Nenda kwa yaliyomo

Korogwe (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Korogwe
Korogwe is located in Tanzania
Korogwe
Korogwe

Mahali pa mji wa katika Tanzania

Majiranukta: 5°5′24″S 38°32′24″E / 5.09000°S 38.54000°E / -5.09000; 38.54000
Nchi Tanzania
Mkoa Tanga
Wilaya Korogwe
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 86,551

Korogwe ni mji upande wa Kaskazini-Mashariki wa Tanzania ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Korogwe. Tangu kupata halmashauri yake ni moja kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga kwenye pwani ya Tanzania.

Mwaka 2012 mji ulikuwa na wakazi 68,308 walioishi katika kata 8 za eneo lake.

Mwaka 2012 eneo la mji wa Korogwe lilitengwa na Wilaya ya Korogwe ya awali na kuwa na halmashauri yake ya pekee.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 86,551 [1].

Pia ni makao makuu ya Dayosisi ya Kanisa la Anglikana ya Tanga.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Korogwe ilianza kama makazi ya kundi la Wasigua (waliojiita pia Waruvu) kwenye kisiwa cha mto Ruvuma. Hapa palikuwa na mkutano wa njia mbili za misafara kutoka Ziwa Viktoria Nyanza na nyingine kutoka Ugogo.

Wakati wa ukoloni wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kulikuwa na kituo cha posta[2], wakati wa koloni ya Tanganyika Korogwe ilikuwa makao makuu ya wilaya [3].

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Kamusi ya Koloni za Kijerumani, makala "Korogwe"
  3. Korogwe District, linganisha Forgotten Mandate: A British District Officer in Tanganyika by E. K. Lumley, uk. 80, iltazamiwa kwa google books Mei 2016
Kata za Wilaya ya Korogwe Mjini - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Bagamoyo | Kwamndolwa | Kwamsisi | Kilole | Magunga | Majengo | Manundu | Masuguru | Mgombezi | Mtonga | Old Korogwe

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Korogwe (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.