Kitswana
Mandhari
Kitswana ni lugha ya Kibantu nchini Botswana na Afrika Kusini inayozungumzwa na Watswana. Ni lugha ya taifa nchini Botswana. Katika sensa ya mwaka wa 2011 idadi ya wasemaji wa Kitswana nchini Afrika Kusini imehesabiwa kuwa watu 4,070,000. Nchini Botswana, kuna wasemaji 1,070,000 (1993). Pia kuna wasemaji 29,400 nchini Zimbabwe (1969) na wasemaji 12,300 nchini Namibia (2006). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitswana iko katika kundi la S30.
Viungo vya nje
- lugha ya Kitswana kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kitswana
- lugha ya Kitswana katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/tsn
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitswana kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |