Ukenekaji
Mandhari
Ukenekaji (kwa Kiingereza: distillation) ni mchakato wa kutenganisha mchanganyiko kiowevu kwa sehemu zake kama sehemu hizi zina viwango vya kuchemka tofauti. Mchakato wa ukenekaji hutumiwa sana katika kemia ingawa si kazi ya kikemia bali ya kifizikia.
Mchanganyiko hutiwa moto hadi sehemu moja ya mchanganyiko inapochemka yaani inageuka kuwa mvuke. Mvuke huo hukusanywa katika chombo cha kitoneshi (condenser) ambamo unapozwa na kutonesha hadi kuwa kiowevu tena. Kiowevu hicho huitwa mkeneko (distillate).
Mkeneko kwa kawaida bado ni mchanganyiko lakini ina kiwango kikubwa zaidi ya dutu yenye kiwango cha kuchemka cha chini zaidi. Mchakato wote unaweza kurudishwa mara kadhaa ili kuelekea dutu safi zaidi.
Mifano:
- maji ya matunda yaliyochachuka ni mchanganyiko wa maji, alikoholi mbalimbali na dutu nyingine. Mnamo nyuzijoto °C 65 methanoli inaanza kuchemka ambayo ni sumu, kuanzia nyuzijoto °C 78 ethanoli inachemka ambayo ni alikoholi inayotafutwa kwa matumizi ya pombe kali au alikoholi ya kitiba;
- mafuta ya petroliamu ni mchanganyiko wa dutu nyingi; huchemshwa katika ngazi mbalimbali ili kupata bidhaa zinazolengwa; katika ukenekaji wa petroliamu, petroli huchemka kabla ya diseli.
- maji ya bahari hukenekewa ili kupata maji safi ya kunywa. Chumvi tupu hubaki.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Alcohol distillation
- Case Study: Petroleum Distillation
- "Binary Vapor-Liquid Equilibrium Data" (searchable database). Chemical Engineering Research Information Center. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2007.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |