Trifilo wa Nikosia
Mandhari
Trifilo wa Nikosia (Roma, Italia, au Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, mwanzoni mwa karne ya 4 – Nikosia, Kupro, 370) alikuwa askofu wa mji huo[1].
Baada ya kusoma sheria huko Beirut, Lebanoni[2], aliongokea Ukristo kwa msaada wa Spiridoni wa Tremetusia akasaidia sana kutetea imani sahihi na kupinga teolojia ya akina Ario. Kwa hiyo Atanasi alimsifu.
Maandishi yake [3] yamepotea. Imebaki tu kumbukumbu ya ufasaha wake katika kuhubiri ambao kadiri ya Jeromu ulizidi ule wa wengine wote wa wakati ule[4][5][6][7].
Tangu kale anaheshimiwa na Ukristo wa Mashariki na Ukristo wa Magharibi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Juni[8].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/93027
- ↑ Sozomeno, Historia Ecclesiastica, I, 11
- ↑ Jeromu, De viris illustribus, 92.
- ↑ Orthodox Church in America. "St Triphyllius the Bishop of Leucosia (Nicosia) in Cyprus". Lives of the Saints. Orthodox Church in America. Iliwekwa mnamo Machi 29, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "SAINT TRIPHYLLIUS". St. Nicholas Russian Orthodox Church, McKinney, Texas. Iliwekwa mnamo Machi 29, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "St. Triphyllius, bishop of Leucosia (Nicosia) Cyprus". stjohndc.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-01. Iliwekwa mnamo Machi 29, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "St. Triphyllius". Saints and angels. catholic.org. Iliwekwa mnamo Machi 29, 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |