Nenda kwa yaliyomo

Uhuru wa dini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hali ya uhuru wa dini nchi kwa nchi (Pew Research Center study, 2009). Rangi ya njano hafifu inamaanisha vizuio ni vichache, kumbe nyekundu inaonyesha kuna vizuio vingi.

Uhuru wa dini ni mojawapo kati ya haki za msingi za kila binadamu kutokana na hadhi yake inayomtofautisha na wanyama. Yaani akili yake inamfanya atafute ukweli, jambo linalohitaji kuwa huru kutoka kwa mwingine yeyote.

Uhuru huo unaendana na wajibu na haki ya kufuata dhamiri hasa katika masuala ya dini na maadili.

Haki hiyo inatajwa katika Tamko la kimataifa la haki za binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, ingawa haitekelezwi vizuri katika nchi nyingi, hasa zile zinazofuata rasmi dini fulani au zinapinga dini zote.

Haki hiyo inajumlisha haki ya kuwa au kutokuwa na imani fulani, kuibadili, kuitekeleza katika ibada za binafsi na za pamoja, kuishuhudia kwa maneno na matendo, kuitangaza, n.k. maadamu mtu hatendi makosa ya jinai wala hasababishi vurugu katika maisha ya jamii.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Suala la kukubali haki hiyo katika sheria za nchi lilikabiliwa tangu zamani; maarufu ni hasa Hati ya Milano iliyotolewa na Konstantino Mkuu mwaka 313 ili kuruhusu Ukristo katika Dola la Roma baada ya miaka karibu 250 ya dhuluma.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uhuru wa dini kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.