Buskerud
Buskerud ni moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo limepakana na Akershus, Oslo, Oppland, Sogn og Fjordane, Hordaland, Telemark, na Vestfold. Ofisi ya utawala ya jimboni hapa ipo mjini Drammen.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Buskerud inaanzia kutoka Hurum katika Oslofjord hadi katika milima ya Halling na Hardanger. Kikawaida jimbo hugawanyika katika wilaya za zamani. Ambazo ni Eiker, Ringerike, Numedal na Hallingdal. Hønefoss ni wilaya kuu ya Ringerike.Upande wake wa magharibi ni milima na mabonde Uwanda wa misitu na ya juu, malisho ya nyasi; sehemu yake ya mashariki ina bonde tambarare na maziwa mengi na mito. Tyrifjorden na Krøderen ni miongoni mwa maziwa makubwa. Numedalslågen, ziwa la tatu ambalo ni refu sana nhini Norwei, linanza mjini Hordaland, linapitia Buskerud hadi Vestfold ambapo inakutana na bahari, wakati mto Begna unamwagikia katika ziwa Sperillen.
Manispaa
[hariri | hariri chanzo]Ukubwa | Jina | Wakazi[1] | Eneo km² |
---|---|---|---|
1 | Drammen | 62,566 | 136 |
2 | Ringerike | 28,806 | 1,437 |
3 | Kongsberg | 24,714 | 761 |
4 | Lier | 23,267 | 283 |
5 | Nedre Eiker | 22,687 | 116 |
6 | Røyken | 18,894 | 112 |
7 | Øvre Eiker | 16,616 | 421 |
8 | Modum | 12,911 | 468 |
9 | Hurum | 9,045 | 156 |
10 | Hole | 5,976 | 135 |
11 | Ål | 4,672 | 1,083 |
12 | Gol | 4,479 | 517 |
13 | Hol | 4,422 | 1,669 |
14 | Sigdal | 3,514 | 813 |
15 | Nes | 3,420 | 776 |
16 | Flesberg | 2,578 | 542 |
17 | Nore og Uvdal | 2,514 | 2,281 |
18 | Krødsherad | 2,117 | 341 |
19 | Hemsedal | 2,087 | 715 |
20 | Rollag | 1,390 | 484 |
21 | Flå | 998 | 674 |
Jumla | Buskerud | 257,673 | 12,336 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Statistisk Sentralbyrå (Kigezo:Kombef). www.ssb.no.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Buskerud fylkeskommune, Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Hallingdal
- Ringeriks region
- Drammens region
- Vest region
60°30′00″N 09°30′00″E / 60.50000°N 9.50000°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Buskerud kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |