Nenda kwa yaliyomo

Joseph Keter

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali
Riadha ya Wanaume
Anawakilisha nchi Kenya
Michezo ya Olimpiki
Dhahabu 1996 Atlanta Mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa Wanaume

Joseph Keter (amezaliwa 13 Juni 1969) alikuwa mwanariadha wa Kenya, mshindi wa shindano la mita 3000 kuruka vizuizi na Kidimbwi cha maji katika Michezo ya Olimpiki ya 1996.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa mjini Lessos, Wilaya ya Nandi mnamo 13 Juni 1969.

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Yeye ni ofisa wa Jeshi la Nchi Kavu la Kenya. Alikuwa tu na msimu mmoja wa mafanikio katika kazi yake ya riadha wakati alishinda dhahabu katika Mashindano ya Olimpiki.

Nishani yake ya Dhahabu

[hariri | hariri chanzo]

Katika michezo ya Olimpiki ya Atlanta, anayeshikilia rekodi ya dunia katika shindano la mita 3000 kuruka viunzi na maji, Moses Kiptanui alikuwa akipigiwa upato kushinda lakini alipokea upinzani mkali kutoka kwa Keter katika finali. Wawili hawa walikuwa wamefika kidimbwi cha mwisho wakiwa sako kwa bako lakini Keter akafungua mwanya na kumwacha mwenzake, huku akishinda mbio hizo kwa tofauti ya sekunde 1.11.

Baada ya Olimpiki, Keter alimshinda Kiptanui tena jijini Zürich, huku akiweka muda wake bora zaidi wa 8.05.99. Baada ya msimu huo wa kusisimua, Keter aliendelea kukimbia kwa misimu mingine na akashinda mashindano ya IAAF Grand Prix katika shindano hili hilo mnamo 1997.