Nenda kwa yaliyomo

Mayotte

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mayote)
Department of Mayotte
Département de Mayotte (French)
Eneo la Mayotte
Mji mkuu
na mkubwa
Mamoudzou
Lugha rasmiKifaransa
Lugha ya taifaKimaore, Kibushi
Eneo
 • Jumlakm2 374
 • Maji (asilimia)0.4% [1]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2024320,901
 • Msongamano860/km2
 • Kwa kila mtu$11,300
HDI (2022)0.780
SarafuEuro (€)
Majira ya saaUTCUTC+3
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu++262
Jina la kikoa.yt

Mayotte ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte). Linaundwa na visiwa vya Maore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komori lakini si kisiasa. Mayotte iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Nzwani.Ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe. Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Andriantsoly, Sultani wa mwisho wa Mayotte, 1832-1843.

Mayotte inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika.

Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komori vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayotte.

Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayotte ikawa koloni la Kifaransa.

Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komori walidai uhuru na kuunda Umoja wa Komori, Mayotte iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.

Lugha na dini

[hariri | hariri chanzo]

Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayotte, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.

Upande wa dini, asilimia 97 ni Waislamu na 3% ni Wakristo.

Kisiwa cha Mayotte kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).

Bahari karibu na Mamoudzou.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  1. "percentage of land in water in Mayotte" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-03-20.