Nenda kwa yaliyomo

Pafnusi Mkaapweke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pafnusi Mkaapweke alikuwa padri mmonaki wa Misri, mwanafunzi wa Makari Mkuu[1], katika karne ya 4.

Alikuwa hatoki chumbani, isipokuwa kwa kushiriki Liturujia ya Kimungu siku za Jumamosi na Jumapili katika umbali wa kilometa 8; kutoka huko alikuwa anarudi na maji ya kumtosha wiki nzima.

Alitembelewa na Yohane Kasiani katika bonde la Sketi mwaka 395, alipokuwa na miaka 90.[2]

Pia anajulikana kwa masimulizi yake kuhusu maisha ya wakaapweke wengi wa jangwa la Misri, kama Onufri mkaapweke.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Julai, 25 Septemba na tarehe nyingine.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Vivian, Tim (2004). St Macarius the SpiritBearer. St Vladimir's Seminary Press. ku. 64, 131, 140, 195.
  2.  "Paphnutius" . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.