Nenda kwa yaliyomo

Pietro Mennea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pietro Mennea

Pietro Paolo Mennea (jina la utani: Freccia del Sud, yaani "Mshale wa Kusini"; 28 Juni 195221 Machi 2013) alikuwa mwanariadha wa Italia. Ni mwanariadha pekee wa kiume aliyefuzu katika fainali nne mfululizo za Michezo ya Olimpiki za mita 200 tangu mwaka 1972 hadi 1984.[1]

Alifanikiwa zaidi katika mbio za mita 200, akishinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki huko Moscow mwaka 1980 huku akiweka rekodi ya ulimwengu ya kumaliza mbio kwa sekunde 19.72, mnamo Septemba 1979. Rekodi hiyo ilidumu kwa karibu miaka 17 - rekodi ndefu zaidi katika historia ya miaka hiyo barani Ulaya.

  1. Rowbottom, Mike (23 March 2013) Pietro Mennea: Olympic sprint champion whose 200 metres world record stood for 17 years – Obituaries – News. The Independent (2013-03-23). Retrieved on 2015-07-09.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pietro Mennea kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.