Nenda kwa yaliyomo

Xzibit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alvin Nathaniel Joiner
Mwanamuziki Xzibit akiwa Mjini Berlin
Mwanamuziki Xzibit akiwa Mjini Berlin
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Xzibit
Nchi Detroit, Michigan, Marekani
Alizaliwa 18 Septemba 1974
Aina ya muziki Rap na Hip Hop
Kazi yake Mwanamuziki, Muigizaji
Miaka ya kazi mn. 1995 -
Ameshirikiana na Tha Alkaholiks, Snoop Doggy, Ras Kass, Saafir, Strong Arm Steady, Dr. Dre, Kurupt, Eminem, Defari
Ala Sauti
Kampuni Loud, Sony, Open Bar, Koch

Alvin Nathaniel Joiner (Amezaliwa 18 Septemba 1974) Anafahamika zaidi kama Xzibit ni mwanamuziki wa Rap na Hip Hop, muigizaji, na pia mtangazaji wa TV kutoka mjini Detroit, Michigan, Marekani na kuinukia mjini Albuquerque, New Mexico akiwa na Baba yake mzazi pamoja na Mama yake wa Kambo.

Pia Xzibit anaendesha kipindi cha TV katika Televisheni ya MTV's maarufu kama "Pimp My Ride". Xzibit huwa anadesturi ya kila baada ya miaka miwili anatoa albamu mpya, tangu alivyotoa albamu ya kwanza mwaka 1996 iitwayo "At the Speed of Life" ikawa anakwaida ya kutoa mara tu miaka miwili imepita. Albamu iliyotoka karibuni ilkuwa ikiitwa "Full Circle" na ilitoka mwezi wa Oktoba 2006.

Maisha ya Mwanzo na Muziki

[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na umri mdogo Xzibit alifundishwa namna ya kuandika na mama yake mzazi 'Trena' ambaye baadae alifariki wakati Xzibit akiwa na umri wa miaka tisa.

Baadae baba yake Xzibiti akaowa mke mwingine baada ya kifo cha mke wa kwanza amabye ni mama yake mzazi Xzibit na familia kuamia mjini Albuquerque, New Mexico ambako Xzibit alikotumia ujana wake wote huko.

Alivyofika umri wa miaka 13 Xzibit akaanza kusikiliza nyimbo za Rap na kujaribu kuandika baadhi ya 'Mashairi', ambapo hakufika mbali kutoka na baba yake na mama yake wa kambo walikuwa watu wa dini sana ambao wote wawili ni "Mashaidi wa Yehova".

Kati ya miaka 14 na 17 Xzibit alitumia mda wake akiwa mitaani huko huko alikuwa anaaishi Albuquerque, na kupata matatizo mengi tu, Kuanzia hapo akawa mtu wa matatizo tu hadi baadae akafukuzwa shule, ambayo ilioko huko huko mjini Albuquerque.

Kupata Umaarufu

[hariri | hariri chanzo]

Xzibit alikuwa kama mwanachama flani hivi wa kundi la "the Likwit Crew", Pia hao ni moja kati ya wanachama wa "West Coast rappers", akiwemo Tha Alkaholiks na King T.

Baada kupata ushirika wa kushiriki katika matamasha mbali mbali na hao jamaa hiyo ilikuwa 1995, na baadae kumpeleka studio iliyokuwa inaitwa Loud Records na kuweza kutoa albamu ya kwanza ilioitwa "At the Speed of Life" ambayo yenyewe ilkuwa ni albamu ya msanii mchanga anayefanya vizuri katika masuala ya muziki, hiyo ilikuwa mwaka 1996.

Mwaka 1998 Xzibiti alitoa albamu nyingine iliyoitwa "40 Days & 40 Night", Ambayo yenyewe ilileta mwamko fulani na watu wengi walikubali kuwa Albamu ya pili ni nzuri kuliko iliyopita, na akawa unaongoza kikosi cha watu wenye vipaji cha West Coast's licha ya kuwa wengi walikuwa waki sema kuwa jamaa hato pata mafanikio.

Albamu Alizotoa

[hariri | hariri chanzo]

Filamu Alizoshiriki

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Xzibit kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.