotumia Tovuti za Wikimedia, na kwa jumla kuboresha huduma zetu. Kwa mfano, tunatumia maelezo haya kutoa usalama zaidi, kuboresha matumizi ya simu, na kufahamu jinsi ya kupanua na kuisaidia zaidi jamii za Wikimedia. Pia tunatumia Maelezo ya Kibinafsi kwa njia iliyoelezwa katika sehemu za Sera hii inayoitwa "Kwa Sababu za Kisheria" na "Kukulinda Wewe, Sisi na Wengine."
Je, Tunaweza Kushiriki Maelezo Yako Wakati Gani?
We use and share your Personal Information when you give us specific permission to do so, for legal reasons, and in the other circumstances described below.
Kwa Idhini Yako
Tunashiriki Maelezo yako ya Kibinafsi kwa kusudi fulani, ukikubali. Kwa mfano, ukipokea ufadhili wa kielimu na tunaomba ruhusa ya kushiriki Maelezo yako ya kibinafsi kwenye jarida la eneo. Unaweza kupata maelezo zaidi katika orodha ya mifano kwenye Maswali Yanayoulizwa Sana.
For Legal Reasons
Tutafichua Maelezo yako ya Kibinafsi kwa mamlaka ya umma au watu wengine kwa ili kutii mchakato rasmi wa kisheria ikiwa tu tunaamini ni halali kisheria. Angalia pia Maelezo na mwongozo kuhusu ya taratibu na miongozo ya maelezo ya mtumiaji. Tutakuarifu kuhusu maombi kama ikiwezekana. Tunafanya hivyo ili kuendeleza masilahi yetu halali na/au kutii majukumu yetu ya kisheria
Tutafikia, kutatumia, kuhifadhi, na/au kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi tukiwa na sababu nzuri ya kuamini kuwa inatosheleza dhamana halali na inayoweza kutekelezwa kisheria, arifa ya kutokea mahakamani, amri ya mahakama, sheria au kanuni, au amri nyingine ya kimahakama au kiutawala. Hata hivyo, ikiwa tunaamini kuwa ombi fulani la kufichua maelezo ya mtumiaji ni batili kisheria au yanakiuka mfumo wa kisheria na mtumiaji aliyeathiriwa hataki kupinga ufichuzi huo, tutajitahidi kukataa ombi hilo. Tumejitolea kukujulisha kupitia barua pepe angalau siku kumi (10) za kalenda, inapowezekana, kabla ya kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi ili kujibu maagizo ya kisheria. Hata hivyo, tunaweza kutoa arifa ikiwa hatujazuiwa kisheria kuwasiliana na wewe, hakuna tishio la kuaminika la kuhatarisha maisha au kusababisha majeraha ambalo limesababishwa au kuzidishwa kwa kufichua ombi, na umetupatia anwani ya barua pepe.
Hakuna chochote katika Sera hii ya Faragha kinakusudiwa kupunguza mapingamizi yoyote ya kisheria au utetezi unaoweza kuwasilisha dhidi ya ombi la mtu mwingine (iwe ni la kiraia, kijinai au kiserikali) kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi. Tunapendekeza utafute ushauri wa wakili wa kisheria mara moja ikiwa ombi kama hilo limewasilishwa kukuhusu.
Ili upate maelezo zaidi, tembelea Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Arifa ya Kutokea Mahakamani.
Ikiwa Shirika Litahamishwa (Uwekano Mdogo Sana!)
Ikitokea kwamba umiliki wa Wakfu umebadilishwa, tutakutumia arifa ya siku 30 kabla ya Maelezo yoyote ya Kibinafsi kuhamishiwa kwa wamiliki wapya au kuwa chini ya sera tofauti ya faragha.
NI vigumu sana kutokea, lakini ikitokea kuwa umiliki wa sehemu yote au kubwa ya Wakfu huu utabadilika, au uongozi ukibadilika (kwa njia kama vile kuungana na shirika lingine, kujumuishwa au kununuliwa), sawa na maslahi yetu halali, tutaendelea kuweka siri Maelezo yako ya Kibinafsi, isipokuwa kama ilivyoelezwa katika Sera hii, na kukuarifu kupitia Tovuti za Wikimedia na arifa kwenye WikimediaAnnounce-L au orodha ya kutuma barua ambayo ni sawa na hii angalau siku thelathini (30) kabla ya Maelezo yoyote ya Kibinafsi kuhamishwa au kuwekwa chini ya sera tofauti ya faragha.
Kukulinda Wewe, Sisi na Wengine
Sisi, au watumiaji wenye haki fulani za kiutawala, tunatumia na kufichua Maelezo ya Kibinafsi ambayo ni muhimu sana:
- kutekeleza au kuchunguza ukiukaji wa sera za Wakfu wa Wikimedia au sera za jamii ambazo huenda zimetokea;
- kulinda shirika letu, miundombinu, wafanyakazi, makandarasi, au umma; au
- kuzuia majeraha tarajiwa au makubwa ya kimwili au kufa kwa mtu.
Tunafanya hivi kusimamia uhusiano wetu na wewe, kuendeleza maslahi yetu halali, na/au kufuata majukumu yetu ya kisheria.
Sisi, au watumiaji fulani wenye haki fulani za kiutawala kama ilivyoelezwa hapa chini, tunahitaji kutumia na kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi ikiwa inaaminika kuwa ni muhimu kutekeleza au kuchunguza ukiukaji tarajiwa wa Masharti ya Matumizi, Sera hii ya Faragha, au sera zozote za Wakfu wa Wikimedia au sera zozote za jamii. Tunaweza pia kuhitaji kufikia na kushiriki Maelezo ya Kibinafsi ili kuchunguza na kujitetea dhidi ya vitisho au vitendo vya kisheria.
Tovuti za Wikimedia ni za ushirikiano wa watumiaji wanaoandika sera nyingi na kuchagua kati yao watu watakaokuwa na haki fulani za kiutawala. Haki hizi zinaweza kujumuisha ufikiaji wa kiasi kidogo cha maelezo ambayo la sivyo yangekuwa ya faragha yanayohusu michango ya hivi majuzi na shughuli za watumiaji wengine. Wanatumia ufikiaji huu kusaidia kulinda dhidi ya uharibifu na unyanyasaji, kupambana na unyanyasaji wa watumiaji wengine, na kwa ujumla wanajaribu kupunguza tabia za dhuluma kwenye Tovuti za Wikimedia. Vikundi hivi tofauti vya kiutawala vilivyochaguliwa na watumiaji vina miongozo yao ya faragha na usiri, lakini vikundi vyote hivyo vinapaswa kukubali kufuata Sera ya Ufikiaji Maelezo Yasiyo ya Hadharani. Vikundi hivi vya kiutawala vilivyochaguliwa na watumiaji vinawajibikia watumiaji wengine kupitia ukaguzi na udhibiti: watumiaji huchaguliwa kupitia mchakato unaoendeshwa na jamii na kusimamiwa na wenzao kupitia kufuatilia vitendo vyao wakiwa wameingia katika akaunti. Hata hivyo, majina ya kisheria ya watumiaji hawa hayajulikani na wahudumu wa Wakfu wa Wikimedia.
Tunatumai kuwa hali hii haitatokea kamwe, lakini tunaweza kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi ikiwa tunaamini kwamba ni muhimu kuzuia kujeruhiwa au kufa kwa mtu, au kulinda shirika letu, wafanyakazi, makandarasi, watumiaji au umma. Tunaweza pia kufichua Maelezo yako ya Kibinafsi ikiwa tunaamini ni muhimu kugundua, kuzuia, au kutathmini na kushughulikia uwezekano wa barua taka, zisizo, ulaghai, unyanyasaji, shughuli haramu, na usalama au tishio la kiufundi. (Angalia orodha ya mifano katika Maswali Yanayoulizwa Sana upate maelezo zaidi.)
Kwa Watoa Huduma Wetu
Tunafichua Maelezo ya Kibinafsi kwa watoa huduma wetu wengine au makandarasi ili kusaidia kuendesha au kuboresha Tovuti za Wikimedia na kutoa huduma ili kuendeleza malengo yetu.
Tunatumia watoa huduma au makandarasi wengine kusaidia kuendesha au kuboresha Tovuti za Wikimedia kwa ajili yako na watumiaji wengine. Tunawapa idhini ya kufikia Maelezo yako ya Kibinafsi watoa huduma au makandarasi kama inavyohitajika ili kutufanyia huduma au kutumia zana na huduma zao. Tunaweka masharti, kama vile makubaliano ya siri, ili kusaidia kuhakikisha kuwa watoa huduma hawa wanashughulikia Maelezo yako ya Kibinafsi kila wakati kwa kulinda faragha yako kwa mujibu wa kanuni za Sera hii. Ili upate maelezo zaidi, tafadhali tembelea Maswali Yanayoulizwa Sana.
Ukitembelea Tovuti za Wikimedia kwa kutumia kifaa chako cha mkononi, tunatumia kutumia anwani yako ya IP kuwapa watoa huduma maelezo yasiyokutambua kwa jina au ya jumla kwa kuhusu kiwango cha matumizi katika maeneo fulani.
Baadhi ya watoa huduma wetu wanatuomba tuchapishe viungo kwenye sera zao za faragha; orodha ya watoa huduma hawa na viungo vya sera zao vinaweza kupatikana kwenye ukurasa huu.
Kuelewa na Kufanya Jaribio
- Tunawapa wasanidi programu na watafiti wa kujitolea idhini ya kufikia mifumo iliyo na Maelezo yako ya Kibinafsi ili kuwaruhusu kulinda, kusanidi na kuchangia kwenye Tovuti za Wikimedia.
- Tunashiriki pia Maelezo yasiyo ya Kibinafsi au maelezo yaliyojumuishwa, ambayo tunashiriki kwa watu wengine wanaopenda kuchunguza Tovuti za Wikimedia.
- Tunaposhiriki Maelezo ya Kibinafsi kwa watu wengine kwa madhumuni haya, tunaweka ulinzi imara wa kiufundi na kikandarasi ili kulinda Maelezo yako ya Kibinafsi yanayolingana na Sera hii na maslahi yetu halali.
Programu ya chanzo huria inayowezesha Tovuti za Wikimedia inategemea michango ya wasanidi programu wa kujitolea, ambao hutumia wakati mwingi kuandika na kujaribu misimbo ili kusaidia kuiboresha na kubadilika kulingana na mahitaji ya watumiaji wetu. Ili kuwezesha kazi yao, tunawapa baadhi ya wasanidi ufikiaji mdogo wa mifumo iliyo na Maelezo yako ya Kibinafsi, lakini ni muhimu tu kwao kusanidi na kuchangia kwenye Tovuti za Wikimedia.
Vivyo hivyo, tunashiriki Maelezo yasiyo ya Kibinafsi au maelezo jumuishi kwa watafiti, wasomi, wasomaji na watu wengine ambao wangependa kuchunguza Tovuti za Wikimedia. Kushiriki Maelezo haya ya kibinafsi huwasaidia kuelewa takwimu na mitindo ya matumizi, utazamaji na demografia. Kisha wanaweza kushiriki matokeo yao na sisi na watumiaji wetu ili tuweze kuelewa vizuri zaidi na kuboresha Tovuti za Wikimedia.
Tunapotoa ufikiaji wa maelezo ya Kibinafsi kwa watengenezaji au watafiti wengine, tunaweka mahitaji, kama vile ulinzi wa kiufundi na wa kimkataba, ili kusaidia kuhakikisha kuwa watoa huduma hawa hutibu Maelezo yako ya Kibinafsi kila wakati na kanuni za Sera hii na maagizo yetu. Ikiwa wasanidi au watafiti hawa watachapisha kazi au matokeo yao baadaye, tunawaomba wasifichue Maelezo yako ya Kibinafsi. Tafadhali kumbuka kuwa, licha ya majukumu tunayowapa wasanidi na watafiti, hatuwezi kukuhakikishia kwamba watatii makubaliano yetu, wala hatukuhakikishii kuwa tutachunguza au kukagua miradi yao kila mara. (Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu utambuzi mpya kwenye Maswali Yanayoulizwa Sana.)
Kwa Sababu Uliyatoa Hadharani
Maelezo unayochapisha yataonekana hadharani na yanaweza kuonekana na kutumiwa na kila mtu.
Maelezo yoyote unayochapisha hadharani kwenye Tovuti za Wikimedia yatasalia hivyo tu - ya hadharani. Kwa mfano, ukiweka anwani yako ya posta kwenye ukurasa wako wa mazungumzo, ipo hadharani, na haijalindwa na Sera hii. Na ukibadilisha maelezo bila kujisajili au kuingia katika akaunti yako, anwani yako ya IP itaonekana hadharani. Tafadhali fikiria kwa makini kuhusu kiwango chako cha faragha unachotaka kabla ya kufichua Maelezo ya Kibinafsi kwenye ukurasa wako wa mtumiaji au mahali pengine popote.
Je, Tunalindaje Maelezo yako ya Kibinafsi?
Tunatumia hatua, sera na taratibu mbalimbali halisi na za kiufundi ili kusaidia kulinda Maelezo yako ya Kibinafsi dhidi ya kufikiwa, kutumiwa au kufichuliwa bila ruhusa.
Tunajitahidi kulinda Maelezo yako ya Kibinafsi dhidi ya kufikiwa, kutumiwa au kufichuliwa bila ruhusa. Tunatumia hatua, sera na taratibu mbalimbali halisi na zana kiufundi (kama vile taratibu za kudhibiti ufikiaji, kinga za mtandao, na usalama halisi ) zilizoundwa kulinda mifumo yetu na Maelezo yako ya Kibinafsi. Hakika, hawezekani kuhamisha au kuhifadhi data kwa njia salama kabisa, kwa hivyo hatuwezi kukuhakikishia kuwa usalama wetu hautaathiriwa (kupitia hatua za kiufundi au kwa kukiuka sera na taratibu zetu).
Hatutawahi kukukuomba nenosiri lako kupitia barua pepe (lakini tunaweza kukutumia nenosiri ya muda kupitia barua pepe ikiwa umeomba kuweka upya nenosiri lako). Ukipokea barua pepe inayokuomba nenosiri lako, tafadhali tujulishe kwa kuituma kwa [email protected], ili tuweze kuchunguza chanzo cha barua pepe hiyo.
Tutahifadhi Maelezo Yako kwa Muda Gani?
Isipokuwa kama ilivyoelezwa vinginevyo katika Sera hii, tunahifashi Maelezo yako ya Kibinafsi kwa kipindi kinachotuwezesha kudhibiti, kuelewa na kuboresha Tovuti za Wikimedia au kufuata sheria inayotumika.
Tukishapokea Maelezo ya Kibinafsi kutoka kwako, tutayahifadhi kwa muda mfupi zaidi iwezekanavyo unaolingana na malengo ya kutengeneza, kuelewa na kuboresha wa Tovuti za Wikimedia, na majukumu yetu chini ya sheria inayotumika. Wakati mwingi, Maelezo ya Kibinafsi yanafutwa, kujumlishwa au kuondolewa utambulisho baada ya siku 90. Maelezo yasiyo ya Kibinafsi yanaweza kuhifadhiwa kwa muda usio na kikomo kama inavyofaa. (Angalia orodha ya mifano kwenye Maswali Yanayoulizwa Sana.)
Tafadhali kumbuka kuwa unapotoa mchango kwenye Tovuti yoyote ya Wikimedia, historia ya ukurasa itaonyesha wakati ulitoa mchango wako, jina lako la mtumiaji (ikiwa umeingia katika akaunti), au Anwani yako ya IP (ikiwa utabadilisha maelezo ukiwa hujaingia katika akaunti). Uwazi wa historia ya ya michango na marekebisho ya miradi ni muhimu kwa ufanisi na uaminikaji wake. Ili upate maelezo zaidi kuhusu kanuni zetu za kuhifadhi data, angalia miongozo yetu ya kuhifadhi maelezo.
Your rights
Ikiwa ungependa kuomba ufikiaji au kuondolewa kwa Maelezo yako ya Kibinafsi, unaweza kuwasiliana nasi.
Ili upate maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kuomba kuondolewa kwa Maelezo yako ya Kibinafsi, au haki zingine unazoweza kuwa nazo kuhusiana na Maelezo yako ya Kibinafsi, angalia Maswali Yanayoulizwa Sana. Ikiwa ungependa kuomba kufikia , kusasisha au kuzuia/kukataa kuchakatwa kwa Maelezo yako ya Kibinafsi, au kupokea nakala ya Maelezo yako ya Kibinafsi ili uyapeleke kwa shirika lingine, unaweza Kuwasiliana Nasi. Tutashughulikia ombi lako kwa mujibu wa sheria inayotumika.
Tafadhali kumbuka pia kuwa unaweza kutumia baadhi ya haki hizi bila kukatizwa nasi. Kwa mfano, ikiwa wewe ni mtumiaji aliyesajiliwa, unaweza kufikia na kusasisha Maelezo ya Kibinafsi katika sehemu ya Mapendeleo, na pia kupakua data ya akaunti yako ya mtumiaji. Unaweza pia kudhibiti aina za arifa unazopokea na ni mara ngapi unazipokea kwa kwenda kwenye Mapendeleo yako ya Arifa.
Ili kulinda Wakfu wa Wikimedia na watumiaji wengine, ikiwa hukubaliani na Sera hii ya Faragha, unaweza kukosa kutumia Tovuti za Wikimedia.
Wakfu Uko Wapi na Hili Linanihusu Vipi?
Wakfu wa Wikimedia ni shirika lisilo la faida lililoko San Francisco, California, na seva na vituo vya maelezo viko Marekani. Ukiamua kutumia Tovuti za Wikimedia, iwe ukiwa ndani au nje ya Marekani, unaelewa kuwa Maelezo yako ya Kibinafsi yatakusanywa, kuhamishwa, kuhifadhiwa, kuchakatwa, kufichuliwa na kutumiwa vinginevyo nchini Marekani kama ilivyoelezwa katika Sera hii ya Faragha. Unaelewa pia kuwa maelezo yako yanaweza kuhamishwa na sisi kutoka Marekani kwenda nchi zingine, ambazo zinaweza kuwa na sheria tofauti au zisizo kali za ulinzi wa maelezo ikilinganishwa na nchi yako, katika harakati za kukuhudumia.
Jibu Letu kuhusu Hoja za Usifuatilie (DNT)
Tumejitolea sana kulinda Maelezo ya Kibinafsi ya watumiaji. Chini ya Sera hii, tunaweza kushiriki maelezo yako tu chini ya hali fulani, ambayo unaweza kufahamu zaidi katika sehemu ya "Tunaweza Kushiriki Maelezo Yako Wakati Gani" ya Sera hii ya Faragha. Hasa, hatushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi kwa madhumuni ya uuzaji.
Kwa sababu tunalinda watumiaji wote kulingana na Sera hii ya Faragha, hatubadilishi tabia zetu tukikabiliwa na hoja ya kivinjari ya "usifuatilie". Ili upate maelezo zaidi kuhusu hoja ya Usifuatilie na jinsi tunavyozishughulikia, tafadhali tembelea Maswali Yanayoulizwa Sana.
Changes to This Privacy Policy
Mabadiliko makubwa katika Sera hii hayatafanywa hadi baada ya kipindi cha maoni ya umma cha angalau siku 30.
Kwa sababu vitu hubadilika baada ya muda na tunataka kuhakikisha Sera yetu ya Faragha inawakilisha kwa usahihi maadili na sheria zetu, huenda tutahitaji kurekebisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara. Tuna haki ya kufanya hivyo kwa njia ifuatayo:
- Ikiwa kuna mabadiliko makubwa, tutawatumia watumiaji wrtu mabadiliko yaliyopendekezwa kwa angalau lugha tatu (3) (zilizochaguliwa kwa hiari yetu) kwa kipindi cha maoni wazi kisichopungua siku thelathini (30) za kalenda. Kabla ya kuanza kwa kipindi chochote cha maoni, tutatuma arifa ya mabadiliko hayo na fursa ya kutoa maoni kupitia Tovuti za Wikimedia, na kupitia arifa kwenye WikimediaAnnounce-L au orodha sawa ya barua.
- Kwa mabadiliko madogo, kama marekebisho ya kisarufi, mabadiliko ya kiutawala au kisheria, au marekebisho ya taarifa zisizo sahihi, tutachapisha mabadiliko na, ikiwezekana, tutoe angalau ilani ya siku tatu (3) za kalenda kupitia WikimediaAnnounce-L au orodha sawa ya barua.
Tunakuomba ukague toleo jipya zaidi la Sera yetu ya Faragha. Ukiendelea kutumia Tovuti za Wikimedia baada ya tarehe yoyote iliyokubaliwa ya toleo linalofuata la Sera hii ya Faragha utakuwa ukikubali Sera hii ya Faragha.
Wasiliana Nasi
Ikiwa una maswali au maoni kuhusu Sera hii ya Faragha, au maelezo yaliyokusanywa chini ya Sera hii ya Faragha, tafadhali tutumie barua pepe kwa [email protected] au wasiliana nasi moja kwa moja. Ikiwa unaishi katika Eneo la Kiuchumi cha Ulaya na una maswali kuhusu maelezo yako ya kibinafsi au ungependa kuomba kuyafikia, kuyasasisha au kuyafuta, unaweza kuwasiliana na mwakilishi wetu kupitia barua pepe kwa [email protected], au kupitia barua kwa:
- Bird & Bird GDPR Representative Ireland
- 29 Earlsfort Terrace
- Dublin 2
- D02 AY28
- Ireland
- Mwakilishi mkuu: Vincent Rezzouk-Hammachi
Ikiwa wewe ni mtu anayeishi Uingereza na una maswali kuhusu maelezo yako ya kibinafsi au ungependa kuomba kuyafikia, kuyasasisha au kuyafuta, unaweza kuwasiliana na mwakilishi wetu kupitia barua pepe kwa [email protected], au kupitia posta kwa:
- Bird & Bird GDPR Representative Services UK
- 12 New Fetter Lane
- London
- EC4A 1JP
- United Kingdom
- Mwakilishi mkuu: Vincent Rezzouk-Hammachi
Mwakilishi wetu wa Eneo la Kiuchumi la Ulaya na wa Uingereza anapaswa kutumiwa ujumbe wa maswali tu kuhusiana na ulinzi wa data.
Kulingana na nchi unayoishi, unaweza pia kuwa na haki ya kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka inayosimamia nchi au mkoa wako.
Asante!
Asante kwa kusoma Sera yetu ya Faragha. Tunatumai unafurahia kutumia Tovuti za Wikimedia na unathamini ushiriki wako katika kuunda, kuendeleza na kuboresha hazina kubwa zaidi ya maarifa ulimwenguni isiyolipishwa.
Tafadhali kumbuka kuwa ikitokea tofauti yoyote ya maana au ufafanuzi kati ya toleo asili la Kiingereza na tafsiri ya Sera hii ya Faragha, toleo asili la Kiingereza linachukua nafasi ya kwanza.
This version was approved by Amanda Keton on June 7, 2021, pursuant to the Delegation of policy-making authority by the Board, and went into effect on June 25, 2021. Previous versions can be found below:
- Privacy Policy (May 2018 - June 2021): effective from May 24, 2018, until June 24, 2021
- Privacy policy (June 2014 - May 2018): effective from June 6, 2014, until May 24, 2018
- Privacy policy (November 2008 - June 2014): effective from November 25, 2008, until June 6, 2014
- Privacy policy (August 2008 - November 2008): effective from August 19, 2008, until November 25, 2008
- Privacy policy (June 2006 - August 2008): effective from June 21, 2006, until August 19, 2008
- Privacy policy (April 2005 to June 2006): effective from April 2005 until June 21, 2006