Andrea Bobola
Mandhari
Andrea Bobola, S.J. (Sandomir Palatine, Polandi, 1591 – Janów, leo nchini Belarus, 16 Mei 1657) alikuwa padri mmisionari na hatimaye mfiadini wa Shirika la Yesu, anayejulikana kama "mtume wa Lithuania" na "mwindaji wa roho" kwa sababu alijitosa kurudisha umoja kamili kati ya Wakristo.[1]
Hatimaye alikamatwa na askari, akateswa na kuuawa katika uasi wa Khmelnytsky[2][3].
Alitangazwa kuwa mwenye heri na Papa Pius IX tarehe 30 Oktoba 1853, halafu mtakatifu na Papa Pius XI tarehe 17 Aprili 1938.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Merrick, David Andrew (1891). Saints of the Society of Jesus: With a sketch of the Society. William H. Sadlier. uk. 16.
- ↑ Daurignac, J. M. S. (1865). History of the Society of Jesus From Its Foundations to the Present Time (Volume II). John P. Walsh. ku. 12–13.
- ↑ "Who is St. Andrew Bobola? - St. Andrew Bobola Parish, Dudley, MA". www.standrewbobola.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-04. Iliwekwa mnamo 2018-08-21.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- Andrew Bobola – Saint of the Roman Catholic Church
- St. Andrew Bobola Polish RC Church in London Ilihifadhiwa 16 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |