Makampuni ya mawasiliano ya China yanayoonyesha teknolojia na bidhaa zenye ubunifu kwenye tamasha la AfricaTech 2024 nchini Afrika Kusini, yamejiwekea malengo makubwa ya kupanua wigo katika soko la Afrika linalokua kwa kasi.
Tamasha hilo linalofanyika kuanzia Novemba 12 hadi 14 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Cape Town, ni tukio kubwa zaidi la mawasiliano na teknolojia barani Afrika na limevutia wahudhuriaji 15,000, waonyeshaji zaidi ya 300, na wasemaji 450 kutoka barani Afrika na sehemu nyingine duniani.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia za kidigitali wa Afrika Kusini Bw. Solly Malatsi ametoa wito kufanyika kwa juhudi za pamoja kuendeleza mustakabali wa kidijitali barani Afrika.
Kampuni ya Tehama ya China Inspur inashiriki kwa mara ya kwanza kwenye tamasha hilo na kuonesha matumaini kuhusu ukuaji wake barani Afrika.