Nenda kwa yaliyomo

Sayyid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 07:21, 17 Oktoba 2017 na Riccardo Riccioni (majadiliano | michango)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Sayyid (سيد) ni cheo cha heshima cha Kiarabu kinachomaanisha hasa ukoo wa kiume wa Mtume Mohammad.

Maana ya Kiarabu

[hariri | hariri chanzo]

Kimsingi "sayyid" yamaanisha "Bwana": ni namna ya kumtaja mtu kwa heshima. Hutumiwa hivyo katika nchi nyingi za Waarabu. Katika lahaja ya Moroko yafupishwa kuwa "sidi" (kutoka sayyidi - Bwana wangu).

Maana ya Kiislamu

[hariri | hariri chanzo]

Hata nje ya Waarabu neno linatumiwa kati ya Waislamu kama cheo cha heshima kwa ukoo wa Mtume Muhammad. Mara nyingi lataja wote wanaohusiana na Husain na Hasan wajukuu wa Mtume kupitia binti yake Fatima na Ali ibn Abi Talib.

Mara nyingi ni watu wa ukoo wa Husain tu wanaoitwa "sayyid" ilhali hao wamepewa cheo cha "sharif". Lakini siku hizi "sayyid" hutumiwa pia kwa wote.

Mabinti wa sayyid wa kiume huitwa "sayyida" isipokuwa watoto wa sayyida na baba asiye sayyid hawapokei cheo hiki.

Kati ya Dawoodi Bohra cheo "syyedina" hutumiwa kwa kiongozi mkuu wao kwa maana ya kimsingi ya Kiarabu "Bwana wetu" hata kama yeye hatoki katika ukoo wa Fatima.

Masayyid wa uwongo

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia watu wengi walijipatia cheo hiki kwa sababu ya heshima na pia faida za kiuchumi kwa sababu masayyid walisamehewa kodi mbalimbali katika milki ya Osmani.

Hivyo Waosmani waliunda ofisi ya kusimamia Masayyid na kukinga cheo hiki dhidi ya "muhtasayyid" yaani masayyid wa uwongo.

Tovuti ya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sayyid kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.