Alyson Hannigan
Alyson Hannigan | |
---|---|
Alyson Hannigan mnamo mwezi wa Mei 2015 | |
Amezaliwa | Alyson Lee Hannigan 24 Machi 1974 Washington, D.C., Marekani |
Jina lingine | Alyson Denisof |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1986–hadi sasa |
Ndoa | Alexis Denisof (tangu 2003- hadi sasa) |
Watoto | 2 |
Alyson Lee Hannigan (amezaliwa tar. 24 Machi, 1974) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kucheza uhusika wa Willow Rosenberg kwenye mfululizo wa kipindi cha Televisheni cha Buffy the Vampire Slayer (1997–2003), Lily Aldrin kwenye ucheshi wa How I Met Your Mother kupitia TV ya CBS (2005–hadi sasa) na Michelle Flaherty katika mfululizo halisi wa filamu za American Pie (1999; 2001; 2003; 2012).[1]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Hannigan alizaliwa mjini Washington, D.C. ni mtoto pekee wa Bi. Emilie (Posner) Haas, wakala wa masuala ya ardhi na viwanda, na Bwana Al Hannigan, dereva wa magari makubwa ya safari.[2] Baba'ke ni Mwamerika mwenye asili ya Ireland na mama'ke ni Myahudi.[3][4] Wazazi walitalikiana wakati ana umri wa miaka miwili tu na muda mwingi alilelewa na mama'ke tu huko mjini Atlanta, Georgia.[5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]1978 – 1996
[hariri | hariri chanzo]Akiwa na umri wa miaka minne, Hannigan akaanza kuonekana katika matangazo.[6] Alihamia mjini Hollywood akiwa na umri wa miaka 11.[7] Akiwa anaishi na mama'ke na baadaye kuhitimu katika shule ya North Hollywood High School, baadaye akajiunga na Chuo Kikuu cha "California State", Northridge ambapo alipata shahada ya saikolojia.
Uhusika mkubwa kabisa wa kwanza wa Hannigan wa kwenye filamu ya My Stepmother Is an Alien,[1] toleo la ubunifu wa kisayansi ambalo pia linavichekesho ndani yake mnamo 1988; mmoja kati ya washirika wenza katika filamu hiyo alikuwepo mwigizaji Seth Green, ambaye baadaye aliungana nae kama muhusika wa kawaida katika tamthilia ya Buffy akiwa kama bwana wake. Kisha mwaka wa 1989, uhusika wake wa kawaida wa kwanza kwenye mfululizo wa TV ulikuja pale aliposhirikishwa kwenye ucheshi mfupi wa Free Spirit.
Akiwa msichana, Hannigan aliwatunza watoto wa Bob Saget, ambaye baadaye alikuja kuhadithia katika mfululizo wake wa TV , How I Met Your Mother.[8]
1997 – hadi sasa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka wa 1997, Hannigan alichaguliwa kucheza uhusika wa Willow Rosenberg, rafiki wa karibu wa Buffy Summers, katika mfululizo wa televisheni wa Buffy the Vampire Slayer.[9] Kipindi hicho kilipata mafanikio makubwa mno, na Hannigan akapata kutambulika vya kutosha, hatimaye kuonenakana katika nyusika maarufu kadha wa kadha ambazo zililenga hasa watazamaji vijana, ikuwa ni pamoja na American Pie, American Pie 2, Boys and Girls na American Wedding.[1] Pia alipata kuonekana kiduchu kwenye mfululizo unaotokana na hadithi ya Buffy, Angel, akitumia tena uhusika wake uleule wa Willow katika vipengele kadhaa (ikiwa ni pamoja na "Orpheus," wakati wa msimu wa nne wa Angel na msimu wa saba wa Buffy), lakini hakuna tena baada ya Buffy kumaliza kutayarishwa kwake.
Mwaka wa 2012, Hannigan ameurudia tena uhusika wake wa Michelle kwenye American Reunion.[10]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Hannigan ameolewa na mwigizaji mwenzake wa katika tamthilia ya Buffy the Vampire Slayer Alexis Denisof katika hoteli ya Two Bunch Palms Resort huko mjini Desert Hot Springs, California, mnamo tar. 11 Oktoba, 2003. Wawili hao wana watoto wawili wa kike, Satyana Marie Denisof, amezaliwa mnamo tar. 24 Machi, 2009,[11] na Keeva Jane Denisof, amezaliwa mnamo tar. 23 Mei, 2012.[12] Hannigan ni mama mlezi wa mtoto wa kiume wa Joss Whedon, Arden, na mume wake, Alexis Denisof, ni baba mlezi wake.[13]
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
1986 | Impure Thoughts | Patty Stubbs | Kama Alyson Hannigan |
1988 | My Stepmother Is an Alien | Jessie Mills | |
1991 | Switched at Birth | Gina Twigg, Umri 13–16 | Filamu ya TV |
1995 | The Stranger Beside Me | Dana | Filamu ya TV |
1996 | Case for Life | Iris | Filamu ya TV |
1996 | For My Daughter's Honor | Kelly | Filamu ya TV |
1998 | Dead Man on Campus | Lucy | |
1999 | Hayley Wagner, Star | Jenna Jakes | Filamu ya TV |
1999 | American Pie | Michelle Flaherty | |
2000 | Boys and Girls | Betty | |
2001 | American Pie 2 | Michelle Flaherty | |
2001 | Beyond the City Limits | Lexi | |
2003 | American Wedding | Michelle Flaherty | |
2004 | Americana | Andrea | Filamu ya TV |
2005 | In the Game | Haijulikani | Mfululizo wa TV |
2006 | Date Movie | Julia Jones | |
2011 | Love, Wedding, Marriage | Courtney | Amecheza na mume wa maisha ya kweli Alexis Denisof |
2012 | American Reunion | Michelle Flaherty-Levenstein |
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
1989–1990 | Free Spirit | Jessie Harper | Muhusika mkuu; vipengele 14 |
1990 | Roseanne | Jan | Kipengele: "Like, a New Job" |
1993 | Almost Home | Samantha | Kipengele: "The Dance" Episode: "Hot Ticket" |
1994 | Touched by an Angel | Cassie Peters | Kipengele: "Cassie's Choice" |
1996 | Picket Fences | Peggy Patterson | Kipengele: "To Forgive Is Devine" |
1996 | Friends for Life | Emma Daniels | Unaired TV Pilot |
1997–2003 | Buffy the Vampire Slayer | Willow Rosenberg | Muhusika Mkuu; vipengele 144 |
1999–2000 | 100 Deeds for Eddie McDowd | Gigi | Kipengele: "Dogs Day Out" Episode: "The Return of Gigi" |
2000 | Wild Thornberrys | Gerda | Kipengele: "Every Little Bit Alps" |
2001–2003 | Angel | Willow Rosenberg | Kipengele: "Disharmony" Kipengele: "There's No Place Like Plrtz Glrb" Episode: "Orpheus" |
2004 | That '70s Show | Suzy Simpson | Kipengele: "Sally Simpson" Episode: "Won't Get Fooled Again" |
2004 | King of the Hill | Stacey Gibson | Kipengele: "Talking Shop" |
2005 | Veronica Mars | Trina Echolls | Kipengele: "Ruskie Business" Kipengele: "Hot Dogs" Kipengele: "My Mother, the Fiend" |
2005–hadi sasa | How I Met Your Mother | Lily Aldrin | Uhusika Mkuu |
2009 | Goode Family | Michelle | Kipengele: "Graffiti in Greenville" |
2011 | The Simpsons | Melody | Msimu wa 22: Kipengele 11: "Flaming Moe" |
2011 | American Dad | Chelsea | Msimu wa 7: Kipengele cha 5: "Virtual In-Stanity" |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 "How I Met Your Mother Cast: Alyson Hannigan". CBS. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-31. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
- ↑ "Film Reference Alyson Hannigan Bio". Filmreference.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2010-03-07.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Bloom, Nate (2004-07-09). "Celebrity Jews". the Jewish News Weekly of Northern California. Iliwekwa mnamo 2006-07-16.
- ↑ Pearce, Garth. "Alyson Hannigan Interview", The Sunday Times, 2003-07-13. Retrieved on 2007-07-12.
- ↑ Biography for Alyson Hannigan at the Internet Movie Database
- ↑ "Interview: Alyson Hannigan on American Pie". Scotland on Sunday. Aprili 22, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-16. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Former Atlantan Alyson Hannigan interview for 'How I Met Your Mother'". The Atlanta Journal-Constitution. Septemba 21, 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-22. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "It's Evening in America". Vanity Fair. May 2012. Page 158.
- ↑ "Where Are They Now? Buffy the Vampire Slayer". People. Desemba 3, 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-02. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Alyson Hannigan, Cobie Smulders and 'Mother'-hood". USA Today. Aprili 15, 2012. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wihlborg, Ulrica (2009-03-31). "Alyson Hannigan Welcomes a Daughter!". People. Iliwekwa mnamo 2009-03-31.
- ↑ "Alyson Hannigan and Alexis Denisof Welcome Daughter Keeva Jane". People. Juni 12, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-02. Iliwekwa mnamo 2012-06-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hannigan is godmother of Joss Whedon's son, Alyson Hannigan.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Angalia mengine kuhusu Alyson Hannigan kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
picha na media kutoka Commons | |
nukuu kutoka Wikiquote |