Usiku wa Pasaka
Mwaka wa liturujia |
---|
Magharibi |
Mashariki |
Usiku wa Pasaka ni kesha kuu la mwaka wa Kanisa ambapo Wakristo wanashangilia ufufuko wa Yesu katika giza la kati ya Jumamosi kuu na Jumapili ya Pasaka: ndipo Injili zote zinaposimulia kwamba Yesu Kristo aliweza kufufuka baada ya kusulubiwa na kuzikwa siku ya Ijumaa kuu.
Ndio wakati mwafaka wa kubatiza hasa watu wazima, kwa sababu sakramenti hiyo, pamoja na kipaimara na ekaristi, inashirikisha kifo na ufufuko wa Yesu.
Hata hivyo, madhehebu yanatofautiana katika liturujia hata ya sikukuu hiyo.
Asili
[hariri | hariri chanzo]Kihistoria, usiku wa Pasaka uliadhimishwa na Waisraeli wa kale hasa namna iliyoratibiwa na Torati, ambamo jambo muhimu zaidi ni kula nyama ya mwanakondoo aliyechinjwa kama kafara. Tangu wakati wa Musa mlo huo umekuwa ukumbusho wa kutoka kwao katika unyanyasaji au utumwa nchini Misri.
Yesu alikamilisha hata ibada hiyo kwa kujifanya Mwanakondoo wa Mungu kama alivyotambulishwa na Yohane Mbatizaji katika mto Yordani.
Kwa kujitoa kufa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu na ondoleo la dhambi alivuka kutoka dunia hii kurudi kwa Baba na kuwezesha wote kuacha utumwa wa shetani, dhambi na kifo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- 50 Easter Vigil Prayers Ilihifadhiwa 31 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
- An Easter Vigil service
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |