Martinique
Martinique | |||
| |||
Nchi | Ufaransa | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Fort-de-France | ||
Eneo | |||
- Jumla | 1,128 km² | ||
Idadi ya wakazi (2016) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 376,480 | ||
Tovuti: http://www.cr-martinique.fr/ |
Martinique (kwa Kifaransa; kwa Krioli: "Matinik" au "Matnik") ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi. Ni eneo la ng'ambo la Ufaransa na mkoa (departement) wa Ufaransa. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Eneo lake ni km² 1,128.
Makao makuu ni Fort-de-France. Miji mingine ni pamoja na Sainte-Anne na St. Pierre (iliyoharibiwa na mlipuko wa volkeno ya Mont Pelee mwaka 1902).
Watu
[hariri | hariri chanzo]Idadi ya wakazi ni 376,480. Takriban 83% ni wa asili ya Afrika au machotara wa aina mbalimbali. Wazee wao waliletwa huko kama watumwa kwa ajili ya kazi katika mashamba ya miwa. Kikundi kikubwa cha pili ni Wahindi (10%), Wazungu (6%). Waliobaki ni Waarabu, Wachina n.k.
Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wengi wanaongea pia Krioli yenye asili ya Kifaransa ambayo hata hivyo haieleweki tena na Wafaransa wa Ulaya.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo: 86% ni Wakatoliki, 5.6% Waprotestanti.
Utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Martinique ni maarufu kwa muziki wake wa zouk. Mwanamuziki mashuhuri wa aina hii ni Kassav.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Guadeloupe, eneo lingine la Ufaransa katika Bahari ya Karibi
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
- Serikali
- Martinique : the island of flowers - Official French website (in English)
- Prefecture Région Martinique Archived 21 Februari 2009 at the Wayback Machine. - Official site
- Regional Council of Martinique Archived 9 Novemba 2000 at the Wayback Machine. Tovuti rasmi
- Taarifa za jumla
- Martinique katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Martinique
- Safari
- Martinique Tourism Authority - Official site
- Zananas Martinique Archived 16 Februari 2015 at the Wayback Machine. - Informations site
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Martinique kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |