Roentgeni
Roentgeni (Roentgenium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Roentgeni (Roentgenium) |
Alama | Rg |
Namba atomia | 111 |
Mfululizo safu | Simetali |
Uzani atomia | 280 u |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 18, 1 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Asilimia za ganda la dunia | 0 |
Roentgeni (jina la awali hadi 2004: Unununium) ni elementi sintetiki yenye namba atomia 111 katika mfumo radidia na uzani atomia wa isotopi yake yenye nusumaisha ndefu ni 280. Alama yake ni Rg.
Roentgeni haitokei kiasili kwa sababu nusumaisha ya isitopi zake ni fupi mno. 272Rg ina nusumaisha ya sekunde 0.0038 pekee; isotopi yenye nusumaisha ndefu ya sekunde 3.6 ni 280Rg. Hadi sasa isotopi mbili nyingine zilitambiluwa zenye nusumaisha ya millisekunde 170 (279Rg) na 6.4 (274).
Roentgeni ilitambuliwa mara ya kwanza na wanasayansi wa taasisi ya utafiti wa kinyuklia huko Darmstadt. Walifaulu kuitengeneza katika chombo cha nyuklia mara sita pia watafiti Wajapan walifaulu mara chache. Jina limekubaliwa kimataifa kuwa "Roentgeni" kwa heshima ya Konrad Röntgen.
Kama elementi zote za sintetiki hazina matumizi zatengenezwa tu kwa kusudi la utafiti. Duniani hazipatikani kiasili tena hata kama uwezekano ya kwamba ziliwahi kupatikana zamani ila tu kutokana na maisha mafupi ya atomi zao zimeshapotea muda mrefu. Kama ingewezekana kuitengeneza kwa kiasi kikubwa kidogo inawezekana itakuwa na rangi kama [dhahabu] lakini hadi sasa atomi chache hazikutosha kutazama rangi.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- WebElements.com - Roentgenium
- IUPAC: Proposal of name roentgenium for element 111
- IUPAC: Element 111 is named roentgenium Ilihifadhiwa 18 Machi 2006 kwenye Wayback Machine.
- Apsidium - Roentgenium Element 111 Ilihifadhiwa 22 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Unununium Element At Chemicalelements.com