Nenda kwa yaliyomo

Bwawa la Turkwel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bwawa la Turkwell ikiangaliwa kutoka angani

Bwawa la Turkwel (pia: Turkwell) ni bwawa lililoundwa katika magharibi ya Kenya kwa kujenga lambo la kuzuia mwendo wa mto Turkwel kaskazini mwa Kapenguria kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi.

Bwawa hilo huwa na madhumuni mbalimbali kama vile uzalishaji wa umememaji, umwagiliaji,uvuvi na utalii.

Lambo lilijengwa kati ya 1986 na 1991 likiwa na kituo cha umeme ambacho ni kikubwa cha tatu nchini chenye uwezo wa kuzalisha megawati 106 . [1]

Ukuta wa lambo ni mrefu nchini Kenya ukiwa na kimo cha mita 153.

Kituo cha umeme kimejengwa chini ya ardhi kina jenereta mbili zenye rafadha za megawati 56.

Tofauti ya mwinuko kati ya bwawa na kituo cha umeme ni kumudu mita 356. [2]
  1. Turkwel History. tovuti ya Kengen.coi.ke, iliangaliwa 22 Februari 2015
  2. "Tender for Rehabilitation of Turbine Governor & Control Equipment, Excitation System, Generator & Transformer Protections Systems and MV/LV Supply Distribution System for Turkwel Hydro Power Station-Kenya" (PDF). Kenya Electricity Generating Company Limited. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 22 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]