Accra
Jiji la Accra | |
Nchi | Ghana |
---|---|
Mkoa | Greater Accra |
Wilaya | Accra Metropolis |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 2,270,000 (1,910) |
Tovuti: ama.ghanadistricts.gov.gh |
Accra ni mji mkuu wa Ghana ukiwa na wakazi 1 650 000[1]. Accra ni kitovu cha uchumi, biashara na mawasiliano ya nchi. Iko ndani ya mkoa wa Accra Kuu.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Accra ilianzishwa na Waga katika karne ya 15 BK kama kituo cha biashara na Wareno. Wareno walijenga boma kwa ajili ya biashara hiyo na Waswidi, Waholanzi, Wafaransa, Waingereza na Wadenmark walifuata.
Eneo la Accra ya leo liliendelea kuwa mji kati ya boma tatu za Uingereza (Jamestown), Denmark (Osu) na Uholanzi (Ussherstown). Maeneo hayo matatu leo ni kitovu cha mji wa kisasa.
Baada ya Waingereza kushinda Waashanti, Accra ikawa mji mkuu wa koloni la Pwani la dhahabu. Mji uliendelea kukua baada ya kujengwa kwa reli na bandari.
Katika miaka ya 1940 Accra ilikuwa pia mwanzo wa upinzani dhidi ya Waingereza ulioleta uhuru wa Ghana mwaka 1956.
Leo hii Accra imepata mji pacha wa karibu wa Tema baada ya kuhamishwa kwa viwanda na bandari kwenda Tema inayounganishwa na Accra yenyewe kwa reli na barabara kuu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Archived 28 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Accra Taxi Ride Archived 15 Julai 2006 at the Wayback Machine. - video inayoonyesha safari ya Taxi katika Accra (Kiingereza)
- Mark Moxon, Travel Writer - Makala kuhusu ziara katika Accra mwaka 2002 (na picha) (Kiingereza)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Accra kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |