Kaizari Karoli V
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kaisari Karoli V)

Karoli V (pia: Carlos I wa Hispania[1]; 24 Februari 1500 – 21 Septemba 1558) alikuwa Kaizari wa Dola Takatifu la Kiroma[2] kuanzia 1519 hadi kujiuzulu mwezi wa Septemba 1556.
Alimfuata babu yake, Maximilian I, na kufuatiwa na mdogo wake Ferdinand I.
Kwa jina la Carlos I alikuwa mfalme wa kwanza wa Hispania tangu mwaka 1516. Kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa na makoloni mengi hasa barani Amerika, aliweza kusema, "Katika ufalme wangu jua halitui kamwe".
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Karoli, Carlos, Karl, Charles, Carlo, ni maumbo tofauti ya jina lilelile la asili ya Kigermanik katika lugha mbalimbali za Ulaya
- ↑ Dola Takatifu la Kiroma lilikuwa jina la milki iliyounganisha Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji pamoja na maeneo kadhaa ya Italia, Ufaransa na Ucheki wa leo katika enzi ya kati hadi 1806.
![]() |
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Ujerumani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kaizari Karoli V kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |