0% found this document useful (0 votes)
2K views29 pages

MAKALA YA Bina-Adamu!

This document analyzes the motif of journey in the Kiswahili novel Bina-Adamu! by K.W. Wamitila. It identifies 19 different journeys undertaken by the main character throughout the novel. Each journey presents themes that contribute to the overall journey of liberation in the story. The journeys depict the lives of Africans before, during, and after colonialism in relation to events happening elsewhere in the world. The analysis shows how the writer skillfully used multiple distinct journeys by a single protagonist to effectively convey their themes.
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as DOCX, PDF, TXT or read online on Scribd
0% found this document useful (0 votes)
2K views29 pages

MAKALA YA Bina-Adamu!

This document analyzes the motif of journey in the Kiswahili novel Bina-Adamu! by K.W. Wamitila. It identifies 19 different journeys undertaken by the main character throughout the novel. Each journey presents themes that contribute to the overall journey of liberation in the story. The journeys depict the lives of Africans before, during, and after colonialism in relation to events happening elsewhere in the world. The analysis shows how the writer skillfully used multiple distinct journeys by a single protagonist to effectively convey their themes.
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as DOCX, PDF, TXT or read online on Scribd

MBURU C.

KIARIE

MOTIFU YA SAFARI KATIKA RIWAYA YA Bina-Adamu!


MBURU C. KIARIE
______________________________________________________________________________
Uchambuzi na uhakiki wa kazi ya fasihi andishi huhusu riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi andishi. Ambapo,
maudhui, wahusika na fani huchunguzwa. Fani ya motifu ya safari imetumika katika riwaya ya kihistoria ya BinaAdamu! ya K.W. Wamitila. Lengo kuu la makala haya likiwa ni kuchunguza namna motifu ya safari katika riwaya
hii ya Bina-Adamu! Nia ikiwa ni kuonyesha safari tofauti zilipo riwayani na kufafanua kwa fasili namna safari
zilizopo zinawasilisha maudhui yapi riwayani. Matokeo ya uchunguzi yanabainisha kuwa; kuna safari 19 tofauti
riwayani, kila safari ina maudhui yanayochangia kujenga safari kuu riwayani ambayo ni safari ya ukombozi. Safari
zilizopo zinaeleza maisha ya Mwafrika kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni hadi kufikia sasa
yakihusishwa na yaliyokuwa yakiendelea katika sehemu nyingine za dunia.
The study of written literature involves novels, plays, short stories and poetry where criticism on the theme, characters
and the stylistic devices is done. This study concerns one of the historic Kiswahili novels by K. W Wamitila, BinaAdamu!, where a stylistic device of Journey motif has been used. The objective of the study was to show how the
journey Motif has been used in the Novel. This aimed at identifying the various journeys made in the novel and the
theme presented by each of the journeys and to give an interpretation of the journeys made in the novel. The study
found that: there are 19 different journeys in the novel and that every journey presents various themes that contribute in
building the main journey in the novel. The interpretation of the journeys give a detailed account of the African nations
before the onset of colonialism, during the colonial era and after the colonial era to date in relation to what was
happening in the rest of the world in the three eras.

______________________________________________________________________________
UTANGULIZI
Katika riwaya ya Bina-Adamu!, mbinu ya kimtindo ya kutumia safari imetumia kwa wingi
katika juhudi za mwandishi kuwasilisha maudhui yake. Hadithi imejengeka katika safari 19
ambazo zilifanywa na mhusika mkuu kuanzia mwanzoni mwa riwaya hadi mwisho wake.
Mchango wa makala haya ni kutoa maelezo ya kina ya namna ambavyo mwandishi wa riwaya
hii K.W. Wamitilla alivyofaulu katika kutumia safari nyingi tofauti zilizo na lengo moja katika
hadithi moja ili kufanikisha kuwasilisha maudhui yake. Mwandishi walifaulu katika kufanya hivi
kwani kila safari tofauti ili sheheni udhui mahsusi.

DHANA YA MOTIFU YA SAFARI


Casano (2014) anaeleza kuwa, motifu hutumiwa katika tungo za kifasihi zilizo vitabuni,
filamuni, na katika ushairi pale inapotumiwa kama mbinu ya kisanaa na watunzi. Anasema kuwa,
motifu yaweza kuwa chochote kile; wazo, kitu, falsafa fulani, hali, mhusika, mandhari, tukio, au
1

MBURU C. KIARIE

usemi. Motifu hutumiwa kuibua dhamira, maudhui, mtazamo fulani na huwa na maana
iliyofumbwa. Ndumbaro (2013) alishughulikia msingi wa kuwepo kwa motifu za aina anuai za
fasihi za mataifa na makabila tofautitofauti ulimwenguni. Aliainisha uwepo wa motifu kadha
katika fasihi hizo. Zikiwemo; motifu za dhamira, motifu ya ujumbe, motifu ya wahusika, motifu
ya mtindo, motifu ya falsafa, na motifu ya mandhari. Tafiti hizi hazikushughulikia nasafi ya
safari katika tungo za kiriwaya hasaa riwaya ya Bina-Adamu!.
Wamitila (2008), anaelezea motifu ya safari kuwa ni sehemu muhimu ya utunzi wa ngano
hivi kwamba, ngano nyingi zilihusisha wahusika kufunga safari. Aidha safari zenyewe zikiwa za
mhusika shujaa akiondoka kwenda kufikisha ujumbe, kwenda kutafuta suluhu kwa tatizo la
kijamii, au, kwenda kuiletea jamii ufanisi. Kwa mfano, visasili vingi vimejengeka katika safari
ambazo hufungwa na mhusika mkuu. Mfano ukiwa ni hadithi ya asili ya kifo inayopatikana
katika jamii nyingi za Afrika. Hadithini, wahusika tofauti hutumwa na Mwenyezi Mungu kuja
duniani kumfahamisha mwanadamu kuwa hatakufa na kisha baadaye kutumana kuwa atakufa.
Wanyama mbalimbali wanafungishwa safari kufikisha ujumbe huu. Motifu ya safari hapa
inatumiwa kukuza kisasili chenyewe. Motifu ya safari hapa inahusu safari mbali mbali za
wahusika tofauti hali ambayo ni tofauti na yaliyotafitiwa na utafiti huu ambapo safari zilizopo ni
tofauti zikifanywa na mhusika mmoja.
Motifu ya safari katika riwaya ya Bina-Adamu!
Sehemu hii imebainisha safari zilizopo katika riwaya ya Bina-Adamu!. Safari zote
zilizofanywa na mhusika mkuu zimetambulishwa kama zilivyojitokeza riwayani na kutolewa
fasili kwa mujibu wa nadharia ya utafiti ya umuundoleo. Muhimili wa nadharia utakaotumiwa
katika sehemu hii yote ukiwa ni ule unaodai kuwa maana ya utungo wa kifasihi hutegemea
ufahamu na uelewa aliyonao msomaji. Kwa kuwa riwaya hii ni ya kihistoria na inahusisha
wahusika wa kihistoria, ufasili utatolewa kulingana na matukio halisi ya kihistoria yaliyotukia
katika hali halisi duniani, kama yalivyotendwa na wahusika wa kihistoria katika jamii na nchi
zao.
Mhusika mkuu ambaye ni msimulizi wa hadithi, pia anaweza kurejelewa kama Msafiri. Fasili
yake ikiwa mkombozi. Kutokana na ukaidi wake anaamua kufunga safari kuelekea kwenye kiini
2

MBURU C. KIARIE

cha kijiji chake sehemu ambayo iliogopwa na kuaminiwa kuwa aliyeelekea huko angepatwa na
madhara makubwa. Uamuzi huu wake unakuwa mwanzo wa safari nyingine nyingi zikifuatana
moja baada ya nyingine kuelekea maeneo tofauti ya ulimwengu. Hali hii ya safari kufuatana
inaafikiana na dondoo alilolitumia mwandishi mwanzoni mwa riwaya alipomnukuu Elliot T.S.:
Tukiitacho mwanzo aghalabu ni hatima na hatima kuifikia ni kufanya [Link]
katika uvumbuzi wetu na hatima ya uvumbuzi kwetu itakuwa kufika tulipoanzia na
kupajua pahali hapo kwa mara ya kwanza (Wamitila, 2002, Uk 5).
Utafiti huu umebainisha kuwa kila safari iliyopo riwayani husababisha kuzuka kwa safari
nyingine. Iliyotangulia ifikapo mwisho wake, nyingine inaanza. Hali huwa hivi kuanzia mwanzo
wa riwaya hadi mwisho wa riwaya. Jambo linalobakia kuwa fumbo ni ikiwa safari zote
zilizofungwa zilikuwa ni ndoto au hali halisi katika maisha ya mhusika huyu mkuu riwayani.
1 Safari ya Ukaidi
Safari hii tutaiita ya ukaidi kwani inatokana na ukaidi wa msimulizi dhidi ya maonyo ya
nyanyake aliyemchukulia kuwa mwongo. Alikaidi itikadi ya jamii kuwa sehemu ile iliyokuwa
kiini au kitovu cha kijiji ilikuwa hatari. Nia yake ilikuwa kwenda kuwasaka huntha watatu
ambao akiwapata ataweza kukirejesha kijiji chake katika hali yake ya kawaida kwani mambo
yalikuwa yamewaharibikia katika kila hali. Anayokumbana nayo ni dhihirisho kuwa sehemu hii
haikuwa salama kwani: alihisi kufuatwa na asiyemuona, alimkuta Mkazi wa tatu ambaye
alifahamu kufika kwake bila ya kumgeukia na baadaye kugeuka kuwa kunguru alipomkaribia,
radi ilipiga kukiwa na jua kali, kisha mwanga mkubwa uliomwingia macho na kumtia kiwi na
kumfanya kutoweza kuona hali iliyofuatwa. Jua linatoweka ghafla na giza kuingia. Anapigwa
makofi na mateke na wasioonekana. Anasikia vicheko vya wasichana-wavulana wasiooenekana,
na baadaye anashikishwa mkongojo kwa lazima. Sauti za bundi na watu wasioonekana
waliolalamikia na kumtusi kwa kukanyagwa zikafuata. Kwa mujibu wa nadharia ya utafiti
mwandishi hapa anaonyesha jinsi uamuzi wa mkombozi yeyote yule huwa ni hatari. Kuongoza
harakati za ukombozi ni kujiingiza katika siasa na siasa ni mchezo hatari ulio na changamoto na
vikwazo vingi na wakati mwingine huhatarisha maisha. Ndiposa mwandishi anasema kuwa siasa
zimelaaniwa na yeyote ajiingizaye kwenye siasa huwa amejitosa kwa mateso, matusi, vita,
kulaaniwa na maovu mengine.
3

MBURU C. KIARIE

Safari ya pili inaanza hapa pale msafiri anapoona mwanga upande wa mbele gizani na
kuamua kuufuata. Fasili hapa kwa mujibu wa nadharia ikiwa hata uamuzi wake ukionekana
kuwa mgumu na hatari bado kuna matumaini yanayowakiliswa na mwangaza ulikuwa gizani.
Haya yanapatikana kati ya ukurasa wa 7 hadi wa 11. Kwa mfano katika tunaambiwa:
Ile radi ilipiga tena kisha ghafla jua likaanza kupotea na giza kuanza kueneaenea. Sasa
nilijua kuwa ilikuwa wazi kama ilivyosemwa. Kijiji hiki kilikuwa kijiji cha mazimwi;
mazimwi yanayowala watu. Jua liliendelea kuzama. Jua linamezwa na mashetani
(Wamitila, 2009, Uk 9).
Mfano mwingine ni katika ukurasa wa 11 ambapo Msafiri anaeleza:
Nilitafuta mkongojo wa kutembelea. Sehemu iliyokuwa nyuma ilikuwa na mti fulani;
niliuona kabla jua halijazama ghafla. Nilirudi kuufuata. Ahhhhh, umenikanyaga mbavu,
mjinga. Unatafuta nini huku? Udaku wenu unakupelekeni wapi siku hizi? Ililia sauti ya
[Link] sikuona mtu yeyote. (Wamitila, 2002, Uk.11)
2. Safari kupitia Njia ya Uhalisia
Safari hii inafanyika kuanzia ukurasa wa 12 hadi ukurasa wa 15. Msafiri anatembea katika
giza totoro na anaongozwa na viunzi kadha vya binadamu vilivyokuwa mifupa iliyotoa
mwangaza. Kulingana na muhimili wa nadharia ya umuundoleo unatuoongoza katika sehemu
hii, mifupa inayotoa mwangaza yawakilisha dhana kuwa ufahamu alionuia kuutafuta
utaongozwa na yaliokuwa yametendeka hapo zamani yaani historia inayohusu waliomtangulia au
matukio ya kihistoria yaliyohitaji ukombozi upatikane. Azima ya ukombozi ya walikata tamaa na
matumaini yatakuwa msukumo wa kumwongoza.
Walifika palipokuwa na kiingilio cha pango kilichokuwa kimeandikwa NJIA YA
UHALISIA. Maandishi haya kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo yakimaanisha kuwa
Msafiri anaelekea kufunuliwa mambo yanayodhihirisha uhalisia unayoikumba jamii yake. Hii
ilikuwa njia ndefu iliyopitia chini ndani ya pango. Utelezi mkubwa uliotokana na kinyesi cha
popo uliokuwapo unasababisha ateleze na kumteremsha kwa kasi ya ajabu hadi sehemu ya chini.
Anapotokezea anakumbana na jitu refu ajabu lililokuwa limeandikwa UMERO JAPA
mgongoni. Maandishi ambayo kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo maana yake ikiwa ni
uhalisia katika jamii ya kisasa unaoongozwa na kutawaliwa na mataifa yenye uwezo
yakiwakilishwa na Uingereza, Marekani, na Japan. Mataifa haya huendeleza dhuluma
4

MBURU C. KIARIE

zinazoelezwa kuwa za kibeberu dhidi ya mataifa nayoendelea kama ya Afrika. Ndiposa


yanasemekana kuwa jitu linanuka kama beberu.
Msafiri anakumbana na watu watatu: Mhubiri, Mwanafalsafa na Mwanasayansi. Kulingana
na mhimili wa nadharia unaotuongoza hapa, mhubiri anawakilisha imani za dini na masuala
yake, mwanafalsafa akiwakilisha ufahamu wa kina wa mambo yanayohusu uongozi na siasa,
naye mwasayansi akiwakilisha elimu sayansi na teknolojia. Mambo haya matatu ndiyo hutawala
maisha ya mwanadamu kila siku na lazima msafiri aweze kuyaelewa. Wanamfahamisha kuwa
mbali na kukumbana na lile jitu lililokuwa na harufu ya beberu atakumbana na mengine mengi.
Katika safari hii anapitia mateso kadha yakiwemo: kupigwa teke, kofi na fimbo na mtu
asiyemuona, aliyekuwa akimwelekeza, kuumizwa masikio na sauti iliyomkirihi masikio,
kupambana na popo waliokuwa wengi ajabu, kupambana na hofu aliyotiwa na kuwapo kwa
bundi wengi na sauti zao. Safari inaingia mkondo mwingine alipotumbukia katika mto uliokuwa
na maji mengi ajabu lakini hawakuzama na badala ya kuteremshwa na mkondo wa maji
walivutwa nyuma kwa kasi ya ajabu. Mwisho wa safari hii kunaelezwa hivi:
Hatukwenda sana kabla ya kutumbukia kwenye mto uliokuwa na maji mengi ajabu.
Lakini hatukuzama; badala yake tulielea juu juu. Mwenzangu alinishikilia na kiasi fulani
nikajihisi kama Petro aliyetembea juu ya maji. Lakini badala ya kwenda mbele, mkondo
wa maji ulituvuta tukawa tunarudi nyuma tena kwa kasi ya ajabu. (Wamitila, 2002, Uk.
15)
Yaani, Msafiri anarudishwa nyuma kwa matukio ya awali ya kihistoria yaliokuwa yametokea
ulimwenguni na katika maisha yake ayaelewe kwanza ili aweze kuelewa hali inayoikabili jamii
yake ilianzia wapi na kwa nini iko jinsi ilivyo. Kwa kutumia mhimili wa ulioteuliwa ya
umuundoleo, Mkombozi alitakiwa kuelewa kuwa jukumu alilojitwika lahitaji kwanza aweze
kujielea. Pia alifaa aelewe historia ya jamii yake. Ufahamu huu ungemwezesha kupiga hatua
mbele.
3. Safari ya kurudi utotoni
Safari hii inafanyika kati ya ukurasa wa 16 hadi 20. Msafiri anajipata kijiji alichofahamishwa
kilijulikana kama Zakongwe baada ya safari ya majini kukatizwa alipopigwa kwa kishindo
kikubwa hadi kando ya mto. Fasili hapa kwa mujibu wa nadharia inayoongoza utafiti huu ikiwa
5

MBURU C. KIARIE

kuwa Mkombozi amerudishwa nyuma kwa matukio ya zamani ya kihistoria miaka ya kabla ya
kufika kwa usasa wakati watu hawakuvaa mavazi ya kisasa kama nguo bali walikuwa wakivaa
kipande kidogo tu cha ngozi ya wanyama sehemu ya mbele. Msafiri alifahamishwa na mzee
mmoja wa Zakongwe kuwa:
Ikiwa hujajifunza kuwa kama mtoto huna popote utakapofika. Ulimwengu utaangamia
siku utakapompuuza mtoto. (Wamitila, 2002, Uk. 17)
Wenyeji wake hawakuvaa nguo ila kipande cha ngozi mbele. Alilazimika kucheza michezo
na watoto. Ilibidi Msafiri arudi katika hali ya kutojua kama walivyo watoto wadogo ili aweze
kuanza kuielewa historia ya mambo yaliyoikumba jamii yake hapo zamani kama njia ya
kutayarisha aelewe namna jamii yake ilivyo hivi sasa. Alipovua nguo zake kama wenyeji wake,
mwili wake ukakunjamana na ghafla akarudia utoto akawa na umbo la mtoto na kuwa mmoja wa
wale watoto. Hapa aliishi kwa mzee aliyejulikana kama Babu. Fasiri yaki kwa mujibu wa
nadharia ya umuundoleo ikiwa kiwakilishi cha ufahamu wa historia ya jamii ya Mkombozi .
Babu huyu alimkabidhi mkoba na kumhiviza aitambue na kuienzi asili yake na mila na itikadi za
jamii yake pale anapomwambia:
Utunze huu, ndani mna utu, mapenzi na kiini cha kuwako kwako. Mkoba huu utakufaa
sana siku zijazo. Usiudharau kwa sura; mwacha asili ni mtumwa. (Wamitila, 2002,
Uk.19)
Siku moja, Msafiri walipokuwa katika mchezo wao ya kitoto wa kujificha alikabiliwa na joka
kubwa lilikuwa limeandikwa VITAS mgongoni linalomfanya kuanguka mtoni. Kwa mujibu wa
nadharia ya umuundoleo, yamkini neno VITAS ni jina la jukwani la Kirusi la mhusika Vitaliy
Vladasovich Grachov aliyeimba kwa Kirusi. Kwa hivyo fasili hapa kwa mujibu wa nadharia ni
kuwa, Mkombozi anafahamishwa kuhusu historia ya nchi ya Urusi au Bara Uropa ili afahamu
uhusiano uliokuwapo wa matatizo yanayoikumba jamii yake na bara hili. Huu unakuwa ndio
mwisho wa safari yake ya Zakongwe aliporudi utotoni.
4. Safari na Hanna
Safari hii ipo kuanzia Uk. 21-31. Inaanza Msafiri anapojikuta kwenye mto uliokuwa na maji
yaliyoenda kasi ajabu kuelekea mbele huku akiwa anaelea juu ya maji na mkongojo wake. Safari
yake ya mtoni ilikatizwa na kisiki kikubwa kilichokingama mtoni kilipomgonga na kutupa hadi
6

MBURU C. KIARIE

nchi kavu. Mwangaza wa jua kali ukampofusha macho ghafla na cha kushangaza ni kuwa nguo
zake zilikuwa zimekauka. Mwili wake ulikuwa umerejea utu uzima ila vyanda vya mikono
vilikuwa vya mtoto. Baadaye anakumbana na mwanamke aliyefanana na marehemu mkewe.
Mwanamke huyu alijitambulisha kama Hanna au Anna. Hanna alimfahamisha kuwa atakuwa
msaidizi wake safarini. Wakazi walikuwa makundi mawili: walioishi kwa matumaini, yaani
waliishi kesho na walioishi jana, yaani walioishi kwa mawazo. Hanna anamwongoza Msafiri, na
tunaelezwa jambo la ajabu:
Niliweza kumtambua Hanna kutokana na mwangaza uliokuwa ukikonyeza kwenye
kisogo chake kama wa kimulimuli. Lakini alifika mahali fulani na kupinda sehemu
nyingine na kunipotea..Nilitega masikio na kusikia: Msaidieni jamani! Ana nia nzuri
huyu Bina-Adamu msafiri. Sikuweza kumwona msemaji wake. Nilitulia kisha nikasikia
nimepigwa kofi shavu la kulia. Geuza shavu la pili nilitii kisha nikapigwa kofi jingine.
Haya shika! Sikutambua nilichokuwa nikiambiwa nishike..Nilikuwa nikishikishwa ule
mkongoja wangu. (Wamitila, 2002, Uk 25)
Msafiri anaendelea kwa kufuata viunzi huko mbele hadi wanatokea sehemu ya pili. Msafiri
anaonyeshwa majengo ambayo hayakuwa yamekamilika kwa ajili ya UMERO JAPA.
Alionyeshwa pia machimbo ya madini katika eneo ambalo hakukuwa na mimea ila bundi wengi
mapangoni. Alipitishwa sehemu ya watu wa mabanda mabovu waliokuwa na furaha na akajiunga
nao kula. Hawa ni wale walioishi kesho kwa matumaini. Walimfahamisha Msafiri kuwa alikuwa
na mwendo mrefu wa kwenda huku wakimtakia heri njema. Walidai kuwa waliporwa madini ya
dhahabu, fedha na langa kwa ahadi ya kulipwa lakini hawakulipwa. Wanamkabidhi kibuyu
kilichokuwa na kinywaji fulani. Wakati wa kuondoka unapofika, Hanna anamwongoza na
anaposita anapigwa bakora ya mgongo. Kwa mujibu wa nadharia ya umuunduleo, mwandishi
analenga kuonyesha dhuluma za kiuchumi ambazo mataifa machanga hutendewa na mataifa
yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi. Mataifa haya yenye uwezo yakiwakilishwa na Uingereza,
Marekani na mataifa ya Mashariki ya Mbali yakiwakilishwana Japan, huhadaa mataifa ya Afrika
kwa ahadi za uongo kisha baada ya kupata malighafi na madini wanayoyahitaji wao huondoka
bila kutimiza ahadi zao. Mataifa ya Afrika huachiwa kujiliwaza kuwa huenda kukaja mkombozi
atakaye waokoa dhidi ya wadhalimu hawa. Kibuyu anachokabidhiwa Msafiri kinawakilisha
matumaini na imani walionayo kuwa ataweza kuyarekebisha mambo.
5. Safari kuelekea Milimani
7

MBURU C. KIARIE

Safari hii ipo kati ya Uk 32-41. Hali yake msimulizi inabadilika na kuwa mbilikimo.
Anaongozwa safari na wale viunzi hadi kijiji cha Ropa kilichokuwa na majengo mabovu huku
watu wakiwa wamejishika tama kwani wamekata tamaa. Katika hali halisi kijiji cha Ropa ni
kijiji kinachopatikana Kusini mwa nchi ya Poland. Anakabiliana na mwanamke aliyekuwa
amemshika bundi mkononi. Huku Ropa, bundi alikuwa ishara ya busara. Katika Uk.33
tunaelezwa,
Nilisimama mbele ya mwanamke aliyekuwa amemshika bundi mkononi. Nilisita. Songa
mbele! Nilisukumwa lakini mara hii nilisimama nikawa nachezacheza kama mtu
anayesukumwa aingie majini lakini hataki. Yule ndege simpendi! Mwanamke aliyekuwa
amemshika aliniangalia kisha akavuta tabasamu kubwa. Huyu ndege ni ishara ya busara
huku Ropa! Niliambiwa na mwenzangu. Ishara ya busara? nilisema kwa sauti.
(Wamitila, 2002, Uk 33)
Kulikuwa na watu wa rangi tofauti hata weupe mahali hapo kuonyesha kuwa na
mchanganyiko wa watu wa asili tofauti. Huenda ikawa ni Ufaransa. Jengo kuu lilikuwa
limeinama baada ya kupigwa na mizinga na watu wa kutoka nje yaani, P.P wakati wa vita vya
Fyura kwa nia ya kukomesha tabia zilizochochewa na kiumbe wa Wotan (mfalme wa mashujaa
wafu na mganga). Fyura likiwa jina la msanii mwanamke hadithi yake imechezwa hata katika
filamu iliyojulikana kama Agarest Generations of War, ambaye aliwapoteza wazazi wake na
kijiji chake kwa mahasidi wenye nguvu kwa jina Gridamas. Anaapa kulipiza kisasi dhidi ya
mahasidi hawa wenye nguvu katika vita vilivyoitwa vita vya fyura ila alishindwa. Waton naye ni
mhusika mwanamke katika maigizo ya DC Comics ambaye alinajisiwa na mtu aliyedai kuwa
mtumishi wa mungu jambo lililomsukuma Wotan kujifunza mambo ya uchawi na kuishia
kuabudiwa kama mungu wa uchawi mwenye uwezo na nguvu nyingi ajabu zakuweza kujibadili
kutoka mwili mmoja hadi mwingine hata kuwa mwanamume.
Kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo mwandishi hapa analinganisha vita vilivyokuwa
vimetokea hapo zamani katika mataifa ya ulaya kama michezo ya kuigiza au matokeo ya mizaha
iliyovuka mipaka na kuleta maafa na uharibifu wa mali. Anaongozwa na wenyeji wa hapa.
Wanakumbana na watu waliokuwa wakiujenga upya ukuta uliokuwa umebolewa hapo majuzi
lakini wajenzi hawa hawakutaka kuukubali uhalisia huo. Kwa Mujibu wa nadharia ya
umuundoleo fasiri tunayoweza kuipata hapa ni kuwa hata mataifa haya ya ughaibuni pia huwa na
8

MBURU C. KIARIE

matatizo wakiyoyapitia kama vita miongoni wao iliyopelekea uharibifu mkubwa wa mali. Kwa
hivyo, Mkombozi alifaa afahamu kuwa wadhalimu wao bali na uwezo walionao wao pia
wanamatatizo japo huku nje wanaonekana kama hawana.
Wanakumbana na kikundi alimokuwa kijana aliyekuwa amefuzu masomo yake ya digrii
akiwa amebebwa katika kigari kilichofanana na kile kitumiwacho kuuzia bidhaa madukani huku
wakimshangilia. Kikundi cha pili ni cha mzee na vijana wengi walionyolewa denge na kujipaka
rangi nyingi kichwani huku wamebeba vibendera vidogo wakiimba wimbo nia yao ikiwa
kufukua makaburi ya Wayahudi kwa sababu ya kuwa wabaguzi wa rangi. Kundi hili liliitwa
Gastarbeiter. Yaani, wafanyikazi wakutoka nje ya Ugerumani kutoka nchi za Uturuki, Urusi, na
Uzeshi. Yadaiwa walikuwa wameumwa na jinamizi la Wotan. Yaani walikuwa ni wakimbizi
waliokuwa wametoroka dhiki za maisha ya kwao wakija huku kutafuta usalama na riziki.
Kikundi cha tatu kilikuwa kimebeba vitabu nyuma yao pakiwa jamaa aliyevalia joho jeupe kwa
jina Dr. Joseph Mengele (Daktari Wa Kifo). Katika historia ya Ujerumani, huyu alikuwa afisa wa
Kijerumani wa kikundi cha Schtzstaffel (SS) na Daktari katika Auschiwitz Concetration camp
wakati wa vita vya pili vya dunia. Josef Mengele alichunguza watu ambao hawana mbegu
ifaayo kisha kupendekeza njia ya kuwaangamiza. Nia yake ikiwa kuunda jamii yenye sifa nzuri,
akili stadi, macho ya rangi ya samawi, waliokamilika na shupavu. Waliamini wataumiliki
ulimwengu wakimshinda P.P.
Fasili ambayo tunaweza kuipata hapa tukingozwa na nadharia ni kuwa hata mataifa yenye
uwezo mkubwa wa kiuchumi na kisiasa vilevile katika historia yao yalikuwa na matatizo ya
kijamii kama uwepo wa wakimbizi, ubaguzi wa rangi, ukosefu wa kazi na uhasama baina ya
watu wa asili tofauti kama ilivyokuwa kati ya Wajerumani na Wayahudi. Kwa hivyo ilikuwa
muhimu kwa mkombozi kuifahamu historia ya jamii za Bara Uropa kuhusiana na vita, ubaguzi
katika misingi ya kikabila, ukatili wa kivita na ukosefu wa utu wa wanasayansi wenye mawazo
potovu na misukumo ya kuuongoza ulimwengu. Mkombozi anapata fursa ya kuutambua unafiki
wa mataifa haya kwani wao wakija Afrika hujifanya wangwana na wacha Mungu ilhali hata
makanisa kwao yalikuwa yamegeuzwa na kuwa mahoteli kwa ukosefu wa waumini. Watu huku
walikuwa wametekwa na mambo ya kisasa na hawaa za ulimwengu kwani wengi wanapatikana
katika Macdonalds hasa vijana na katika vyumba vya sinema. Hanna anamuashiria waondoke na
9

MBURU C. KIARIE

safari hii inaishia pale msafiri anapoamua kujipumzisha chini ya mti mkubwa uliokuwa na
kivuli.
6. Safari ya Bustani ya Amani
Safari inapatikana katika Uk. 42-48. Msafiri anazinduka usingizini na anakumbana na wale
watu watatu: Mhubiri, Mwanafalsafa na Mwanasayansi ambao wanatokea na kutoweka. Safari
inayoanzishwa na Hanna na viumbe wengine inaanzishwa kwa sala na Mhubiri. Wanaandamana
wote na kutokezea eneo la walemavu wa miguu na mikono huku watoto wakiwa wamebambuka
ngozi. Maelezo yanatolewa kuwa:
Nilifuata ujia mwembamba hadi nilipotokeza kwenye sehemu iliyokuwa na watu
waliolemaa mikono na miguu. Palikuwa na watoto wengi waliokuwa na alama alama
kama walimwagiwa kitu fulani kilichowabambua ngozi. Watoto hawa walikuwa
wamemzunguka mzee aliyekuwa akiwasimulia hadithi fulani. Niliwaacha na kushika ujia
uliokuwa huko nyuma na mara hii kujiwa hata na nguvu za kukimbia. (Wamitila, 2002,
Uk. 46)
Hapa palijulikana kama Bustani ya Amani. Kulitapakaa karatasi zilizokuwa na ujumbe
uliohimiza uzalendo wa Mwainu. Janga lililokuwa limekumba eneo hili ni matokeo ya vitendo
vya P.P kutupa bomu lililowaua na kuwadhuru pakubwa waliobaki kiasi cha wao kuzaa vilema.
Nadharia ya umuundoleo hapa inatuongoza kuangalia yaliyotukia kule Japan wakati wa vita vya
pili vya dunia. Japan iliposhambuliwa na majeshi ya Marekani

kwa makombora hatari

yaliyoacha maafa na vifo vya wengi.


7. Safari ya Mji wa Ajabu
Safari hii yatokea kuanzia Uk. 48-51. Msafiri alijikuta bila wa kumwelekeza na akashika njia
iliyopita msitu uliokuwa na giza ajabu. Alitokezea katika mji wa ajabu. Kulikuwa na mataa ya
ajabu kila sehemu hungejua iwapo ni mchana au usiku. Alitembea kulikokuwa na jengo kubwa la
kioo. Jengo lililokuwa la utafiti wa teknolojia. Anatembezwa jengoni na Hiro na kuonyeshwa
jengo lililojaa mashine na mitambo tofauti na watafiti wengi. Kusudi likiwa wasiwachwe nyuma
na P.P. Alifika bandarini mlimokuwa na kiwanda cha magari (reconditioned) alipoelezwa kuwa
wenyeji hawakutumia magari yaliyotumiwa bali waliyaandaa na kuyauza nje. Alielezwa kuwa
mataifa yanayouziwa yakigomea bidhaa zao, nao husitisha misaada ya kiuchumi kwayo. Mataifa
10

MBURU C. KIARIE

haya yanayouziwa haya magari vilevile hayakuwa na idhini ya kuvua samaki kama
inavyoelezwa:
Wanao (samaki) lakini hawana idhini ya kuwavua, sisi tunayo. Wanapatikana kwenye
maji ya kimataifa, International Waters. Tunawavua na kuwapakia kwenye makopo.
Kwao ndiyo maendeleo hayo! Wakiyagomea nasi misaada ya kiuchumi kwao tunaizuia
(Wamitila, 2002, Uk. 50)
Alielezwa kuwa wengine pia kama vile akina Churchill, ukoo wa Kaiser, Franco na P.P pia
walifanya hivi. Fasili hapa kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo ni kuwa Mkombozi anapata
ufahamu wa chanzo cha matatizo mengi ya kiuchumi katika jamii yake. Kuwa yalisababishwa na
urundikaji wa visivyohitajika na kutumika katika mataifa yaliyoendelea kiteknolojia na kiuchumi
katika mataifa ya Afrika kwa kuwekewa vikwazo na masharti ya kibiashara. Safari yake inakoma
alipozama majini na kupoteza fahamu. Aliamini alimezwa na samaki kama Yona. Tunaelezwa:
Lakini kuyafupisha maelezo, nilitumbukia kwenye mafunjo yaliyokuwa huko na kabla
sijajua nilikokuwa nilizama majini. Sijui ilivyokuwa baada ya hayo. Inaelekea nilimezwa
na samaki kama Yona; mimi na kibuyu changu pamoja na hata mkongojo wangu.
(Wamitila, 2002, Uk. 51)
8. Safari ya kumwelewa P.P
Safari ipo Uk. 52-57, Msafiri anazindukana baada ya alichodhani ni kutemwa na samaki.
Mikono yake ilikuwa imepauka rangi. Huku jua lilichomoza sehemu ya kusini. Aliongozwa na
wale viumbe wa ajabu. Mara anatokewa na wale watatu (Mhubiri, mwanasayansi na
Mwanafalsafa). Wakatembea siku, miezi au hata miaka. Mhubiri akashika njia yake naye Msafiri
akafuatana na Mwanafalsafa na Mwanasayansi. Wanampatia sifa za P.P, kuwa alikuwa:
Anapenda kuchezacheza sana na hata kuharibu majengo, ana kiburi na ni Msemaji
uongosisi hatuchezei hivyo, anamwogopa Stalin lakini anatutusitusi kila
wakati..Ehh, tunasikia kuwa anashindwa hata kuijua adabu ya kutumia lugha.
Anapenda kujisifusifu na kujipiga kifua. Baadhi wanasema ni(Wamitila, 2002, Uk. 55)
Safari yake inamfikisha katika jengo la Macdonald baada ya wale wawili kwenda zao.
Wenyeji wanamwongoza sehemu mbalimbali za nchi hii yao kuanzia mashambani kulikokuwa
na mashamba makubwa yaliyolimwa viazi na wote kwa ushirika mkubwa. Alifahamishwa kuwa
ushirikiano huo ulikuwa matokeo ya mapinduzi. Wenyeji wanazungumzia matatizo yao ya rubo
11

MBURU C. KIARIE

yaliyotatiza usafirishaji wa bidhaa zao. Matatizo haya walidai yalisababishwa na P.P. Daima
alikunywa kinywaji kutoka kibuyu chake ambacho hakikwisha kilichokuwamo. Fasili inayoweza
kutolewa kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo ni kuwa Mkombozi alitakiwa aone jinsi
ushirikiano baina ya watu waliounganika kwa nia moja unavyoweza kuzaa matunda ya ufanisi.
Kwa hivyo lazima ahimize umoja na ushirikiano katika jamii yake. Kibuyu alichopewa
kisichoisha kinywaji kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo, ni imani na matumaini ambayo
Mkombozi anahitaji awe nayo iliaweze kufanikiwa kwani akikosa haya mawili hataweza
kuletela ukombozi.
9. Safari ya mawazoni
Safari hii iliyo katika Uk. 58-62, tutaiita ya mawazo kwani Msafiri anarudisha nyuma
mawazo yake katika maisha yake ya utotoni kuanzia kuzaliwa kwake. Anasema:
Sehemu iliyokuwa imefutika katika akili yangu siku nyingi ilianza kunikunjukia
nilipokuwa huko. Nilianza kuyakumbuka matukio ya utotoni. Niliikumbuka hadithi ya
babu kuhusu kuzaliwa kwangu (Wamitila, 2002, Uk. 58)
Anatoa maelezo ya namna nyanyake alimchukulia kama jagina wa kijiji aliyekuwa amerudi
kwani alizaliwa akiwa amelifunga jicho moja kama jagina aliyekuwa ameaga hapo mbele akiwa
amefunga jicho moja baada ya kupigwa na radi. Yeye alichukuliwa kuwa jagina wa pili.
Alifanyiwa miviga ili kumpoza maumivu ya kichwa ambayo aliambiwa yalisababishwa na radi.
Yaani, yalikuwa maumivu ya radi. Ilibidi afanyiwe mviga wa kukikashifu na kukibeza kile
kitendo kilichomwua jagina wa kwanza aliyeuawa na radi hivyo basi akatiwa kwenye chumba
kilichotiwa moto na kisha kutolewa na yale maumivu yakamtoka na jicho kufunguka. Fasiri
kulingana na nadharia ya umuundoleo ni kuwa, Mkombozi yeyote yule aelewe kuwa kiongozi
huzaliwa na uongozi. Kuwa shughuli za kumtawaza kuwa kiongozi ni jambo ambalo jamii huwa
haina budi kwani maisha yake ya ukombozi kulingana na mwandishi huwa ni majariwa na
yanayomkumba huwa hana hiari bali kuyakubali. Yaelekea kuwa katika jamii nyingi za kiafrika
majagina wa kwanza yaani wakombozi wakwanza walikuwa wameaga hasa baada ya kupigania
ukombozi wa mataifa yao kutoka kwa mkoloni. Sasa ukombozi wa pili unahitajika na mkombozi
wa pili anawakilishwa na mhusika Msafiri.

12

MBURU C. KIARIE

10. Safari katika ndoto


Safari hii inafanyika katika Uk. 63-65. Inaanza Msafiri alipokanyaga kitu kitelezi na
kumfanya kuteleza kwa kasi ya ajabu na kujiwa na ndoto. Ndotoni anakumbana na lile jitu refu
ajabu tena. Msafiri anaelezwa kuwa:
Nilisikia sauti nzito ambayo siwezi kusema ilikotokea. Niliyatupa macho yangu mbele
(katika ndoto hiyo maana kwa kweli nilikuwa nimeyafunga) lakini sikuona kitu wala
mtu. Niliyaelekeza kushoto lakini hata huko yalikosa kuambulia chochote. Niliyainua
juu. Hatimaye yalinata juu ya jitu refu lililokuwa na miguu myembamba ajabu; labda
likisukumwa tu lingeanguka. Hili lilikuwa pande la jitu. Nilishindwa kuiona ilikokomea
ile miguu ya kiumbe huyo wa [Link] niliweza kuziona pia zake za miguu
zilizokuwa kubwa kama masahani. (Wamitila, 2002, Uk. 63)
Jitu hili linamfahamisha kuwa linamiliki maisha yake, lina uwezo wa kumchezea
linavyotaka, linadai kuwa lilikuwa chanzo cha furaha ya kijiji, elimu, vyakula, ujuzi, raha zote na
ndoto pia, kuwa lilikuwa kama hydra, lina vichwa vingi na lina uwezo wa kufa na kufufuka.
Mara akasikia sauti za watu waliokuwa na furaha na vigelegele. Kisha akasikia sauti ya
asiyeonekana kutoka juu ikizungumzia kubadilika kwa mambo kwani mishahara ilikuwa
midogo, uchumi ulikuwa umezorota, ubinafsi ulikuwa umezidi katika awamu mpya ya world
economy. Zile kelele za furaha zikabadilika na kuwa za maombolezo na kilio cha huzuni.
Anawaona watu wakielekea mashambani na majembe. Sauti inamfahamisha kuwa wale watu
wataishi kubaki nyuma kwa muda mwingine akisema (mnenaji asiyeonekana) hayawezi maisha
kama hayo.
Kulingana na nadharia ya umuundoleo Jitu hapa linawakilisha nchi ya Marekani ambayo
inatawala dunia na tawala za mataifa madogo kama ya Afrika duniani. Taifa hili lenye uwezo
inalinganishwa na Hydra aliyekuwa nyoka mkubwa ajabu wa majini kule Ugiriki na katika
visakale vya Warumi. Joka hili lililokuwa na vichwa vingi ambavyo iwapo kichwa chake kimoja
kingekatwa kingine au vingine vingi vilimea. Damu, hewa aliyoipumua nje na harufu yake
zilikuwa [Link], sera na vitendo vya mataifa haya wenye uwezo vilikuwa somu na hatari
kwa mataifa madogo. Marekani huathiri uchumi, siasa, elimu, afya na shughuli zote za maisha ya
wananchi wa mataifa haya. Uchumi wa nchi hizi changa hutawaliwa na mataifa kama Marekani
kupitia mifumo ya kiuchumi kama soko huru. Soko ambazo huhimiza uhuru wa mataifa kama
Marekani huku nchi zisizo na uwezo zikifuata masharti yao kuzinufaisha. Jamii za nchi hizi
13

MBURU C. KIARIE

changa zilikuwa na uhitaji mkubwa wa mkombozi atayewaokoa kutoka kwa jitu hili Marekani na
washirika wake. Ndiposa msafiri anaeleza kuwa maono yake yalikatizwa na mwanguko mkubwa
juu ya ardhi tifutifu. Kisha:
Palikuwa na watu waliosimama hapa na pale. Wawili watatu walikuwa wamepiga magoti
wakisali. Yaelekea hawa ndio niliokuwa nikiwaona katika maono yangu. Nilitingisha
kichwa na kuwaangalia kisha nikasikia wote wakisema kwa sauti ya juu Mkombozi
amekuja! Mkombozi amekuja! Je, umekuwa wapi wakati wote huu? Mkombozi
amekuja, niliyapitisha yale maneno yao akilini. Nilitamani kuwaambia kuwa nilikuwa
nimepotea njia(Wamitila,2002. Uk. 65-66)
11. Safari kama Mkombozi
Safari inafanyika kati ya Uk. 67 na 75. Msafiri alikaa na kupumzika na wenyeji wake kwa
muda mrefu si miezi au miaka. Alipewa kijana wa kumwongoza. Alitembezwa palipokuwa
nyumba hamsini ushei ambazo zilikuwa zimeinamiwa na miti ya matunda. Alielezwa kuwa:
Kila kiongozi anakaa huko juu paani, huko ndiko anakochumia matunda kwa urahisi na
kuwapatia watu walioko chini ambao ndio waliomshikia ngazi ya kupanda juu. Lakini
kuna wengine ambao wanachofanya ni kula wakashiba kwanza kisha kuyatupa makaka,
makokwa na maganda huko chini yanakonganganiwa na umati mkubwa ulioko huko.
Wengine wanaiba na kuhamishia kwingine, labda ughaibuni. (Wamitila, 2002, Uk. 67)
Katika nyumba ya kwanza kiongozi ameketi huku bendera ikipepea. Tabia hii ikiwa
ilianzishwa na babu yao Osagyefo (mkombozi) ambaye ndoto yake ilikuwa kuunganisha miji
yote lakini alipuuzwa na wengi. Viongozi waliokuwa juu ya nyumba, walikuwa wanaume.
Yaelezwa kuwa viongozi wengine waliiba yale matunda na kuyauza ngambo. Wengi walikuwa
na vivimbe vipajani baada ya kupigwa mawe kwa manati na P.P. Yaelezwa kuwa wananchi ni
waoga na wanatiwa woga zaidi na askari na jeshi la utawala. Msafiri walishuhudia nyumba moja
iliyofuka moshi huku kukiwa na fujo kila mtu akikimbia njia zake na wengine wakijaribu
kukwea paani alipokuwa ameninginia mlingotini kiongozi kama tumbiri au ngedere. Watu
walitorokea katika nyumba jirani wakilalamikia upofu wa viongozi.
Kama nadharia ya umuundoleo inavyotuongoza, tunaweza kusema kuwa, mwandishi hapa
anatupatia picha na hali ilivyo katika Bara Afrika hasa baada ya mataifa mengi kujinyakulia
uhuru. Mataifa haya yakawa yanatawaliwa na viongozi waafrika weusi ambao badala ya kukuza
nchi zao kwa kuziletea maendeleo na manufaa kwa wote, wao walitumia wadhifa na raslimali za
nchi yao kujitajirisha wao na marafiki zao. Hata kuficha raslimali walizoiba katika mataifa ya nje
14

MBURU C. KIARIE

huko ughaibuni. Wengi wameathiriwa na vikwazo wanavyowekewa na mataifa yenye uwezo


kama vile Marekani. Kiongozi kama Kwame Nkrumah wa Ghana aliyerejelewa kama Osagyefo
au mkombozi alikuwa na ndoto ya kuunda muungano mmoja wa nchi za Afrika lakini
akapuuzwa. Alihisi kuwa mataifa yote ya Afrika yalikuwa na matatizo sawa na maadui sawa na
iwapo wangeungana wangekuwa na nguvu dhidi ya matatizo yaliyowakumba na maadui wa
maendeleo wa kutoka mataifa yeyenye uwezo ya ughaibuni. Yaani, nia yake ilikuwa kuzikomboa
nchi za Afrika kwani viongozi waliokuwapo walikuwa wameshindwa kuongoza na kutatua
matatizo yanayokumba raia wa nchi zao. Hali hii ilikuwa mbaya kiasi cha baadhi ya wananchi
kuanza kupinga tawala zao na hata ghasia kuzuka hali inayowafanya wananchi kuwa wakimbizi
katika mataifa jirani. Suala la ukoloni mamboleo linadhihirika pale viongozi wanaonekana kuwa
na vivimbe usoni. Yaani, viongozi hawa walikuwa wamelazimishwa kutenda kama walivyotaka
watawala wa mataifa wenye uwezo. Walilazimika kuyaruhusu maaifa haya yenye uwezo kutumia
raslimali za nchi zao kwa manufaa yao huku wananchi wakibaki kuadhirika kutokana na vitendo
na maamuzi wa viongozi wao. Hii ni kwa sababu wananchi hawakufikiwa na huduma za
kimsingi kama chakula na afya bora. Viongozi wamejitenga na wananchi waliowachagua na
kuishi mbali na wao jambo linalodhihirisha kugawika kwa jamii katika misingi ya watawala na
watawaliwa.
12. Safari ya Kisiwani
Hii inafanyika kutoka Uk. 76-83. Msafiri anaamua kuendelea na safari japo sasa hakuwa na
waliyeandamana naye. Anaeleza kuwa:
Badala ya kuifuata njia niliyokuwa nimependekezewa na yule kijana, nilishika njia
tofauti iliyoishia baharini. Kwa bahati nzuri mara hii kulikuwa na vyombo vya kusafiria.
Ilipasa kila mtu kutoa pesa kulipia usafiri huo. Sikuwa na pesa za kulipia nauli lakini
waliohusika waliamua kukitwaa kitabu changu kimoja (miongoni mwa nilivyopewa huko
nyuma) kama fidia ya nauli. (Wamitila, 2002, Uk. 76)
Kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo Mkombozi lazime aweze kutoa uamuzi wake
mwenyewe wa namna anavyofikiria kufanikisha juhudi zake. Hivyo basi wakati mwingine si
lazima afuate maelekezo anayopewa bali anaweza kuamua mambo tofauti kutegemea hekima
yake. Mwandishi anaonyesha kuwa ili kupiga hatua katika harakati za ukombozi kulihitajika
matumizi ya fedha na zilipokosa ilibidi kuchukua hifadhi za raslimali zilizopo ili kuweza kupiga
15

MBURU C. KIARIE

hatoa. Masharti yaliyowekwa na mataifa yalioendelea kwa nchi zinzoendelea ni kuwa lazima
zitoe sehemu ya hifadhi au raslimali zake kwa mataifa hayo ili kupata maendeleo kutoka huko.
Safari inakatizwa na ilibidi wapige kambi katika kisiwa kilichokuwa chembamba kutokana
na hali mbaya ya mawimbi ya bahari. Alikuwa bado na azima ya kuvuka upande wa pili wa
bahari na mara sauti ilimjia kama ya ndotoni na mara alipokuwa amesimama pakateguka na
akatumbukia majini. Alielea majini na kufika ukingo wa bahari. Baharini aliliona gogo ambalo
liliandamana naye. Kisha alipozindukana baada ya kupumzika pale ufukweni aliliona lile gogo
kando yake. Gogo lilibadilisha sura, mara ya nyanyake na mara ya marehemu mkewe Hanna.
Hali hii ilimfanya kudhania pengine ameingiwa na kichaa. Aliweza kujipumzisha na kusoma
vitabu na alivutiwa na kile kilichokuwa na hadithi ya Che. Hadithi iliyokuwa ya ukombozi na
ufahamu. Ilimhusu daktari aliyeacha kazi ili kupambana na Yanguis kupata ukombozi wa nchi.
Yanguis alikuwa nguvu kuu ulimwenguni. Yaani, kitabu kilihusu Muajentina Che Guevara,
aliyekuwa daktari aliyetembea Marekani Kusini na kukuza hisia za uasi na hamu ya
kuwakomboa wenyeji walikuwa wamezongwa na umaskini mkubwa, njaa na magonjwa. Ilibidi
akabiliane na utawala uliokuwa na nguvu kuu wa Marekani. Juhudi zake za kuwahamasisha
watu kuasi na kujikomboa zilisababisha kuwindwa na hatimaye kuuwawa kwake. Kulingana na
nadharia inayoongoza utafiti huu, Mkombozi anapatiwa picha ya anavyofaa kuwa kama
mkombozi kupitia hadithi ya Che. Kuwa kiongozi yeyote wa ukombozi lazima ajitolee kwa hali,
mali na hata kwa maisha yake kuikomboa jamii yake.
Msafiri aliendele na safari kupitia msitu ulioshikamana ajabu huku akifuatwa na mtu
asiyeonekana aliyekohoa na kupiga chafya. Mara akawaona watu walioimbaimba wakiwa
wameshika vimuli. Safari inachukua mkondo mwingine uliosababisha mwisho wa safari hii pale
Msafiri anaeleza kuwa:
Nilisonga mbele na kuangukiwa na kitu kilichokuwa joto joto kama kinyesi cha ndege.
Mara hii miliamua kuinua kichwa changu juu. Katika jitihada za kufanya hivyo
nilikifungua kinywa changu na kuangukiwa na rundo fulani ambalo nililitema nje haraka.
Unyanya fulani uliniingia nikaza kukohoa na kujitahidi kutapika hatimaye nilianza
kutapika, nikatapika, nikatapika wee.e..e mpaka nikaanza kuona kisuunzi. Miti
ilionekana kwenda huku na huku, kuanza kupinda pinda, kuanzaaa. Nilianguka.
(Wamitila, 2002, Uk.83)
13. Safari katika nchi ya magofu
16

MBURU C. KIARIE

Safari hii ipo katika kurasa za 84-90. Alipozindukana na kuanza safari na kutokea mahala
palipokuwa na magofu makubwa kama anavyoeleza:
Baada ya muda nilitokeza mahali palipokuwa na magofu makubwa. Ilivyoelekea
palikuwa na majengo makubwa zamani, labda ya kifalme. Nilitembea polepole bila ya
kutaka kuingia ukingo fulani..(Wamitila, 2002, Uk. 85)
Anamkuta mzee ambaye alikuwa juu ya jabali. Alimfahamisha namna watu walivyopuuza
agizo lake la kuharibu kila kitu na kuwaonya kutoshirikiana na mtu bila ya kujua nia yake
wakakataa. Alidai historia ina hukumu kali. Alikuwa amewakanya kuhusu biashara aliyoidai
kuwa ilikuwa ya Ali Baba na Wezi Arubaini ya kuwanadi watu. Lakini wakampuuza na hata
kuingilia kula Hamburger na kunywa Coke huku wakitazama mipira ya NBA katika televisheni.
Alidai historia itawahukumu kama itakavyomhukumu P.P. Mzee alizidi kueleza kuwa magofu
yalikuwa ya kituo cha usomi kilichoamrishwa kifungwe na mtu aliyejulikana kama Bina-Adamu
kwani hawakutaka kiendelee na utafiti wake wa kuifunua Historia kwa kila mtu kwa vile historia
waliiogopa. Kituo kilifungwa kwa kudaiwa kuwa malengo yake yalikuwa mabaya. Baadaye
hospitali ikaanzishwa na kisha kufungwa baada ya dawa kuuzwa na wanasiasa wapate pesa za
kufanya biashara. Mzee akalalamikia ujio wa Global Village iliyoletea kila mtu matatizo
ulimwenguni na uharibifu wa sayansi aliouita global pillage. Kituo kilipofungwa ulianza Wimbo
wa Mefu ulioeleza kuhusu kushushwa kwa thamani ya hela, ugavi wa hela ubanwe, matumizi ya
hela yakatwe, soko la hela lifanywe huru, na mishahara duni ipunguzwe.
Kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo, mwandishi anamfikisha Mkombozi Marekani
palipo na makao makuu ya Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF-International Monitary Fund)
alipopata ufahamu wa uwepo wa utandawazi na athari zake katika mataifa machanga katika
sekta ya kiuchumi. Mambo ambayo anaeleza kuwa yaliongozwa na shirika hili analolilejelea
kama Mefu. Anaeleza jinsi mataifa yenye uwezo wa kiuchumi yanavyokandamiza mataifa kwa
kuongoza soko ya sarafu za nchi ulimwenguni na thamani ya hela ilikuimarisha chumi zao huku
za nchi changa zilizorota. Analalamikia kuundwa kwa mifumo kama Global village ambayo
ilipatia nchi zenye uwezo kuimarisha dhuluma zao katika mataifa madogo ili kujinufaisha bila
kunufaisha mataifa hayo. Analalamikia harakati za kisayansi anazoziita Global Pillage, kwani
badala ya kuimarisha maisha zimeyaathiri maisha ya watu vibaya kwa madhara ya matokeo
yake.
17

MBURU C. KIARIE

Msafiri aendeleapo na safari yake kando ya bahari anakuta kundi lilokuwa likilia kuwa
mafuta yamemwagwa baharini ili kufisha samaki sehemu ya ukingo wa bahari na kuwafanya
wenyeji kutegemea makopo ya samaki wanaovuliwa katika maji ya kimataifa. Kwa mujibu wa
nadharia ya umuundoleo, mwandishi anamrejesha Mkombozi Afrika na kumwonyesha namna
mataifa yaliyoendelea yanavyosababisha kuporomoka kwa chumi za mataifa yanayoendelea ili
kuyashurutisha kuyategemea iwapo yanataka kuendelea. Walilalamikia ukosefu wa ushirikiano
wa zile nyumba hamsini ushei yaani mataifa ya Afrika, kama chanzo cha matatizo yao kwa
sababu ya ubinafsi na pingu za wadhamini ambao waliwaona kuwa waharibifu wakuu. Yaani,
mataifa ya Afrika yanakosa kuelewana na kuunda ushirika kwa vile kila nchi ina wadhamini
ambao wanaendeleza ukoloni mamboleo na ambao matakwa yao yanakinzana na yanaendeleza
utengano wa mataifa haya badala ya kuyaleta pamoja.
14. Safari ya kukutana na Mzee- Kiongozi wa kijiji
Safari hii ipo katika Uk.91-104. Msafiri anakutana na kikundi cha watu waliokuwa
wanalalamikia kubaguliwa na ndugu yao kwa sababu ya rangi, kubakwa kwa Mamanchi. Kuwa
ndugu yao anakula matunda peke yake na wenzake wachache ambao wanaiba mbegu pamoja.
Mbegu ambazo wangepanda ili wapate matunda mengi yawafaidi wote. Walidai kuwa, walikuwa
wakirudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kiongozi wao hakujali hata maslahi ya watoto na
waliokuwa chini ya mti wa matunda. Yeye alibaki kuninginia mlingotini kama kima. Walidai
kuwa nyumba ilikuwa imejaa moshi na watu wameanza kuvutana. Kulingana na nadharia ya
umuundoleo, mwandishi anaagazia suala la ufisadi na namna linavyoendelezwa na watawala
wafisadi wa nchi changa za Kiafrika. Viongozi ambao wanazirudisha nchi zao kimaendeleo
kutokana na vitendo vya vya kifisadi vya kujali maslahi yao na ya marafiki zao tu. Msafiri
aliongozwa na kijana mwenye kubeba manati na katika Uk. 91. tunaelezwa kuwa;
Kadiri tulivyopita nyumba ndogo ndogo (niliambiwa ni nyingi) kuelekea palipokuwa na
nyumba kuu ndivyo sauti za uchungu zilivyoongezeka. Sehemu za nje nje hazikuwa na
miti yoyote ya matunda. Niliona migomba ya ndizi hapa na pale ila kulikuwa na mimea
mwitu kadha.(Wamitila, 2002, Uk. 91)
Walifikia nyumba kuu, iliyokuwa na kitambara kilichopepea kwenye mlingoti uliokuwa juu
yake. Mitunda ya miembe ilikuwa imezingirwa na miiba kuwakataza watu wasiukaribie labda.
Palikuwa pande la mtu lililosimama huko ili kuzuia watu wasiukwee mwembe. Kando kulikuwa
18

MBURU C. KIARIE

na watu waliokuwa wakiimba tenzi kumsifu aliyekuwa juu ya nyumba. Kiongozi alionekana
akila embe na kujichafua. Kiongozi huyu alikuwa na uvimbe juu ya jicho la kushoto na
walimwita Musa wa Leo na alikuwa na ulinzi mkali sana. Yaelezwa kuwa, P.P alikuwa
mjombake Yanguis; aliyekuwa mlingotini. P.P alikuwa wa msaada sana kwao hadi kuwapa
bunduki. Wema na ukarimu wake waliufananisha na ule wa Fyuraha, Hiro na Churchill na
kusifia wingi wa makampuni yake yaliyozuka kila mahali. Walimuenzi.
Kwa mujibu wa nadharia ya Umuundoleo, mwandishi anamwelekeza Mkombozi katika
mataifa mbalimbali ya Afrika. Mkombozi alijionea namna viongozi wa nchi hizi waliotawala
baada ya mataifa yao kupata uhuru. Anaonyeshwa jinsi walivyotamausha matumaini ya
wananchi waliowachagua ya kupata utawala na maisha bora. Mataifa yalioendelea yalihadaa
mataifa ya Afrika kuwa yanayasaidia kwa misaada ya zana za vita kumbe nia ni kutengeneza
soko la zana hizi kwa kuhimiza uhasama baina ya mataifa na kilinda tawala hizi dhalimu.
Waliweza kuzipatia tawala hizi uwezo wa kujisetili uongozini kwani ziliwaogofia raia na
wapinzani wao kwa silaha hizi.
Walielekea kwa kina kijana aliyemwelekeza aliposhuhudia umaskini na utu. Bali na kuwa
wakarimu hawakuwa na karo, chakula cha kutosha, ukosefu wa kazi, ukosefu wa dawa
hospitalini, ukosefu wa usalama mambo yaliyosababishwa na viongozi waliowamini kumbe
mambo yaligeuka kuwa kinyume. Alifahamishwa kuhusu kiongozi aliyefungua operesheni Ozoni
leya badala ya kuifunga. Akaelezwa pia kuhusu waziri aliyejenga nyumba yake kilimani juu
karibu na kanisa, ili aonje jua kabla halijachafuliwa na wengine na alitaka kuwa karibu na
Mungu. Hata wakipitia haya yote wenyeji wake walikuwa wakarimu na walikuwa na furaha.
Kwa mujibu wa nadharia inayoongoza utafiti huu, Mkombozi anaelezwa kuhusu viongozi wa
mataifa ya Afrika wakiwakilishwa na waziri walikuwa watu walijitia waliojali maslahi ya
wananchi masikini kabla hayajachaguliwa. Lakini baada ya kuchaguliwa walijikweza na
kujitenga na wananchi. Wakawa wanashughulikia maslahi yao wenyewe na kuwasahau wananchi
masikini waliowachagua. Vilevile, anaeleza kuhusu ukosefu wa ufahamu wa mambo
yanayoeledela ulimwenguni yakiwakilishwa na suala la Ozoni Leya. Yaani, viongozi wengi
waliochaguliwa hawakuwa na hekima na ufahamu wa jinsi siasa na mambo ya ulimwengu
yalivyokuwa yakiendelea.
19

MBURU C. KIARIE

15. Safari ya mkondo wa mwisho.


Msafiri aliamshwa na Hanna kutoka usingizini. Wanaanza safari inayotukia kuanzia Uk. 105115. Alipelekwa mahali kando ya bahari palipokuwa juu na waliweza kujionea sehemu ya chini
iliyojaa watu. Wazungu waliokuwa wakijiburudisha na wasichana weusi. Wengi wa wasichana
hawa wakiwa wamevaa nguo pwaya. Kulingana na nadharia ya utafiti, Mkombozi anaelekezwa
sehemu za biashara ya utalii ili ufahamu namna watalii kutoka ughaibuni walivyokuwa
wakiuporomosha utamaduni wa wenyeji kwa kuwaharibu wasichana wao. Mbele kidogo
tunaelezwa:
Baada ya wakati alinieleza kuwa tulitakiwa kuanza safari yetu. Huu ndio mkondo wa
mwisho. Jua kama hutafanikiwa kuwapata au kuwajua wale huntha basi hakuna
matumaini. Ikiwa huwapati hakikisha umewajua. Hiyo ni hatua muhimu! Baada ya
kusema hivyo alinishika shingo na kunigeuza kama mtu anayechelea kuangalia upande
fulani. (Wamitila, 2002, Uk. 110)
Huko mbele aliwaona wale viumbe wenye kutoa mwanga na kuwafuata. Aliongozwa na
viumbe akipitishwa kando ya bahari palipokuwa na majumba mengi ya ajabu. Sehemu
iliyojulikana kama Bustani ya Eden makazi ya viongozi. Sehemu iliyoangazwa na mataa ya
umeme na kuonekana kama mchana. Baadaye alifika sehemu ukingoni ambako huko chini
kulikuwa na mto wenye maji mengi ajabu kama Bahari Hindi. Mwenzake akajitosa kule na
kumwonyesha weledi wake wa kuogelea. Kisha, Hanna akajitokeza na kujiunga na aliyekuwa
majini na kumhimiza Msafiri ajitome kule. Akajiachilia na kutelemka kina kile kirefu alichohisi
kana kuwa hakikuwa na mwisho. Alipofika majini alijikuta yuko peke yake. Maji yalikuwa
yametulia ajabu sasa yakaenda kasi ya ajabu akielea majini. Alikumbana na meli iliyokuwa na
maandishi ya AMISTADI 1. Alikumbuka kuwa alifundishwa kuwa ilikuwa meli ya kuwabeba
watumwa. Akajivuta kando ya bahari. Katika Uk.115, jambo linatokea linalohitimisha safari hii,
Niliyatupa macho yangu huko chini tena. Mara hii niliwaona Hanna na yule Mwenzangu
wameiweka mikono yao kwa namna iliyounda kitanda fulani. Nilijua kuwa walikuwa
wakiandaa kunidaka niangukapo. Niliushika imara ule mkoba wangu na kuufumbata
kisawasawa mkongojo wangu. Niliyafunga macho kisha nikajitupa. Nilienda kichwa juu,
miguu chini, kichwa chini, upande upande. (Wamitila. 2002, UK. 115)
Fasili tunayoweza kuitoa hapa tukiongoza na nadharia ya umuundoleo ni kuwa, Mkombozi
alirejeshwa nyuma kwa madhila yaliyowakumba waafrika hata kabla ya ukoloni. Waafrika

20

MBURU C. KIARIE

wanaume wenye nguvu walisombwa na kuuzwa kama mifugo kuwa watumwa huko nchi za
ughaibuni, Marekani kusini. AMISTADI I ikiwakilisha jahazi ya mwisho iliyowabeba watumwa
waliogoma na kuupata uhuru wao uliosababisha kukomeshwa kwa biashara ya watumwa.
16. Safari katika nchi ya X
Safari inafanyika kuanzia Uk. 116-126. Msafiri anakumbana na mwanamume mweusi
aliyekuwa amebeba samaki kutoka uvuvini kwa jina X. X alimkaribisha katika nchi ya leo na
kesho na, kumfahamisha kuwa alikuwa karibu kufika katika Bustani ya Eden ya Pili. Kisha
akatokea sehemu iliyokuwa na jamii ya watu walioishi wakiwa uchi wa mnyama. Wao walikuwa
wanaishi jana kwa kuwa leo yao haina furaha. Maisha yao yalikuwa na ukiwa wa ajabu kutokana
na kosa fulani walilolitenda huko nyuma baada ya mkoba fulani kupotezwa jana yao na kama
ungepatikana maisha yao yangekuwa afadhali. Raha yao ilikuwa katika kuipa mgongo historia
na kwamba walikuwa wanaishi katika ndoto. Kulingana na nadharia ya utafiti huu, Mkombozi
anafikishwa Marekani ambayo ilichukuliwa kuwa Edeni ya Pili na waafrika waliokuwa
wamewashiriwa huru kutoka utumwani. Furaha yao ilikuwa ya muda kwani baada ya muda
walibaguliwa na kuonewa kwa misingi ya rangi yao. Matumaini ya maisha bora na yakuwa huru
yakawa ndoto ambayo bado haijatimia.
Msafiri anakumbana na Mwanasayansi na Mwanafalsafa. Mwanasayansi anakimbia
kwenda zake kumshughulikia Dolly Kondoo aliyekuwa zao la utafiti wa kisayansi na
aliyeonyesha dalili za kuzeeka mapema. Mwanafalsafa anaamua kumpeleka Msafiri alikokuwa
P.P na wanaenda kwa kasi ya ajabu na kwa muda mrefu. Mwanafalsafa alimtolea maelezo
ambayo yalihusu jamii hii iliyoishi wakiwa uchi kuwa ni jangwa (ukosefu wa kitamaduni),
ukweli na usiokuwa ukweli kuwa umeunganika, mipaka ya wema na uovu imefutwa, uwili
ulikuwa umesababishwa na FUJO ASILIA katika historia ulikuwa umetoweka na kutawaliwa na
UMOJA WA FUJO. Jamii hii ilikuwa ya rangi nyeupe yaani, wazungu. Msafiri baadaye anatokea
katika sehemu iliyokuwa na watu weusi kama X, tunaelezwa kuwa;
Ujia huo uliishia kunitokeza kwenye kijiji kilichokuwa na watu wachache, wote weusi
kama X. Palikuwako na watu wanaume wawili wazee kupindukia huko nyuma kulikuwa
na watoto wadogo waliokuwa wakicheza makaburini. Wengine walikuwa wakiichezea
misalaba ya makaburi kadha yaliyokuwako. Sikuwaona wanawake wa kuwakanya
wasifanye hivyo. (Wamitila, 2002, Uk. 123)

21

MBURU C. KIARIE

Wazee wale wawili waliozeeka kupindukia walikuwa wakichorachora mchangani. Yamkini,


walikuwa wakimtarajia. Anafahanishwa kuwa makaburi yale yalikuwa ya watu wengi waliokufa
kutokana na matokeo ya kufanyiwa majaribio ya kisayansi ya kuangalia matokeo ya kaswende
katika miili ya bina-Adamu!. Maelezo haya yaliwaliza wote. Walimfahamisha kuwa waliishi
katika urazini wa kuwili, kujijua kupitia macho ya wengine na kuishi pembezoni hali hii ikiwa ni
tanzia ya rangi yao. Anatumwa kwa P.P kuwa msahau jana kesho humkumbusha na kuwa
hawaishi katika ndoto bali katika uhalisia wenyewe. Kisha, akakabidhiwa kitabu kilichokuwa na
anwani The Souls of Black Folk, na kuagizwa akisome akimaliza safari yake. Kwa mujibu wa
nadharia ya utafiti huu, maana matukio haya nikuwa mkombozi anapatiwa ufahamu maovu
waliyotendewa watumwa walikuwa huru kule Marekani. Uhuru walioupata ulikuwa wa muda
kwani waliteswa chini ya misingi ya ubaguzi wa rangi. Vilevile walidhuliwa zaidi walipotumiwa
kama vijaribio vya kisayansi jambo lililowaletea maafa na matatizo mengi ya kiafya.
17. Safari kuelekea Bustani ya Eden ya Pili
Safari yatukia Uk. 127-135. Msafiri hapa anatokea mbele ya jumba kubwa la kioo kitupu. Hili
lilikuwa jumba la teknolojia ya juu kwani kulikuwa na mitambo kama dubwana ambalo lilikuwa
jibwa mashine. Hili lilikuwa jumba la utafiti. Mfano walitafiti ubongo wa Albert Einstein.
Watafiti hawa wanaishi kidogo katika leo lakini sanasana kesho kutwa. Wanaishi katika uhalisia
wa kisayansi na wamo katika Bustani ya Eden ya Pili. Walikuwa katika harakati ya pili ya
kuuokoa ulimwengu baada ya hali ya kwanza kuharibika. Anafahamishwa kuwa kila ukombozi
ulihitaji shujaa ambaye ni mtu binafsi aliyekombolewa kutokana na pingu za historia, anayeona
raha kuuasi ukale, asiyesumbuliwa na kutiwa uchafu na masuala ya urithi wa familia,
aliyesimama pweke pekee, aliyejitegemea na mwenye msukumo wa kwenda mbele bila kujali
lolote. Mwanasayansi aliyemweleza haya anamwita Msafiri, ahangaikaye. Kwa mujibu wa
nadharia ya umuundoleo, mwandishi ameweza kutoa sifa ambazo mkombozi anatarajia awe nazo
iwapo angetarajia kufaulu katika juhudi za kuikomboa jamii yake. Mkombozi alitakiwa ajue
kuwa alikuwa akipambana na mfumo ambao ulikuwa umeendelea sana kimawazo na
kiteknolojia. Hivyo basi na yeye lazima aweze kuwa mwingi wa hekima na ufahamu wa mambo
mengi.

22

MBURU C. KIARIE

Msafiri anaelezwa kuwa ili afike kwa P.P ilibidi apitie sehemu mbili kwanza; Jengo la Mefu
na Jengo la Pembetano. Alifika palipokuwa na nyumba ya ajabu. Nyumba iliyokuwa na kuta za
vioo tupu vya ajabu ambayo ilifunguka ukuta mzima. Vitu vilifanya kazi kwa kuashiriwa kwa
ishara fulani za mikono kama milango kufunguka, bomba la maji kufunguka na kufunga.
Akaonyeshwa mashine ya kukosha vyombo na kuvipangusa, kuvipanga na kuvichukua. Dhamira
ya mitambo hii ni kumfanya bina-Adamu ajitosheleze bila ya usumbufu wa kuingiliana na
wengine kila mara na kuharibu wakati mwingi akiongea. Waliekea hatua nyingine ya ukimya
kama siri ya teknolojia. Fasili ya haya kulingana na nadharia ya utafiti huu ni kuwa, ili
mkombozi amfikie kuelewa utawala wa Marekani lazima kwanzo aelewe utendakazi wa shirika
la fedha ulimwenguni lililona makao yake Marekani na pia yaliyokuwa yakiendelea katika jengo
la Pentagon analoliita jengo la pembe tano. Anabainishiwa ukweli kuwa maendeleo ya
kitenkolojia sio tu ya kurahisisha maisha ya mwanadamu bali yalilenga kukuza ubinafsi.
Alipoondoka kule alikumbana na kikundi cha waombolezaji waliofanya duara wakilia.
Katikati ya mduara alikuwa X aliyekuwa amekufa. Yasemekana alikuwa amepigwa risasi nyingi
ajabu kwa kudhaniwa kuwa mwizi. Kuwa yaliyompata yalitokana na kubaguliwa kwa kuwa
alikuwa mweusi. Alifahamishwa na mwenyeji wa pale namna babu zao walivyofika kule kwa
kusafirishwa katika chombo cha AMISTADI 1 kwa kulazimishwa. Nao baada ya vita vya
kikabila wakakimbilia huku wakidhani kulikuwa Pepo na wakakuta kuwa kulikuwa Bustani ya
Pili kama alivyowaeleza P.P. Wakapewa Kadi za Kijani na kuyafurahia maisha katika ndoto.
Kisha maisha yakabadilika na wakatengwa na kuitwa wezi, wabakaji, na kutuhumiwa kwa
kuhamisha magonjwa ya kwao huko. Mwenyeji akamfahamisha kuwa P ya kwanza ya P.P ni
Peter ila hakukumbuka P ya pili ilisimamamia jina gani. Anafunga safari kuelekea upande wa juu
alikofahamishwa angempata P.P pale tunapoelezwa kuwa;
Nilikusanya virago vyangu na kuondoka kuelekea upande wa juu. Nilipoanza safari
yangu, alipaaza sauti kuniambia maneno fulani lakini yalimezwa na upepo wa mbisho
uliakuwa ukipiga(Wamitila, 2002, Uk.135)
Kwa kuongozwa na nadharia ya utafiti huu Bustani ya pili ya Eden hapa iliwakilisha mataifa
ya ughaibuni yaani Marekani na Uingereza na mataifa mengine ya Uraya ambapo Waafrika
huenzi kufika huko kwa matumaini ya kupata maisha bora kuliko ya huku Afrika. Utawala wa
23

MBURU C. KIARIE

Marekani ulibuni sera ya kuwachuja na kuwabagua waafrika kwa kuanzisha mpango wa kuwapa
wahamiaji kadi za kimajano. Hata waafrika waliyokuwa huru baada ya utumwa hawa kuwa na
bahati kwani walibaguliwa vilevile kwa kuwa weusi.
18. Safari kuelekea Jengo la Mefu na la Pembetano
Safari inatukia katika Uk.136-143. Msafiri anaelekea lilipokuwa jengo kuu na alipokaribia
alisikia sauti za watu waliokuwa wakiimba kwa sauti za kuomboleza wakililia shida alizokuwa
nazo, rubo ina matatizo, shilingi inafifia, wameinyonga pesos, SAPS zinawasapa uhai, Dola
inawakaba shingo na Yen ni kamba ya kitanzi. Kisha akatokea sehemu iliyokuwa na kikundi
kilichopiga kelele na kusongamana na kubananabanana. Walikuwa na vibendera mikononi.
Palikuwa na mlinzi aliyemjia na kumkaribisha kama walivyowakaribisha wageni kutoka
Marekani ya Kusini, Asia, Uropa na Afrika atokako Msafiri. Kwa mujibu wa nadharia ya
umuundoleo, fasili ya haya ni kuwa mwandishi anaelezea taratibu za nchi zenye uwezo za
kiuchumi ambazo hutumiwa na mataifa haya kuhakikisha kuwa maslahi ya mataifa hayo
yanaimarika dhidi ya chumi za mataifa yanayoendelea. Nia yao ikiwa kuhakikisha wamedhibiti
uwezo na hatua ya maendeleo ya nchi zinazoendelea ili zizidi kutegemea misaada na ufadhili wa
mataifa hayo yenye uwezo huku raia wa wataifa hayo yanayoendelea wakiumizwa kiuchumi na
taratibu hizo. Msafiri anaeleza kuwa:
Kadiri tulivyoendelea kusongea mbele ndivyo ile sauti ya watu waliokuwa wakipiga
kelele ilivyofifia. Hatimaye tulifika mbele ya lile jengo. Kulikuwa na maandishi
yaliyoandikwa kwa rangi ya fedha: Jengo la Mefu (Wamitila, 2002, Uk.140)
Jengo alilofahamishwa kuwa hapo ndipo palipitishwa maamuzi muhimu na watu hufika huko
kuwasilisha matatizo yao. Ndani ya jumba palikuwa na jamaa anayeshughulikia masuala ya
kifedha. Msafiri alifahamishwa kuwa mlitokea jamaa fulani kutoka jengoni mle aliyekuwa na
kiburi ila lugha yake ilibadilika kila mara atokeapo mle. Alielezwa namna jamaa huyu
hushindwa hata kutamka [Link] alitamka [Link]-Adamu. Alifahamishwa kuwa
mle ndani mlikuwa na mtambo uliotumiwa kupima uzani. Upande wa kushoto mlikuwa na
Dollar na fedha nyingine ziliwekwa upande wa kulia. Jamaa aliyekuwa msimamizi wa fedha
akiona uzani wa fedha nyingine unaongeza uzani aliwafahamisha wakuu wake. Yaani shughuli
aliyoiita balance of power jambo ambalo halikumpendeza Peter P. Mlikuwa na suala la masoko
24

MBURU C. KIARIE

ya bidhaa za viwandani, sehemu za kusuluhishia tatizo la ajira, na wauza zana za vita. Msafiri
alifahamishwa uwepo wa stadi wa nyimbo mle jengoni. Ila nyimbo zake hazikuimbwa na
wengine kwani wengi waliimba Wimbo wa Mefu. Anaelekezwa pale anampata Peter P. Fasili ya
haya kulingana na nadharia ya umuundoleo nikuwa, Mkombozi alirejeshwa Marekani
kuonyeshwa uwezo ambao nchi hii ilikuwa nao dhidi ya mataifa mengine ulimwenguni. Kwani,
kutoka kikao chake cha Pentagon, Marekani iliweza kuathiri biashara ulimwenguni na usalama.
Jambo lililofanya mataifa kufuata mamuzi yake kuhusiana na miongozo ya kiuchumi
inayotolewa na Shirika la Fedha Ulimwenguni bila kupinga. Yaelezwa kuwa mahitaji ya mataifa
yote waliyohitaji misaada ya kifedha yalifanyiwa hapa na maamuzi kuhusu nguvu za kimataifa
kifedha pia yaliamuliwa.
Msafiri anafuata ujia mwembamba unaotokea palipokuwa na njia panda, moja nyembamba
na nyingine pana. Akafuata iliyokuwa pana huku akipigwa ngoto na mwelekezi wake
asiyeonekana kwa kushindwa hata kuwatambua wale huntha na kwa kupoteza muda. Msafiri na
mwelekezi wake wanapita katika msitu uliokuwa umeshikamana ajabu. Wakaelekea aliposikia
sauti na kuwaona watu waliokuwa wakiburura mifuko mikubwa kuelekea sehemu ya chini.
Kijana aliyekuwa akiamrisha alimfahamisha kuwa walikuwa wakisafirisha zana za vita kwenda
kuuza kwani walikuwa wamesikia kuna familia kadha ambazo zilikuwa zikigombana na
wanaamini karibuni watapigana hivyo walitaka kuliwahi soko. Kwa mujibu wa nadharia ya
umuundoleo, vita vingi vipatikanavyo katika nchi za kiafrika na kwingineko ulimwenguni
hutokana na urahisi wakupatikana kwa zana za vita ambazo huuzwa na mataifa yalionauwezo wa
kiusalama kama Marekani. Kijana yule anatoweka kiajabu na kilichobaki ni vicheko vya kike.
Msafiri anamua kukimbia kuelekea upande aliosikia vicheko na akatokeza sehemu iliyokuwa
wazi. Yule kijana akamtokeza tena na kumuashiria amfuate. Msafiri anaeleza kuwa:
Yule kijana niliyemwacha huko nyuma alitokeza tena na kuniashiria nimfuate. Nilipinda
kulia na kufuata ujia uliokuwa mwembamba ajabu. Hatimaye tulitokeza mahali
palipokuwa na jengo kubwa lenye muundo wa pembe tano..(Wamitila, 2002, UK. 147)
Jengo likiitwa Jengo la Pembe Tano. Alifahamishwa kuwa mle mlinywewa pombe na kuna
jamaa ambaye kila akitoka alirongonya maneno kama mlevi. Kwani, alishindwa kutamka
binadamu na kutamka binyabina-Adamu. Panatokeza askari mwenye bunduki na kila mmoja
25

MBURU C. KIARIE

anatimua mbio kuyaokoa maisha yake. Kwa mujibu wa nadharia ya umuundoleo, mwandishi
hapa anarejelea jengo la Pentagon kule Marekani ambalo huwa jumba la kitawala
linaloshughulikia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa ndipo mipango ya kudhulumu na
kukandamiza nchi nyingine kiulinzi hupangiwa nakutekelezwa. Yote yakilenga kuweka maslahi
ya usalama wa wamarekani mbele ya usalama wa wanandamu wengine ulimwenguni. Marekani
hutumia uwezo wake mkubwa wa kiulinzi kukandamiza (binya binadamu) mataifa ambayo
yanaelekea kuwa na mitazamo tofauti na yanayopinga na kuelekea kutishia matakwa ya
Marekani.
19. Safari ya kukutana na Peter Pan
Safari hii inatukia Uk. 144-156. Msafiri anatokea mahala palipokuwa tambarare. Huko mbele
kulikuwa na kitu kama kichuguu na palikuwa na jitu lililokuwa limeketi hapo. Mbele
akapungiwa mkono na mtu aliyefanana na Hanna. Mbele ya lile jitu kulikuwa na watu
waliosimama hatua kadha. Walikuwa watu wa rangi za kila aina na wenye nywele za kila aina
kuanzia za kipilipili hadi za kisinga. Mmoja wao alikuwa Hiro na kulikuwa na wengine
walioonekana kumtambua lakini hakuwatambua akiwemo kijana aliyekuwa amebebwa na kigari
cha kubebea vitu vya duka. Wote waliangalia mgongo wa lile jitu huku wakiimba wimbo
uliosifia nchi yao na kusifia lile jitu. Jitu lilikuwa likila humberger na chembe chembe
kuwaangukia wale waimbaji. Lilikuwa na uso wa mtoto na macho ya mtoto mdogo sana.
Mwewe mkubwa aliyekuwa ameninginiza bapa lenye maandishi El plurisbus Unum (Katika
wengi mmoja) alizunguka hewani. Fasili hapa kulingana na nadharia ya umuundoleo ikiwa
mataifa ya ulimwengu kutoka mabara tofauti walikuwa nyuma ya utawala wa nchi ya Marekani
ambayo bendera yake na ngao yake ya utawala iliyo na picha ya mwewe na maandishi ya El
Plurisbus Unum zikipepea.
Alifahamishwa na mwenzake asiyeonekana kuwa jitu lile lilikuwa Yanguis au Mjomba na
kuwa alikuwa mdogo juzi lakini baada ya FUJO ASILIA ipite aliishia kuwa vile. Hakuwa na kazi
nyingine ila kubugia vyakula tu. Alijulikana pia kama Peter Pan; yaani P.P. Msafiri vilevile
alielezwa kuwa imeandikwa kuwa watoto wote wanakua isipokuwa Peter Pan. Ambaye alipenda
kurusha mawe kama ilivyo kawaida ya watoto. Toto hili liliposimama lilikuwa na urefu wa ajabu
hivi kwamba, Msafiri hakuweza kuona sura yake. Lilipoongea kulirindima kila mahali.
26

MBURU C. KIARIE

Lilimtambua Msafiri na nia yake ya kuliona. Lilipotaka kujua ataambia wengine nini kulihusu,
aliasema kuwa watu walifanya kosa kulipa sifa za umungu. Jitu lilicheka kicheko cha ajabu,
kicheko cha kuambukizana hivi kwamba wote walicheka. Jitu lilikiri kuwa itakuwa vigumu
kupambana nalo kwani limewaingia akilini kabisa, linahisika kwingi hata lisikokuwako na
kutokuwako kwalo ndiko kuwako kwalo. Likamuuliza angesemaje kuhusu wasichana-wavulana
na likatoweka.
Nadharia ya umuundoleo hapa inatuongoza katika kulinganisha Marekani na mhusika Peter
Pan au The Boy Who Wouldnt Grow Up, aliyebuniwa na msanii mwandishi wa riwaya ya
Kiskotishi, J. M. Barrie (1902) The Little White Bird, kama kijana mkaidi ambaye alikuwa na
uwezo wa kupaa angani lakini ambaye hakuzeeka bali daima alibaki akiwa kijana mvulana
mdogo. Mvulana huyu mkorofi alitumia wakati wake wote kuzuru sehemu tofauti katika kiziwa
cha Neverland akiongoza kikundi cha kihuni kilicho jiita Lost Boys. Mhusika huyu vilevile
ametumiwa riwaya na Geraldine McCaughrean (2006) na katika kipindi cha Televisheni cha
Neverland kule Uingereza mwaka wa 2011. Huenda nchi ya Marekani na Peter Pan kutokana na
namna nchi nii inavyoingilia maswala ya nchi nyingine na kuzua fujo miongoni mwa mataifa
yasiyoiunga mkono. Vilevile nchi ya Marekani inalinganishwa na mhusika ambaye ametumiwa
katika picha za vibonzo kama Square (2005) kama jitu kubwa lipiganalo vita kwa kutumia shoka
kubwa. Kwa hivyo Marekani ni nchi iliyokubwa kiuwezo na yenye nguvu lakini iliyo na ukaidi
na ukorofi wa kitoto kidogo kilichokataa kukua kutoka utotoni. Yaani ni nchi iliyona ukaidi na
uchokozi kama mtoto mtundu asiyewaheshimu wengine.
Baada ya jitu kutoweka Msafiri akajaribu kukimbia kuwafuata wale wasichana-wavulana
ambao alielezwa kuwa ndio wale huntha aliowasaka lakini akazuiwa na Mzee wa Zakongwe.
Mzee alimfahamisha kuwa wanatokeza katika matendo na fikira kama Msafiri mwenyewe na
majina yao yalikuwa Abubepar, Binberu na Mwajihawaa na kuwa walikua wamekwenda kote na
hata kuwacha watoto huko. Mzee huyu alimfahamisha kuwa lazima awasake na wenzake ambao
walikuwa Mwanakabila, Binrangi, Mkengeushi kati ya wengine aliowasahau. Tukiongozwa na
nadharia ya utafiti huu tunaweza kusema kuwa wale huntha watatu ambao Mkombozi alitakiwa
kuwatambua na kuwaelewa walikuwa ni Ubepari, ubeberu na hawaa za ulimwengu. Mambo
haya ndiyo chanzo cha matatizo yaliyokikumba kijiji chake Mkombozi. Lakini yalikuwa na
27

MBURU C. KIARIE

wenzao ambao walikuwa ni Ukabila, Ubaguzi wa rangi, na Ukengeushi ulikuwa umekita mzizi
miongoni mwa wenyeji wa kijiji cha msafiri ambacho kinawakilisha nchi yeyote ile ya Kiafrika.
Anasikia sauti ya chini ikitangaza kuharibika kichwa kwa jagina aliyeyaongoza maandamano
dhidi ya wafidhuli wa nchi yao. Kuwa alifanya kosa kumdharau rais mtu aliyekuwa na uwezo
mkubwa kwa kumfananisha na ngedere aharibuye mahindi shambani na kuwaacha wengi
wakiomboleza. Kuwa Jagina alikuwa amedungwa sindano ya zebaki na kuwa hakuwa na bahati
kwani Mamanchi alikuwa ameaga na angempa dawa. Msafiri aliongea na kuwahimiza kuwa
walikuwa na uwezo na kuwa wasijidharau na wawaelimishe wengine. Ikawa kuwa, hata jicho
lake la kushoto halikufunguka tena. Mwisho wa safari hii Msafiri alikuwa amerejea kutoka safari
katika kitovu cha kiini cha kijiji na huu unakuwa piani mwisho wa riwaya unatukia hivi:
Nilijiangalia na kuangalia nilikokuwa. Nilikuwa nimepiga hatua chache kutoka mahali
palipokuwa na lile gogo. Mkononi nilikuwa na kifimbo kidogo na mkoba niliotoka nao
nyumbani kabla ya kuamua kuja huku. Huku mbali niliwaona watu wakinisongea
polepole; watoto walikuwa wakikimbia kunijia. Nilisikia kicheko cha wasichanawavulana. Je, hii ni ndoto au ni uhalisia? nilijiuliza, halafu nikasema kwa sauti ya juu:
Tahadhari, bina-Adamu! (Wamitila, 2002, Uk. 156)
Ufasili tunaoweza kuupata hapa tukiongozwa na nadharia ya umuundoleo ni kuwa
Mkombozi alikuwa ametembezwa au kufahamishwa mengi yanayohusu maeneo mbalimbali ya
ulimwengu. Hii ilikuwa njia ya kumwaandaa na kumuhami na ufahamu wa yanayohitajika
kufahamika katika juhudi zake za kuikomboa jamii yake. Ni dhahiri kuwa hangeweza kuleta
ukombozi uliptarajiwa akiwa peke yake. Ukombozi ungepatikana tu iwapo mataifa ya Afrika
yataungana, kuelimishana na kuwa na msimamo mmoja wa namna ya kujitetea dhidi ya
kuingiliwa na kudhulumiwa na viongozi wake na tawala za nje zenye uwezo.
HITIMISHO
Utafiti huu umeonyesha kuwa motifu ya safari ni fani ambayo sio lazima ihusishe safari ya
moja kwa moja kuanzia mwanzo hadi mwisho wa hadithi bali kuwepo kwa safari mbalimbali
tofauti zilizounganishwa na kusudi sawa. Uwepo wa safari tofauti tofauti unawezesha kupanuka
kwa maeneo ya kushughulikiwa na mwandishi kama kumfikisha mhusika katika nchi tofauti na
za mbali na hapo kufaulu kuleta pamoja mambo mengi pamoja katika hadithi moja. Safari hizi
tofauti zilizopo zinachangia kukamilika kwa safari kuu iliyohusu ukombozi wa jamii na
28

MBURU C. KIARIE

ulimwengu kwa jumla ambapo kila safari ilibeba dhana tofauti ya uhitaji wa ukombozi. Utafiti
pia kupitia nadharia ya umuundoleo umeonyesha namna binadamu kupitia maelezo ya hali ya
maisha ilivyo kuwa kabla ya ujio wa ukoloni, maisha katika wakati wa ukoloni na jinsi hali
ilivyokuwa baada ya ukoloni hadi kufikia sasa. Ufasili wa yaliyomo riwayani umeonyesha kuwa
hali ya maisha ilivyobadilika katika awamu hizi tatu kisiasa, kiuchumi, kiteknolojia na kijamii
hasa mateso yaliyowakumba watu ulimwenguni na yanayoendelea kuwakumba kutokana na
mabadiliko hayo. Mwandishi amefanya hivi katika juhudi yake yakumpatia msomaji picha
kamili ya binadamu kufikia sasa.
MAREJELEO
Casano, A (2014). Motif in Literature, Examples & Quizs. Education Portal. Retreived from
http/[Link]/sanjose/business-rew/.
Ndamburo E.F. (2013) Taathira Katika Fasihi. Retrieved from J:\[Link]
KATIKA [Link].
Wamitila, K. W. (2002). Bina-Adamu! Nairobi. Phoenix Publishers Ltd.
___________ (2008) Kanzi Ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. [Link]- Muwa
Publishers Ltd.

29

You might also like