Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.[1]
TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mamlaka na malengo
[hariri | hariri chanzo]Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
- Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
- Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
- Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
- Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
- Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
- Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
- Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
- Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.
Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
- Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
- Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
- Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Tanzania Communications Regulatory Authority". Commonwealth of Nations (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-07. Iliwekwa mnamo 2022-06-30.