Nenda kwa yaliyomo

Liposuction

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Liposuction kwa mwanamume aliye na matiti.

Liposuction (ama lipo tu) ni aina ya upasuaji ambayo huondoa mafuta kutoka mwili wa binadamu kwa lengo la kubadilisha maumbile yake. Hamna ushahidi wowote kuwa liposuction hufanya kazi katika kupunguza uzito wa binadamu. Katika nchi za Ulaya lipo hutumika sana.

Athari hatari za upasuaji huu ni kama, kushikamana kwa damu ndani ya mishipa (thrombosis), organ perforation, kuvuja damu na hata maambukizi. Vilevile husababisha vifo asilimia 0.01, yaani moja kwa kesi elfu kumi zilizoripotiwa.

Njia hii ya upasuaji inaweza kufanyika kwa ganzi isiyo nusukaputi. Pia inahusisha utumiaji wa mrija unaotumia shinikizo kunyonya mafuta. Inaaminika kufanya kazi kwa watu ambao wana uzito wa kawaida na ngozi nzuri ambayo itarudi kawaida (elastic skin).

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Lipo sanasana hutumika kwa kujaribu kubanilisha maumbile ya mwili. Upungufu wa uzito kutoka kwa lipo unaonekana kuingia ama kujitokeza kwa muda mchache) lakini kusababisha madhara ya muda mrefu. Baada ya miezi   kadhaa mafuta yanarudi na kutapakaa mwilini. Lipo haiwezi kusaidia watu walio na unene wa kupindukia unaotokana na sababu za kimetaboli kama vile upinzani wa insulini (insulin resistance).

Inaweza pia kutumika kuondoa mafuta mengi katika lymphedema.

Hatari za Liposuction

[hariri | hariri chanzo]

Kuna hatari ambazo zinaweza kujitokeza juu ya lipo yoyote; hatari inaongezeka wakati eneo linalotibiwa linafunika asilimia kubwa ya mwili.

  • Vifo
  • Maumivu
  • Maambukizi
  • Kuvimba
  • Kuungua 
  • Makovu
  • Ulemavu

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liposuction kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.