Entomolojia
Entomolojia (kwa Kiingereza "entomology" kutoka maneno ya Kigiriki ἔντομον, entomon, "mdudu"; na -λογία, -logia, "elimu") ni sayansi ya wadudu. Watu ambao hujifunza wadudu wanaitwa wanaentomolojia. Wadudu wamekuwa wakisomwa tangu nyakati za awali, lakini haikuwa mapema kama karne ya 16 kwamba wadudu walisomwa kisayansi.
Wataalamu wengine wanajifunza jinsi wadudu wanavyohusiana. Wengine hujifunza jinsi wadudu wanavyoishi na kuzaa kwa sababu hatujui mengi kuhusu aina fulani za wadudu. Wataalamu wengine wanajifunza njia za kuweka wadudu mbali na mazao ambayo watu huyatumia kama chakula. Kuna mabilioni ya aina zisizojulikana ulimwenguni kote na wataalamu wa taksonomia au uainishaji wanajumuisha wapya waliopatikana.
Wanaentomolojia hukutana ili kuzungumza juu ya utafiti wao wa wadudu na kushiriki mawazo, kama wanasayansi wote wanavyofanya.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Entomolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |