Nenda kwa yaliyomo

Kukama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kukama kwa mkono

Kukama ni tendo la kuondoa maziwa kutoka kiwele cha mnyama, kawaida ng'ombe (ng'ombe), kifaru wa majini, mbuzi , kondoo na ngamia mara chache zaidi , farasi na punda. Kukama kunaweza kufanyika kwa mikono au kwa mashine.

Kukama kwa mikono

[hariri | hariri chanzo]

Kukama kwa mikono kunafanyika kwa kutomasa na kuvuta chini chuchu kwenyekiwele cha ng'ombe,ukichuruzisha maziwa kwenye ndoo. Njia mbili kuu hutumika:

  • Sehemu ya juu ya chuchu hufinywa kati ya kidole cha shahada na gumba, maziwa yakizuiliwa katika sehemu ya chini, ambayo ni hufinywa na vidole vile vingine, kuyachuruzisha maziwa nje kwa kupitia upenyo katika ncha ya chuchu.
  • Sehemu ya juu ya chuchu hufinywa huku imezibwa na kidole cha shahada na gumba, ambavyo kisha hutelezeshwa chini ya chuchu, kuyasukuma maziwa kuelekea kwenye ncha ya chuchu.

Kukama kwa mashine

[hariri | hariri chanzo]
Kukama kwa mashine kwa akali ndogo

Kukama kwingi katika nchi zilizoendelea hufanywa kwa kutumia mashine za kukama. Vikombe vya chuchu huwekwa kwenye chuchu za ng'ombe, halafu vikombe hivyo hujipindua baina ya eneo lisilo na hewa na eneo lenye hewa ili kuongeza mvuto unaoyatoa maziwa. Maziwa huchujwa na kupozwa kabla ya kuongezwa kwenye tangi kubwa la kuhifadhia maziwa.

Kukama kwa sumu

[hariri | hariri chanzo]

Kukama ni neno linalotumiwa pia kuwa na maana ya kutoa sumu ya buibui na nyoka kwa ajili ya kupata dawa ya sumu.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • (Kiingereza) [1]MilkAcademy (for more applicable information about milking equipments and dairy farming)